Historia

Historia (kutoka Kigiriki ιστορια, historia; pia "tarehe" kutoka Kiarabu تاریخ tarih kwa maana ya "historia": pia tena "mapisi") ni somo kuhusu maisha ya binadamu na utamaduni wao wakati uliopita.

Mara nyingi neno hilo lina pia maana ya maarifa yoyote kuhusu wakati uliopita, yawe au yasiwe maarifa ya watu (kwa mfano "historia ya ulimwengu").

Historia ni hasa mfululizo wa habari za mambo yaliyotokea pamoja na sababu zake.

Binadamu anaziandika ili kuelewa maisha yake, yaani ametokea wapi, amepata mafanikio gani na matatizo gani.

Historia inatufundisha kuishi: kumbukumbu za mambo ya zamani (vita, uhuru, viongozi na mengineyo) zinatuwezesha kuendelea vizuri zaidi.

Wanahistoria wanapata maarifa yao kutoka maandishi ya zamani (hasa kwa historia andishi), kutoka fasihi simulizi na kutoka akiolojia (hasa kwa historia ya awali).

Kurasa zinazohusiana

Hourglass.svg Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
2012

Makala hii inahusu mwaka 2012 BK (Baada ya Kristo).

Baada ya Kristo

Baada ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo (kifupi: BK) ni namna ya kutaja miaka ambayo imekuwa njia ya kuhesabu miaka inayotumika zaidi duniani.

Kila mwaka huhesabiwa kuanzia ule uliodhaniwa kuwa mwaka wa kuzaliwa kwake Yesu Kristo. Miaka iliyotangulia kuzaliwa kwake Yesu huitwa Kabla ya Kuzaliwa kwake Yesu Kristo au kifupi: KK.

Hisabati

Hisabati ni somo linalohusika na idadi, upimaji na ukubwa wa vitu.

Kwa ujumla linahusika na miundo na vielezo.

Hisabati linaundwa na masomo mbalimbali, kama hesabu, jiometria na aljebra.

Neno hisabati katika lugha ya Kiswahili limetokana na neno la Kiarabu حسابات (halisi: hesabu (wingi)).

Somo hili huweza kutumika kutatua matatizo mbalimbali, lakini hasa ni la msingi katika uelewa wa ulimwengu kisayansi. Hivyo hutumiwa na masomo mengine kama Fizikia, Jiografia, Kemia katika mafunzo yake.

Indonesia

Indonesia ni nchi ya visiwa katika Asia ya Kusini-Mashariki. Iko upande wa Kusini-Mashariki kati ya Bahari ya Uhindi na Pasifiki.

Visiwa vyake ni sehemu ya Funguvisiwa la Malay, ingawa Guinea Mpya kwa kawaida haihesabiwi katika fungu hilo.

Indonesia imepakana na Papua Guinea Mpya kwenye kisiwa cha Guinea Mpya, pia na Timor ya Mashariki kwenye kisiwa cha Timor, halafu na Malaysia kwenye kisiwa cha Borneo.

Nchi nyingine zilizo karibu ni Australia, Singapur na Ufilipino.

Italia

Jamhuri ya Italia (kwa Kiitalia: Repubblica Italiana) ni nchi ya Ulaya Kusini inayoenea katika sehemu kubwa ya Rasi ya Italia na baadhi ya visiwa vya jirani kwenye Bahari ya Kati.

Eneo lake ni km² 302,072.84 ambalo lina wakazi 60,483,973 (31-12-2017): ni nchi ya 23 duniani kwa wingi wa watu, lakini ya 8 au 9 kwa uchumi.

Imepakana na Ufaransa, Uswisi, Austria na Slovenia. Nchi huru mbili ndogo zinazozungukwa na eneo la Italia pande zote ni San Marino na Vatikano.

Makao makuu ni jiji la Roma, lenye umuhimu mkubwa katika historia ya dunia nzima.

Kabla ya Kristo

Kabla ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo (kifupi: KK) ni namna mojawapo ya kutaja miaka.

Hesabu hii imekuwa njia ya kuhesabu miaka inayotumika zaidi duniani siku hizi.

Kila mwaka huhesabiwa kuanzia ule uliodhaniwa kuwa mwaka wa kuzaliwa kwake Yesu Kristo. Miaka iliyofuata kuzaliwa kwake hutajwa kwa kuongeza Baada ya Kristo au kifupi: BK.

Kuhusu historia ya hesabu hii tazama:

Historia ya Hesabu "Kabla ya / Baada ya Kristo"

Kanisa Katoliki

Kanisa Katoliki ni jina linalotumika kwa maana mbalimbali, lakini hasa kumaanisha Kanisa la Kikristo linalokubali mamlaka ya kiroho ya Papa wa Roma kama mkuu wa urika wa maaskofu juu yake lote.

Ndilo kubwa kabisa kati ya madhehebu yote ya dini hiyo, likikusanya nusu ya wafuasi wote wa Yesu.

Hata hivyo, Wakristo wa madhehebu mengine wanaokubali kanuni ya imani ya Nisea-Konstantinopoli wanatafsiri tofauti sehemu yake inayokiri Kanisa la kweli kutambulishwa na sifa nne, ya tatu ikiwa kwamba ni katoliki: "Tunasadiki Kanisa moja, takatifu, katoliki, la Mitume".

Kanisa Katoliki, likiwa na miaka karibu elfu mbili, ni kati ya miundo ya zamani zaidi iliyopo duniani na imechangia kwa kiasi kikubwa ustaarabu wa Magharibi, ingawa tangu mwishoni mwa Karne za Kati athari yake inazidi kupungua, ilivyo wazi leo hasa katika masuala yanayohusu jinsia na uzazi.

Imani ya Kanisa hilo inatokana na ufunuo wa Mungu ulivyotolewa kwa Israeli na ulivyokamilishwa na Yesu ambaye alimtambulisha kama Baba na alilianzisha kwa njia ya Roho Mtakatifu aliyetumwa naye juu ya Mitume wake siku ya Pentekoste mwaka 30 (au 33) BK.

Ni imani inayoungamwa katika ubatizo, sakramenti ya kwanza na mlango wa sakramenti nyingine sita: kwamba Mungu ni mmoja tu katika nafsi tatu: Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.

Imani hiyo inatakiwa kutekelezwa katika maadili maalumu yanayotegemea hasa upendo ambao ndio adili kuu na uhai wa mengine yote.

Kutokana na juhudi za kutekeleza matendo ya huruma kwa yeyote mwenye shida, Kanisa Katoliki linatoa huduma za elimu na afya kuliko taasisi nyingine yoyote duniani kote.

Kama vielelezo vya utakatifu ambao waamini wote wanaitiwa, Kanisa linapendekeza watu wa Agano la Kale na wa Agano Jipya, hasa Bikira Maria, lakini pia wale waliojitokeza zaidi katika historia yake kama watakatifu.

Baadhi yao wana wafuasi wengi wanaounda familia za kiroho, mara nyingi kama mashirika ya kitawa yenye karama mbalimbali.

Kifaransa

Kifaransa (kwa Kifaransa: français) ni lugha ya Ufaransa (pamoja na maeneo yake ya ng'ambo), Ubelgiji ya Kusini, Uswisi ya Magharibi, Luxemburg na Kanada. Inazungumzwa pia katika nchi nyingi za Afrika kama vile Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Senegal, Mali, Shelisheli, Chad, n.k., Asia ya Kusini na Amerika zilizokuwa koloni za Ufaransa.

Maji

Maji ni kimiminika ambacho ni kiini cha uhai wowote duniani na pia kiini cha utamaduni wa binadamu. Hakuna mtu anayeweza kuishi bila maji kwa sababu asilimia 50 - 65 za mwili wa mwanadamu ni maji. Hata miili ya mimea na wanyama kwa kiasi kikubwa ni maji. Pia katika dunia maji yamechukua karibu robo tatu ya eneo lake lote (71.11%). Kwa hiyo maji ni kitu cha msingi sana.

Kiasi kikubwa cha maji duniani ni maji ya chumvi katika bahari; maji matamu yanayoweza kutumiwa na binadamu na kwa kilimo ni asilimia ndogo tu ya maji kwenye Dunia.

Maji yana matumizi mengi nyumbani na katika uchumi: nyumbani

maji hutumika katika kunywa, kuogea, kuoshea vitu na vyombo mbalimbali; kiuchumi maji yanatumika viwandani, kwa mfano kupoozea au kuoshea mashine, pia maji hutumika katika usafiri, kama vile meli za mizigo, za abiria na vinginevyo.

Katika matumizi hayo pengine watu hutumia vibaya maji na vyanzo vyake ambavyo ni muhimu vitunzwe kwa kuwa tukiharibu vyanzo hivyo twaweza kuleta hali ya jangwa katika eneo hilo.

Mkoa wa Hatay

Hatay ni mkoa uliopo kusini mwa nchi ya Uturuki, katika pwani ya Mediteranea. Kwa upande wa kusini na mashariki mwa mkoa huu, unapakana na Syria. Mkoa unawakazi wapatao 1,386,224. Wanaokalia katika eneo la kilomita za mraba zipatazo 5,403.

Mkoa wa Trabzon

Trabzon ni jina la mkoa uliopo katika pwani ya Bahari Nyeusi huko nchini Uturuki. Upo kwenye kanda muhimu kabisa, Trabzon ni moja kati ya bandari ya kibiashara ya zamani zamani sana katika miji ya Anatolia. Idadi ya wakazi wa hapa ni 1,061,055 (makadirio ya 2006). Mikoa ya jirani pamoja na Giresun kwa upande wa magharibi, Gümüşhane kwa upande kusini-magharibi, Bayburt kwa upande wa kusini-mashariki na Rize kwa upande mashariki mwa nchi. Mji mkuu wake ni Trabzon. Mkoa huu ndiyo nyumbani kwa jumuiya ndogo ya Wagiriki Wakiislamu wanaongea lugha ya Kipontiki .

Mto Wami

Mto Wami ni mto wa Tanzania mashariki, unaotiririka katika mkoa wa Morogoro hadi mkoa wa Pwani.

Chanzo chake ni katika Milima ya Ukaguru na unaishia katika Bahari Hindi magharibi kwa Zanzibar.

Beseni lake ni kubwa: km² 43,946.

Matawimto yake ni Mto Mkata upande wa kushoto na Mto Lukigura, Mto Mjonga na Mto Chogoati upande wa kulia.

Njia yake inaanza katika Hifadhi ya Mikumi, unakata barabara ya B 129 takriban kilomita 42 kutoka Morogoro. Unaendelea kuelekea mashariki ukipita barabara ya A 14 karibu na Mandera, unaendelea kupita Mvomero na kuishia baharini.

Mto huo umepita katika eneo la kambi ya magereza Mbigiri katika Dakawa. Huo mto husifika sana kwa uvuvi katika eneo hilo la Dakawa. Lakini huo mto unajulikana pia kwa kuwa na mamba wengi pamoja na viboko wakubwa.

Baadhi ya watu hutumia maji hayo kwa kunywa, kuogea, kufulia, kupikia pamoja na shughuli nyingine.

Rufiji (mto)

Rufiji ni mto mkubwa wa Tanzania. Chanzo kiko Tanzania ya kusini-magharibi katika maungano ya tawimito ya mto Kilombero na mto Luwegu.

Unafikia Bahari Hindi kwa njia ya delta yake takriban km 200 kusini kwa Dar es Salaam karibu na kisiwa cha Mafia. Urefu wa Rufiji ni takriban km 600.

Tawimto mkubwa katika beseni yake ni Ruaha Mkuu.

Mwaka 2005 daraja lilikamilika linalorahisisha usafiri kati ya Dar es Salaam na mikoa ya Lindi na Mtwara.

Shaka Samvat

Shaka Samvat ni kalenda rasmi ya kitaifa nchini Uhindi inayotumiwa huko pamoja na kalenda ya Gregori.

Tarehe

Tarehe (kutoka Kiarabu تاریخ tarih kwa maana ya "historia") ni namna ya kutaja historia, lakini kwa kawaida zaidi nafasi ya siku fulani ndani ya mfumo wa kalenda.

Kwa kawaida tarehe inarejelea kalenda ya Gregori. Lakini ilhali kuna kalenda mbalimbali inawezekana kutaja na tarehe tofauti kwa siku ileile kutegemeana na kalenda inayorejelewa.

Ufaransa

Ufaransa ni nchi ya Ulaya na mwanachama mwanzilishi wa Umoja wa Ulaya.

Mji mkuu ni Paris.

Eneo lake ni km² 674,843; na idadi ya wakazi ni 63,044,000.

Imepakana na Ubelgiji, Luxemburg, Ujerumani, Uswisi, Italia, Monako, Andorra na Hispania.

Ufaransa ulikuwa kati ya nchi zenye makoloni mengi ikasambaza lugha yake kote duniani na kutunza uhusiano wa pekee na nchi nyingine zinazotumia Kifaransa.

Uganda

Uganda ni nchi ya Afrika ya Mashariki. Imepakana na Kenya upande wa mashariki, Sudan Kusini upande wa kaskazini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo upande wa magharibi, Rwanda na Tanzania upande wa kusini.

Uganda inamiliki sehemu ya ziwa la Viktoria Nyanza ikipakana huko na Kenya na Tanzania.

Uganda ni nchi mwanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki na wa miundo mingine mbalimbali ya kimataifa.

Uingereza

Uingereza (pia: Ingilandi kutoka Kiingereza: England) ni nchi kubwa ndani ya Ufalme wa Muungano yenye wakazi milioni 50 (83% ya wakazi wote wa Ufalme) na eneo lake ni takriban km² 130,000 (theluthi mbili za kisiwa cha Britania).

Ujerumani

Ujerumani (pia: Udachi, kwa Kijerumani: Deutschland) ni nchi ya Ulaya ya Kati.

Imepakana na Denmark, Poland, Ucheki, Austria, Uswisi, Ufaransa, Luxemburg, Ubelgiji na Uholanzi.

Ni nchi yenye watu wengi katika Ulaya, isipokuwa Urusi ina watu zaidi.

Uchumi wa Ujerumani una uwezo mkubwa: ni nchi inayouza bidhaa nyingi nje kushinda mataifa yote ya dunia.

Muundo wake kiutawala ni shirikisho la jamhuri lenye majimbo 16 ndani yake na kila jimbo lina kiwango cha kujitawala.

Uturuki

Uturuki (Jamhuri ya Uturuki; kwa Kituruki: Türkiye Cumhuriyeti) ni nchi ya kimabara kati ya Asia na Ulaya.

Sehemu kubwa iko Asia ya magharibi lakini sehemu ndogo ya eneo lake upande wa magharibi wa Bosporus iko Ulaya.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.