Ibada

Ibada ni tendo la heshima ya hali ya juu linalotolewa kwa Mungu au miungu.

Inaweza kufanywa na mtu binafsi au na kundi, hasa likiongozwa na kuhani au mwingine aliyekubalika.

Dini zinaelekeza binadamu kufanya ibada inavyotakiwa.

Ibada inasisitiza ukweli wa yule anayetolewa heshima hiyo, kwa mfano kutokana na imani ya dini fulani.[1]Vilevile ukweli wa mtoaji kwa maana ibada lazima itoke moyoni: ndiyo sababu haiwezi kulazimishwa.

Neno la Kiswahili linatokana moja kwa moja na Kiarabu ambapo neno عبادة, ibadah, linahusiana na maneno mengine kama vile "utumwa", na linadokeza utiifu na unyenyekevu hasa kwa Mungu pekee, inavyodaiwa na Uyahudi, Ukristo na Uislamu.[2]

Ukristo unasisitiza uhumimu wa kumuabudu Mungu kama Baba kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu na kufuata ukweli uliofundishwa na Yesu Kristo.

Uislamu unaona ibada kuwa lengo lenyewe la uumbaji wa binadamu na majini.[3][4] Katika karne ya 13 mwanachuo Ibn Taymiyyah aliieleza ibada ni "neno pana linalojumlisha kila jambo ambalo Allah analipenda na anapendezwa nalo - lile usemi au matendo, ya nje na ya ndani".[5][6]

Wataalamu wa sosholojia wanaonyesha kwamba wasio na dini wanaweza wakaabudu mambo mengine kama vile timu ya mpira, chama cha siasa, taifa au wasanii mbalimbali.[7][8]

Katika Kiswahili neno linaweza kuwa na maana ya mazoea: "Kwake ulevi ni ibada".

Religion-Pearce-Highsmith-detail-1.jpeg
Sehemu ya mchoro Dini wa Charles Sprague Pearce (1896).

Tanbihi

  1. Nagata, Judith (Jun 2001). "Beyond Theology: Toward an Anthropology of "Fundamentalism"". American Anthropologist 103 (2).
  2. al-Qamoos al-Muhit
  3. Al-Qur'an 51:56.
  4. Kuhusu swalah tano, Mtume aliripotiwa kusema, Swalini kama munavoniona mimi nikiswali [Imepokewa na Bukhari] Aisha alipokewa kwamba alisema: (Mtume alikuwa akifungua Swalah kwa Takbiri na kisomo cha “Alhamdu lillaahi Rabbil ‘aalamiin”, na alikuwa akirukuu hakiinamishi kichwa chake na wala hakisimamishi sawa, bali alikikiweka baina ya hali hizo mbili. Na alikuwa akiinua kichwa chake kutoka kwenye rukuu, hasujudu mpaka alingane katika kusimama. Na alikuwa akisoma Atahiyatu katika kila rakaa mbili, na alikuwa akikalia mguu wake wa kushoto na akiusimamisha mguu wake wa kulia. Na alikuwa akikataza mkao wa Shetani (kukaa kama shetani) na alikikataza mtu kuiweka chini mikono yake katika kukaa kama vile mnyama wa kuwinda, na alikuwa akihitimisha Swala yake kwa kupiga Salamu) [Imepokewa na Muslim.]
  5. Majmu' al-Fatawa (10/149)
  6. https://www.al-feqh.com/sw/namna-ya-kuswali
  7. http://sydney.edu.au/news/84.html?newsstoryid=10384
  8. http://www.cf.ac.uk/socsi/undergraduate/introsoc/durkheim6.html
Icon-religion.png Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ibada kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Dini

Dini (kutoka Kiarabu اﻟدﻴن, tamka: ad-din) inamaanisha jumla ya imani ya binadamu kadhaa pamoja na mafundisho wanayotoa kuhusu yale ambayo wanayazingatia ama kuyasadiki, yaani mambo ya roho, kama vile kuhusiana na Mungu, maisha na uumbaji.

Ibada ni nguzo mojawapo iliyo dhahiri miongoni mwa dini kadhaa katika kuunganisha dhamira za mwenye kushika dini na mhimili wa imani, lakini dini inahusu pia mafundisho kuhusu maadili, mema na mabaya, imani na jinsi ya kushiriki katika jumuiya za waumini.

Kwa maana nyingine "dini" inataja jina kielelezo juu ya aina mbalimbali za imani jinsi inavyopatikana duniani, yaani jumuiya za kidini.

Hekalu

Hekalu ni jengo la dini mbalimbali, lakini si zote.

Nyingine zinaita maabadi yao kwa majina tofauti, kutokana na mtazamo wa msingi.

Kwa mfano katika Uislamu jengo la ibada linaitwa msikiti.

Huduma

Huduma inaweza kuelezea

Jina

Jina ni neno au maneno ambayo wanapewa watu, wanyama, nchi, vitu n.k. kwa ajili ya utambulisho.

Kaburi

Kaburi ni mahali pa kulaza maiti ya binadamu au mabaki yake.

Tendo lenyewe linaitwa mazishi au maziko na mara nyingi linaendana na aina ya ibada.

Linaweze kuwa na namna nyingi, kadiri ya utamaduni wa wahusika.

Kanisa kuu

Kanisa kuu ni jina la heshima la jengo la ibada la madhehebu mbalimbali ya Ukristo ambalo Askofu wa jimbo (dayosisi) fulani analitumia kwa kawaida kutekeleza kazi yake kama mchungaji mkuu wa waamini wake, kama vile kuhubiri na kufundisha Neno la Mungu, kutakasa watu kwa sakramenti na sala mbalimbali na kuwaunganisha wote katika kumfuata Yesu pamoja.

Kanisa la Kilatini

Kanisa la Kilatini (wakati mwingine "Kanisa la Kiroma") ni moja ya madhehebu yanayounda Kanisa Katoliki. Ndiyo kubwa kuliko yote (97% za waumini wote), likiwa na Wakristo zaidi ya bilioni 1 duniani kote.

Mengine ni Makanisa Katoliki ya Mashariki (3%) yanayofuata mapokeo na hasa liturujia kama ya Waorthodoksi lakini yakiwa na ushirika kamili na Papa wa Roma ambaye ndiye mkuu wa Kanisa la Kilatini, pamoja na kwamba ni pia mkuu wa Kanisa Katoliki lote.

Jina linatokana na kwamba kwa karne nyingi lugha pekee iliyotumika katika ibada zake ilikuwa Kilatini.

Kanisa hilo lote upande wa sheria linafuata Mkusanyo wa sheria za Kanisa, kumbe upande wa liturujia wengi wa waamini wake wanafuata mapokeo ya Kanisa la Roma, lakini wengine wanafuata mapokeo ya Ambrosi wa Milano, au yale ya Lyon, Braga, Toledo na ya mashirika mbalimbali ya kitawa (k.mf. Wakartusi na Wadominiko).

Hivi karibuni waamini waliotokea madhehebu ya Anglikana wameruhusiwa kuendelea kutumia baadhi ya matini yake katika ibada wakiwa sasa ndani ya Kanisa la Kilatini.

Liturgia

Liturgia (pia: liturujia na liturugia; kutoka Kigiriki λειτουργια, leiturgia, yaani huduma kwa umati wa watu) ni utaratibu wa ibada hasa katika Kanisa la Kikristo.

Wakati mwingine neno hili linatumika pia kwa muundo au utaratibu wa sala katika dini mbalimbali.

Kwa kawaida liturgia inamaanisha utaratibu maalumu unaoweka mpangilio wa sala, nyimbo, masomo na sherehe nyingine wakati wa ibada.

Taratibu zinatofautiana kulingana na imani, teolojia, historia na utamaduni wa wahusika.

Hivyo ndani ya Ukristo kuna taratibu mbalimbali ambazo matawi yake makuu ni:

liturgia ya Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki

liturgia ya Wakatoliki wanaofuata mapokeo ya Roma

liturgia ya madhehebu ya Uprotestanti wa asili (Walutheri, Waanglikana, Waprebiteri n.k.), tofauti na ubunifu wa yale ya Wapentekoste n.k.Kiini cha liturgia ya Kikristo ni zile ibada zilizoanzishwa na Yesu mwenyewe, hasa ekaristi.

Liturujia ya Canterbury

Liturujia ya Canterbury ni madhehebu yanayoendeleza mambo bora ya Anglikana ndani ya Kanisa la Kilatini.

Mwaka 2011 na 2012 Papa Benedikto XVI alianzisha majimbo matatu kwa Waanglikana walioamua kujiunga na Kanisa Katoliki kama makundi.

La kwanza lilianzishwa kwa wale wa Uingereza na Wales (lakini pia Uskoti), la pili kwa wale wa Marekani (baadaye liliongezewa wale wa Kanada), la tatu kwa wale wa Australia (halafu pia Japani). Jumla ya waamini ni 12,200, ambao wanazidi kuongezeka haraka chini ya mapadri 162, wengi wao wakiwa na ndoa.

Kila mojawapo linaongozwa na padri mwenye ndoa aliyewahi kuwa askofu wa Kianglikana, isipokuwa lile la Marekani ambalo limepewa askofu wa kwanza ambaye ni mseja.

Kabla ya hapo kulikuwa na parokia tu za namna hiyo huko Marekani na Kanada, zikifuata hati maalumu ya Papa Yohane Paulo II ya tarehe 20 Juni 1980,Tarehe 9 Desemba 2009, Benedikto XVI alitoa hati Anglicanorum Coetibus, iliyoweka taratibu za uanzishaji wa majimbo yasiyopakana na majimbo ya kawaida ya Kilatini kwa Wakristo wa namna hiyo, na kufikia mwisho wa mwaka 2015 parokia zote zilizoanzishwa kabla ya hapo isipokuwa 2 zimejiunga na jimbo la Kimarekani. Mkutano maalumu kwa ajili hiyo ulifanyika tarehe 8-10 Novemba 2012.

Kwa niaba ya Papa, Idara ya Ibada ya Kimungu ilipitisha the Book of Divine Worship kwanza kwa muda mwaka 1984, halafu moja kwa moja mwaka 1987. Kuanzia tarehe 29 Novemba 2015 nafasi yake imeshikwa na "Divine Worship: The Missal".

Ibada nyingine kwa ajili ya ndoa na mazishi zilipitishwa na idara hiyo tarehe 22 Juni 2012.

Liturujia ya Roma isiyo ya kawaida

Liturujia ya Roma isiyo ya kawaida ni taratibu za ibada zinavyotumika katika Kanisa Katoliki kufuatana na mapokeo ya Roma jinsi yalivyokuwa mwaka 1962.

Mabadiliko ya liturujia yaliyofanywa baada ya Mtaguso wa pili wa Vatikano (1962-1965), baadhi yakiwa halali na baadhi kinyume cha sheria za Kanisa, yalisababisha upinzani mkali kutoka kwa wapenzi wa taratibu za awali, ambazo kwa kiasi kikubwa zilipangwa na Papa Pius V baada ya Mtaguso wa Trento na kwa sababu hiyo pengine zinaitwa liturujia ya Trento.

Hatimaye mwaka 2007 Papa Benedikto XVI kwa hati Summorum Pontificum alipanua ruhusa ya kutumia taratibu hizo duniani kote kama namna isiyo ya kawaida ya liturujia ya Roma.

Madhehebu

Madhehebu (kutoka Kiarabu مذهب madhhab) ni mafundisho, maadili na matendo ya ibada yaliyo ya msingi katika dini fulani.

Hutumiwa pia kutaja makundi ndani ya dini fulani ambayo yanatofautiana bila ya kuvunja umoja wa msingi.

Historia inashuhudia hata leo kwamba madhehebu mbalimbali ya dini ileile yanaweza kushindana hata kupigana vita.

Misa

Misa ni adhimisho la ekaristi hasa likifuata mapokeo ya Kiroma.

Mbali ya ibada za mwanzo na mwisho, sehemu kuu ni mbili: Liturujia ya Neno na Liturujia ya Ekaristi. Ya kwanza inafanyika hasa mimbarini, ya pili altareni. Ndizo meza mbili ambapo Mungu Baba analisha wanae.

Mungu

Mungu ni jina lenye asili ya Kibantu linalotumika kwa yeyote anayesadikiwa katika dini mbalimbali kuwa na uhai wa hali ya juu.

Kati ya wafuasi wa dini hizo, wengi wanaona kuwa Umungu, kwa jinsi ulivyo au unavyofirika, haukubali mgawanyiko. Hasa katika Uyahudi, Ukristo na Uislamu wanasisitiza umoja wa Mungu kuwa ndio msingi wa imani yao. Kwao Mungu ni wa milele, anafahamu yote na kutaka hasa uwepo wa viumbe. Tena kwa hiari yake alipenda kujifunua kwa binadamu; kielelezo ni Ibrahimu/Abrahamu aliyefanywa rafiki yake na baba wa waamini wote.

Kuna dini nyingine zinazokubali kuwepo kwa miungu mbalimbali (wawili au zaidi). Hasa dini nyingi za jadi zinaamini wingi wa miungu. Dini kubwa duniani inayosadiki miungu mingi ni Uhindu. Pia katika sehemu za Afrika ya Magharibi ibada za miungu mingi zinaendelea hadi leo.

Muziki wa Kikristo

Muziki wa Kikristo ni muziki uliotungwa ili kutokeza imani ya Ukristo katika sanaa hiyo, kwa mfano katika kumsifu Mungu, kumshangilia Yesu Kristo, na kuomba msamaha wa dhambi.

Hivyo, tofauti na miziki mingine, lengo kuu si kuburudika na uzuri tu.

Namna zake ni tofautitofauti kadiri ya nyakati, madhehebu, utamaduni n.k. Mojawapo, kati ya zile za zamani zaidi, inaitwa muziki wa Kigregori, kwa sababu iliagizwa na Papa Gregori I itumike kanisani.

Matumizi makubwa zaidi ni yale ya ibada, ambapo waamini waliokusanyika wanaimba pamoja, mara nyingi wakiongozwa na kwaya na wakisindikizwa na ala za muziki.

Matumizi mengine ni wakati wa kutoa mahubiri na mafundisho hata barabarani.

Pengine yanafanyika makongamano maalumu kwa wapenzi wa muziki huo, na vilevile siku hizi unarekodiwa kwa vifaa vya teknolojia hata kwa matumizi ya mtu binafsi.

Mwaka

Mwaka ni kipindi cha takriban siku 365 katika Kalenda ya Gregori ambayo imekuwa kalenda ya kawaida kimataifa ikifuata mwendo wa jua.

Sanaa ya Kikristo

Sanaa ya Kikristo ni sanaa iliyokusudiwa kutokeza imani ya Ukristo katika uzuri wake. Mara nyingi hiyo inafanyika kuhusiana na ibada na majengo yanayotumika kwa ajili hiyo.

Kwa ajili hiyo inatumia mada na mifano ya Injili au vitabu vitakatifu vingine, lakini pia habari za maisha ya watakatifu.

Madhehebu karibu yote yanatumia sanaa za aina fulani kwa namna hiyo, ingawa mengine yanakataa uchoraji n.k.

Picha za Yesu ndiyo michoro ya kawaida zaidi, zikifuatwa na zile za Bikira Maria katika Kanisa Katoliki na yale ya Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki.

Kutokana na kujali na kustawisha aina zote za sanaa, Wakatoliki wameshika nafasi ya kwanza katika idadi ya vituo vilivyoorodheshwa na UNESCO kama Urithi wa Dunia. Kwa mfano, nchi nzima ya Vatikani imo katika orodha hiyo.

Wakatoliki katika Mtaguso II wa Vatikano (hati Sacrosanctum Concilium) walikiri kwamba muziki wa Kikristo ndio sanaa bora kuliko zote kwa sababu unahusiana zaidi na Neno la Mungu ambalo unalipamba kwa noti ili lieleweke na kugusa mioyo zaidi.

Uislamu

Uislamu (kwa Kiarabu: الإسلام al-islam) ni dini inayotokana na mafunzo ya Mtume Muhammad.

Wafuasi wa imani hiyo huitwa "Waislamu" na wanakadiriwa kuwa milioni 1,400 hivi. Hivyo ni dini ya pili duniani yenye wafuasi wengi baada ya Ukristo wenye wafuasi milioni 2,200.

Uislamu ni ile imani kuwa muumba ni mmoja tu kwa dhati na sifa zake. Nguzo nyingine za imani zinajengwa juu ya imani ya Mungu mmoja wa kweli, imani juu ya maisha baada ya kifo, imani juu ya Malaika wa Mungu, vitabu vyake na kudra na tafsiri ya vitendo ya imani hii ni: Sala, Zakah, Saumu na Hija.

Ukristo

Ukristo (kutoka neno la Kigiriki Χριστός, Khristos, ambalo linatafsiri lile la Kiebrania מָשִׁיחַ, Māšîăḥ, linalomaanisha "Mpakwamafuta" ) ni dini inayomwamini Mungu pekee kama alivyofunuliwa kwa Waisraeli katika historia ya wokovu ya Agano la Kale na hasa Yesu Kristo katika [[Agano Jipya]] ambaye ni mwanzilishi wake katika karne ya 1.

Dini hiyo, iliyotokana na ile ya Wayahudi, inalenga kuenea kwa binadamu wote, na kwa sasa ni kubwa kuliko zote duniani, ikiwa na wafuasi 2,400,000,000 (33% kati ya watu 7.274 bilioni), ambao nusu ni waamini wa Kanisa Katoliki na nusu ya pili wamegawanyika kati ya Waorthodoksi (11.9%) na Waprotestanti (38%) wa madhehebu mengi sana.

Karibu wote wanakubali Utatu Mtakatifu, yaani kwamba milele yote Mungu ni nafsi tatu zenye umoja kamili: Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Ni kwa jina lao kwamba mataifa yote wanahimizwa kubatizwa kwa maji, ili kuzaliwa upya, kadiri ya agizo la Yesu ili kuingizwa katika fumbo la Mungu pekee kupitia fumbo la kifo na ufufuko wake mwenyewe.

Kitabu kitakatifu cha Ukristo kinajulikana kama Biblia. Ndani yake inategemea hasa Injili na vitabu vingine vya Agano Jipya.

Wakati wa Mababu wa Kanisa misingi ya imani ya Ukristo ilifafanuliwa na Mitaguso ya kiekumeni namna inayokubaliwa na wengi kabisa kati ya Wakristo wa leo. Maungamo yao yanakiri kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu aliyefanyika mtu ili kuwaokoa binadamu. Baada ya kuteswa na kuuawa msalabani alizikwa ila akafufuka, siku ya tatu akapaa kwa Mungu akishiriki mamlaka ya Baba hadi atakaporudi kuhukumu waadilifu na wasiotubu, akiwapa tuzo au adhabu ya milele kadiri ya imani na matendo yao.

Hivyo, kati ya madhehebu ya Ukristo, karibu yote yanamkiri Yesu kuwa kwa pamoja Mungu kweli na mtu kweli: katika umoja na nafsi yake ya Kimungu zinapatikana sasa hali hizo zote mbili.

Yote yanamkiri kuwa Mwokozi wa watu wote, na kuwa ndiye atakayerudi mwishoni mwa dunia kwa hukumu ya wote, ingawa maelezo kuhusu jambo hilo yanatofautiana.

Vilevile yote yanamchukua kama kielelezo cha utakatifu ambacho - kwa msaada wa Roho Mtakatifu na wa sakramenti zilizowekwa na Yesu mwenyewe, kuanzia ile ya ubatizo - kiwaongoze ndani ya Kanisa katika maadili yao maalumu, kuanzia unyenyekevu na upole hadi upendo unaowaenea wote, bila kumbagua yeyote, hata adui.

Waanglikana

Waanglikana ni Wakristo wa madhehebu yenye asili ya Uingereza.

Katika karne ya 16 mfalme Henry VIII alitenga Kanisa la nchi hiyo na Kanisa Katoliki.

Baada ya farakano hilo, yalifanyika mabadiliko mbalimbali upande wa imani, ibada na sheria kuelekea Uprotestanti. Hata hivyo mwelekeo wa Kikatoliki uliendelea kuwepo, na bado una nguvu, hasa katika baadhi ya dayosisi. Hasa miaka hii ya mwisho mvutano kati ya pande hizo mbili umeongezeka hata kusababisha umoja kulegea.

Katika karne zilizofuata, kutokana na uenezi wa himaya ya Uingereza duniani, Anglikana ilienea sehemu nchi, na leo ina wafuasi wengi hasa Afrika (Nigeria, Uganda n.k.). Kwa jumla wanazidi milioni 80.

Majimbo yake 38 yanajitegemea, lakini yanaunda ushirika mmoja. Maaskofu wake wote wanakutana Lambeth kila baada ya miaka 10 chini ya Askofu mkuu wa Canterbury.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.