Isimu

Isimu (au "maarifa ya lugha") ni sayansi inayochunguza lugha. Imegawiwa katika matawi mbalimbali:

Marejeo

  • TUKI 1990, "Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha", Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
  • Massamba, David 2004, "Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha", Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Tazama pia

  • Lango la lugha
Globe of letters.svg Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Isimu kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Jina

Jina ni neno au maneno ambayo wanapewa watu, wanyama, nchi, vitu n.k. kwa ajili ya utambulisho.

Kitenzi

Kitenzi ni istilahi ya sarufi kwa maneno yanayotaja matendo kama vile kufanya, kwenda, kulala, kupiga, kuishi na kadhalika.

Lugha nyingi zinatumia vitenzi ingawa kuna pia lugha zisizoweka tofauti kati ya vitenzi na majina.

Lahaja

Lahaja ni vilugha vidogovidogo vya lugha moja ambavyo hubainishwa na jamii au jiografia.

Lahaja za lugha moja zinatofautiana katika matamshi, miundo ya sarufi na msamiati.

Kama lugha hutofautiana katika matamshi tu, tofauti hizo huitwa lafudhi, si lahaja. Uchambuzi na uchanganuzi wa lahaja ni tawi la isimujamii.

Lahaja hutofautishwa kulingana na vipengele vifuatavyo:

vipengele vya sera (lahaja rasmi na lahaja sanifu)

vipengele vya maoni ya wasemaji wa lugha husika

vipengele vya kijamii (lahaja jamii na lahaja tabaka)

vipengele vya eneoMfano wa lugha yenye lahaja mbalimbali ni Kiingereza na lahaja zake zinavyozungumzwa tofauti Uingereza, Marekani, Uhindi, Australia na maeneo mengine.

Lugha

Lugha (kutoka neno la Kiarabu: لغة) ni utaratibu wa kuwasiliana kati ya binadamu (wengine wanadai hata kati ya viumbe wenye akili).

Somo la lugha linaitwa maarifa ya lugha au isimu.

Mwaka wa 2008 ulikuwa Mwaka wa Lugha wa Kimataifa.

Mzizi

Kwa matumizi mengine ya jina hili angalia MiziziMzizi katika isimu ni sehemu muhimu sana ya neno ambayo haibadiliki hata kama neno litafanyiwa uambishaji, ukanushi, unyambulishaji na kadhalika. Sehemu hii ikibadilika, hata dhana ya neno hilo hubadilika.

Mfano mzizi wa neno "Analima" ni "Lim". Hii hutokana na kuchukua neno na kisha kulitafutia shina lake (kitenzi) na kisha kuondoa kiambishi tamati "a".

Nomino

Nomino ni aina ya neno linalotaja jina la kitu, mahali, mnyama, mtu, sifa au wazo.

Nomino hutokea kwa umbo la umoja au uwingi: kitu, vitu; mtu, watu.

Nomino pamoja na kitenzi hufanya sentensi: mtu anatembea.

Nomino za wingi

Nomino za wingi ni maneno yanayotaja majina ya vitu vinavyopatikana katika wingi tu, basi. Vitu hivyo haviwezi kutenganishwa katika kimojakimoja na kikatajwa kwa jina lake la pekee.

Mifano

Maji

Mchanga

Sukari

Chumvi

Sarufi

Sarufi ni elimu ya kupanga maneno kwa ufasaha. Maelezo hayo yanaweza kutafsiriwa kwa namna mbili tofauti.

Kwanza, yanaweza kutafsiriwa kwa maana ya ufunzaji wa vipengele kama msamiati, utungaji wa sentensi, viashiria, vitenzi na kadhalika. Hapa kuna mambo kama methali, hadithi, vitendawili, itikadi na kadhalika. Basi huachiwa mbali.

Tafsiri ya pili ya maelezo haya huchukua yote yafunzwayo katika lugha fulani. Kama maelezo ya awali, sarufi ina vipengele tofauti tofauti. Ikiwa pamoja na kufunza maneno magumu, vitenzi, nyakati, matamshi, ngeli, vivumishi, majina, vielezi na viingizi. Tena, sarufi ni tawi la isimu.

Vihisishi

Vihisishi ni maneno yanayodokeza vionjo au miguso ya moyo au ya akili.

Vionjo vya moyo huweza kuwa vya furaha au huzuni.

Maneno hayo kwa kawaida hupewa alama ya mshangao (!), au hutengwa kwa mkato (,) yatokeapo katika maandishi.

Mfano wa maneno hayo ni loo!, ebu!, la asha! n.k.

Kila kihisishi huweza kuibua hisia mahususi. kwa hiyo ni vyema kutumia kihisishi kinachofaa.

Viunganishi halisi

Viunganishi halisi (alama yake ya kiisimu ni: U) ni aina ya viunganishi ambavyo vinaunganisha vipashio vyenye hadhi sawa kisarufi. Yaani, kaka na dada, bibi na babu, n.k.

Vivumishi vya amba

Vivumishi vya amba ni maneno ambayo hurejelea nomino au kiwakilishi cha nomino ambayo imetajwa kwa kutumia mzizi wa amba- pamoja na o- rejeshi (urejeshi) inayorejelea nomino husika.

Mfano

Kikombe ambacho kilipotea

Mtoto ambaye anaumwa amepelekwa hospitali

Jembe ambalo limekatika mpini, litatengenezwa

Vivumishi vya kuuliza

Vivumishi vya kuulizia ni maneno yanayoulizia taarifa inayohusu nomino au kiwakilishi cha nomino.

Mifano

Mzee yupi anaumwa?

Miti mingapi imekatwa?

Unafanya kazi gani?

Chakula kipi ni kitamu?

Mwalimu yupi anafundisha vizuri?

Vivumishi vya sifa

Vivumishi vya sifa ni neno/maneno ambayo hutaja maana ya sifa ya nomino au kiwakilishi cha nomino jinsi kilivyo.

Mifano

Paka mwizi amelala jikoni

Ugonjwa hatari umeukumba dunia

Gari zuri limegongwa

Nyumba kubwa imejengwa bondeni

Kijana mpole kasusa kula

Vivumishi vya urejeshi

Vivumishi vya urejeshi ni maneno yanayotoa taarifa ihusuyo nomino au kiwakilishi cha nomino kwa kutumia kirejeshi kinachorejelea nomino ambayo imetajwa. Aina ya Vivumishi rejeshi ni “o” na “-amba”

Viwakilishi vya amba-

Viwakilishi vya amba ni neno/maneno yanayosimama badala ya nomino kwa kutumia mzizi wa amba-.

Mifano

Ambaye amemaliza aje

Ambalo lina kutu litatupwa

Ambazo zimeiva zitaliwa

Ambayo imejengwa bondeni itabomolewa

Ambacho kina sumu kitatupwa shimoni

Viwakilishi vya idadi

Viwakilishi vya idadi/kiasi ni aina ya neno au maneno yanayojulisha idadi ya watu au vitu ambavyo havikutajwa majina. Idadi hiyo inaweza kuwa ya jumla au idadi hali/kamili.

Viwakilishi vya kuuliza

Viwakilishi vya kuuliza ni aina ya neno au maneno yanayosimama badala ya nomino iliyoulizwa.

Viwakilishi vya sifa

Viwakilishi vya sifa ni neno/maneno ambayo hutaja sifa - yanayosimama badala ya nomino inayosifiwa.

Mifano

Warefu wamesimama

Mzuri amepita

Kibaya kinajitembeza

Mpole amekuja

Mwelevu hukaa kimya

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.