Havana

Havana (kihisp. La Habana) ni mji mkuu na mji mubwa wa Kuba kwenye 23°8′N 82°23′W. Kuna wakazi milioni 2.2. Tangu 1982 mji wa kale umepokelewa katika orodha ya urithi wa dunia.

Jiji la Havana
Nchi Kuba
Picha:LaHabana.jpg
Havana wakati wa jioni
La Habana in Cuba
Mahali pa Havana nchini Kuba

Historia

Mji kwa jina la Havana ulianzishwa 1515 na Mhispania Diego Velázquez de Cuéllar lakini ulihamishwa mwaka 1519 kuja mahali pa kudumu uliopo hadi leo. Mji ukakua kuwa bandari muhimu wa kijeshi na kibiashara. Tangu 1607 Havana ilikuwa mji mkuu wa koloni ya Kihispania ya Kuba.

Havana ilikuwa hasa tangu azimio la Hispania la kukusanya "la flota" yaani jahazi za kubebea fedha na bidhaa za Amerika kama kundi kabla ya kuvuka Atlantiki kwa kusudi la kuzuia maharamia Waingereza waliovinda meli za Hispania. Azimio hili lilisababisha mamia ya jahazi kukusanyika katika hori ya bahari mbele ya Havana katika miezi ya Mei hadi Agosti mpaka kuanza safari ya pamoja.

Katika karne za 17 na 18 mji uliendelea kukua kuwa mji mkubwa wa tatu wa Amerika baada ya Mji wa Mexiko na Lima kushinda Boston na New York.

Mwisho wa karne ya 19 Havana iliona mlipuko wa manowari SS Maine katika bandari yake tarehe 15 Februari 1898 ulioanzisha vita ya Marekani dhidi Hispania. Havana ilivamiwa na Waamerika na kutangazwa kuwa mji mkuu wa Jamhuri ya Kuba mwaka 1902.

Athira ya Amerika iliendelea kuwa kubwa hadi mapinduzi ya Kuba na kuingia kwa jeshi la mapinduzi chini ya Fidel Castro tarehe 1 Januari 1959.

Air France

Air France (zamani iliitwa Société Air France, S.A.) ni shirika la ndege kuu la Ufaransa iliyo na makao makuu mjini Tremblay-en-France. Air France inasafiri hadi miji 150 kote duniani.

Air France ilianzishwa mnamo 7 Oktoba 1933 baada ya muungano wa kampuni za Air Orient, Air Union, Compagnie Générale Aéropostale, Compagnie Internationale de Navigation Aérienne (CIDNA), na Société Générale de Transport Aérien (SGTA).

Amanda Palmer (mwandishi habari)

Amanda Palmer (alizaliwa 1976) anaongoza uzinduzi wa Doha Tribeca Film Festival (DTFF) na ni Mkuu wa Burudani wa Al Jazeera ya Kiingereza.

Palmer alijiunga na DTFF kutoka Al Jazeera ya Kiingereza, ambapo kama Mkuu wa Burudani anaunda, na kutayarishwa, vipindi vya elimu na sanaa katika mtandao wa Al Jazeera. Kipindi chake cha "48" kilichochaguliwa kupata tuzo na kipindi cha "The Fabulous Picture Show," (FPS) kinachojulikana kote duniani vimemfanya ajulikane kama mtaalam wa utamaduni.

Kazi ya Palmer imesababisha watengezaji filamu wajulikane kote duniani. Kwa kujenga jukwaa la kimataifa la watengezaji filamu, Palmer amegundua talanta mpya na zinazoibukia ambayo imesababisha idadi ya wasanii wengi kupata fursa ya kuzungusha filamu zao. Katika kazi yake kwa jumla, Palmer hajawahi kusita kueleza changamoto anazopata ikiwa anarikodiwa kwa kamera au hata kazi yoyote nyingine isiyohitajiwa kurikodiwa. Baada ya kupokea shahada yake ya sanaa katika uandishi habari kutoka Chuo Kikuu cha Teknolojia mjini Sydney, Palmer alisomea maonyesho na muziki. Alianza kazi kama mwandishi habari wa kitaifa kwa mtandao wa Channel Seven nchini Australia kabla ya kuhamia jijini London na kuwa mwanamke mdogo zaidi kuwahi kufanya kazi kwenye stesheni iliyo Ulaya. Yeye kisha alihamia CNN na baadaye Associated Press TV kabla ya kujiunga na Al Jazeera ya Kiingereza mnamo Agosti 2005. Sasa yeye yumo katika Kamati cha Filamu Nchini Qatar.

Bandari

Bandari ni mahali pa kupokea meli na kuhamisha mizigo yao pamoja na abiria. Bandari inatakiwa kuipa meli kinga dhidi ya mawimbi makubwa na vifaa ya kupakiza au kutoa mizigo. Kuna mabandari asilia na mabandari yaliyotengenezwa kwa kusudi hii. Kwa jumla bandari ni sehemu muhimu za miundombinu wa nchi.

Mabandari hutengenezwa kando la bahari, maziwa au mito.

Kati ya sifa muhimu kwa ajili ya bandari ni

kina cha maji cha kutosha kulingana na ukubwa wa meli zinazoitumia.

mitambo kama winchi za upakizi

nafasi za ghala

njia za usafiri kama reli na barabara za kusafirisha mizigoMabandari hutofautiana kulingana na kusudi lao na aina za mizigo inayoshughulikiwa humo.

Mabandari madogo zinahudumia wavuvi au jahazi za burudani.

Kuna mabandari yanayopokea mizigo ya kila aina kama bandari ya Dar es Salaam au Mombasa.

Mara nyingi kuna mabandari yanayoshughulika mizigo maalumu kama mafuta, kontena, kivuko na kadhalika.

CNN

Cable News Network (Kifupi: CNN) ni stesheni ya runinga inayotangaza habari iliyoanzishwa na Ted Turner mnamo 1980. CNN ilikuwa stesheni ya kwanza inayotangaza habari masaa 24. Makao yake makuu yako mjini Atlanta, ingawa ina vituo vingine mjini New York, Washington, D.C. na Los Angeles. Kauli yake mbiu ni The Worldwide Leader in News.

Carlos Santana

Carlos Augusto Santana Alves (amezaliwa tar. 20 Julai 1947 mjini Autlán de Navarro, Mexiko) ni mshindi wa Tuzo ya Grammy, akiwa kama mwanamuziki-mpiga gitaa bora wa Kimexiko. Ameanza kujipatia umaarufu tangu kunako miaka ya 1960 na mwanzoni mwa miaka ya 1970 akiwa na bendi yake ya Santana Bendi, ambayo imejizolea umaarufu na mafanikio makubwa kwa muziki wao wa rock, blues, salsa, na jazz fusion.

Bendi imeingizia baadhi ya ala zake mwenyewe, yaani anapiga blues-besi gitaa iendanayo na muundo sawa kabisa na zile ngoma za Kilatini kama vile timbalesi na congasi. Santana aliendlea kufanya shughuli zake za kimuziki kwa takriba miaka kadhaa. Alipata umaarufu mkubwa sana kunako miaka ya 1990. Mwaka wa 2003, gazeti la Rolling Stone nao wamempa Santana namba 15 katika orodha zao za Wapiga Gitaa Wakubwa kwa muda wa miaka 100.

Danay García

Danay García (amezaliwa tar. 5 Julai 1984, mjini Havana, Kuba) ni mwigizaji filamu na tamthilia wa Kikuba. Kwa sasa anashiriki katika tamthilia ya Prison Break, na humu anacheza kama Sofia Lugo.

Eurowings

Eurowings GmbH ni kampuni ya ndege inayotoa huduma kwa bei nafuu nchini Ujerumani, yenye makao makuu huko Düsseldorf na inayomilikiwa kikamilifu na kundi la Lufthansa.

Ilianzishwa mwaka 1996 ikiwa kampuni ya mtu binafsi na tangu 2011 ni mali ya Lufthansa. Hutumikia mtandao wa vikomo yva ndani ya Ulaya pamoja na vikomo vya mbali nje ya Ulaya. Vituo vikuu viko kwenye uwanja wa ndege wa Berlin Tegel, uwanja wa ndege wa Cologne Bonn, uwanja wa ndege wa Düsseldorf, uwanja wa ndege wa Hamburg, uwanja wa ndege wa Hannover, uwanja wa ndege wa Munich, uwanja wa ndege wa Nuremberg, uwanja wa ndege wa Palma de Mallorca, uwanja wa ndege wa Salzburg, uwanja wa ndege wa Stuttgart, na Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Vienna.

Fidel Castro

Fidel Alejandro Castro Rúz(13 Agosti 1926 - 25 Novemba 2016) alikuwa kiongozi wa Kuba tangu mwaka 1959 hadi 2006 akiwa waziri mkuu hadi 1976 halafu rais wa nchi.

Hispania

Hispania (kwa lugha ya wenyewe: España, kwa Kiingereza Spain) ni nchi ya Ulaya ya kusini-magharibi. Imepakana na Ufaransa, Andorra, Ureno na eneo la Kiingereza la Gibraltar.

Kuna pwani ndefu ya Bahari ya Mediteranea na pia ya Atlantiki.

Hispania bara ni sehemu kubwa ya rasi ya Iberia. Visiwa vya Baleari kwenye Mediteranea na Visiwa vya Kanari katika Atlantiki pamoja na miji ya Afrika ya Kaskazini Ceuta na Melilla ni sehemu za Hispania.

Mji mkuu ni Madrid ambayo ni pia mji mkubwa wa nchi.

Eneo la nchi ni km² 500,000 nalo lina wakazi 46.733.038 (2018).

Mfalme Felipe VI amevaa taji mwaka 2014, akishika nafasi ya baba yake Juan Carlos I, anayeheshimiwa sana kwa sababu aliongoza taifa katika mabadiliko ya kutoka udikteta wa jenerali Francisco Franco kuelekea demokrasia. Hasa tendo la mfalme la kuzuia mapinduzi wa kijeshi linakumbukwa sana.

Muundo wa serikali ni Ufalme wa Kikatiba, hivyo kisheria madaraka ya mfalme ni madogo.

Utawala umo mikononi mwa serikali inayochaguliwa na bunge linaloitwa "Las Cortes likichaguliwa kwa kura za kidemokrasia.

Historia ya Hispania

Historia ya Historia inahusu eneo la Ulaya ambalo wakazi wake leo wanaunda Ufalme ya Hispania.

Juanes

Juan Esteban Aristizábal Vásquez (amezaliwa tar. 9 Agosto, 1972 mjini Medellín, Colombia) ni mshindi wa Tuzo ya Grammy. Colombia mwimbaji Juanes ni moja ya pop. Ni kuchukuliwa icon dunia kutokana na mafanikio ya muziki wake katika lugha ya Kihispaniola.

Junipero Serra

Junipero Serra, O.F.M. (jina la kiraia lilikuwa Miquel Josep Serra i Ferrer) alikuwa mtawa, padri na mmisionari wa Kanisa Katoliki. Alizaliwa Petra, Majorca, Hispania, tarehe 24 Novemba 1713, akafariki katika misheni ya San Carlos Borromeo de Carmelo, California, Nueva Espana, leo nchini Marekani, tarehe 28 Agosti 1784.

Alitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa mwenye heri tarehe 25 Septemba 1988, halafu na Papa Fransisko kuwa mtakatifu tarehe 23 Septemba 2015.Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 1 Julai.

Alianzisha misheni moja katika Baja California na nyingine 9 kati ya 21 za kwanza kati ya San Diego na San Francisco, Marekani. Walengwa wakuu wa misheni hizo walikuwa Waindio.

Kuba

-Kwa "kuba" (pia: kubba) kama sehemu ya jengo tazama Kuba (jengo)-

Kuba (pia: Kyuba; kwa Kihispania: Cuba) ni nchi ya kisiwani katika Bahari ya Karibi kusini kwa Marekani.

Nchi inajumuisha kisiwa kikuu cha Kuba ambacho ni pia kisiwa kikubwa cha Antili Kubwa) pamoja na kisiwa cha Isla de la Juventud na visiwa vidogo vingine vingi.

Kuba ni nchi kubwa kati ya nchi za Karibi yenye wakazi wengi.

Utamaduni wake unaonyesha athari za historia yake kama koloni la Hispania kwa miaka mingi, pia ya wakazi wenye asili katika watumwa kutoka Afrika na ya kuwa jirani na Marekani.

Kurusha kisahani

Mchezo wa kurusha kisahani ni fani katika riadha ambapo kisahani kizito kinarushwa kwa mkono wa mwanariadha kwa umbali mkubwa iwezekanavyo.

Asili ya mchezo huu ni Ugiriki ya Kale. Lengo ni kurusha kisahani mbali kuliko wadhindani.

Katika michezo ya Olimpiki ya Ugiriki ya Kale kurusha kisahani kulikuwa mashindano ya mara kwa mara. Sanamu za wacheza kisahani na picha zao kwenye vyungo vya kufinyangwa vimehifadhiwa hadi sasa.

Katika karne ya 19 mwalimu wa michezo Christian Georg Kohlrausch aligundua upya mchezo huu uliosahauliwa pamoja na wanafunzi wake mjini Magdeburg. Kutoka msingi huu kurusha kisahani kuliingia katika michezo ya Olimpiki ya kwanza ya kisasa mwaka 1896.

Leon Trotsky

Leon Trotsky (kwa Kirusi Лев Дави́дович Тро́цкий, Lev Davidovich Trotsky, ubini wa awali Бронште́йн, Bronshtein) alikuwa Myahudi wa Urusi (Yanovka, leo nchini Ukraina, 7 Novemba 1879 – Coyoacán, Mexico City, Meksiko 21 Agosti 1940) maarufu kwa mwanamapinduzi wa kikomunisti.

Baada ya kuwa kiongozi wa kwanza wa Jeshi Jekundu na kushiriki uongozi wa Umoja wa Kisovyeti, alishindana na Stalin akaondolewa madarakani (1927) na hatimaye kufukuzwa nchini (1929).

Akiendelea kupinga siasa ya Stalin kutoka Meksiko, aliuawa baada ya majaribio yake mengi kushindikana.

Ujumbe wake hasa ulikuwa kwamba mapinduzi yanatakiwa kuwa ya kudumu.

Madola

Katika mabara, lile lenye nchi nyingi zaidi ni Afrika likiwa na nchi au madola 54, likifuatiwa na bara la Ulaya likiwa na madola 48, kisha Asia likiwa na madola 44, halafu Amerika ya Kaskazini pamoja na Amerika ya Kati likiwa na madola 23, na baada yake ni Australia na Pasifiki (Oshania) likiwa na madola 14, na mwishowe ni Amerika ya Kusini likiwa na madola 12. Kwa hivyo, kwa ujumla, kuna madola 195 ulimwenguni.

Malaria

Malaria ni ugonjwa wa kuambukiza ambao unaambukizwa na mbu wa jenasi Anopheles na kusababishwa na kidubini aina ya protisti Plasmodium. Mara nyingi ugonjwa huo huitwa "homa" tu, ingawa homa ni dalili yake mojawapo tu, pia kuna magonjwa mengi yanayosababisha homa.

Malaria inatokea katika maeneo ya kitropiki na yanayokaribia tropiki ikiwa ni pamoja na sehemu za Amerika, Asia na Afrika. Mwaka 2015 duniani kulikuwa na maambukizi milioni 214 ya malaria, na watu 438,000 walikufa, wengi wao (90%) wakiwa barani Afrika, hasa watoto wachanga katika mataifa ya kusini kwa jangwa la Sahara. Malaria ni mojawapo ya magonjwa yaliyoenea sana na ni tatizo kuu la afya ya umma. Kwa kawaida huhusishwa na umaskini, lakini pia ni sababu ya umaskini na kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya uchumi.

Spishi tano za vimelea vya Plasmodium huweza kumwambukiza binadamu; aina iliyo mbaya zaidi husababishwa na Plasmodium falciparum. Malaria inayosababishwa na Plasmodium vivax, Plasmodium ovale na Plasmodium malariae husababisha ugonjwa usio shadidi sana kwa binadamu na aghalabu haijui. Spishi ya tano, Plasmodium knowlesi, husababisha malaria kwa nyani aina ya makaku lakini inaweza pia kumwambukiza binadamu. Kundi hili la spishi ya Plasmodium linalosababisha ugonjwa kwa binadamu kwa kawaida hujulikana kama vimelea vya malaria.

Kawaida, watu hupata ugonjwa wa malaria kwa kung'atwa na mbu wa kike wa jamii ya Anopheles aliyeambukizwa. Mbu aina ya Anopheles pekee ndio wanaoweza kusambaza malaria, na ni lazima wawe wameambukizwa kupitia damu waliyofyonza kutoka kwa mtu aliyeambukizwa. Mbu akimng'ata mtu aliyeambukizwa, kiasi kidogo cha damu huchukuliwa, damu hiyo huwa na vimelea vya malaria. Wiki moja baadaye, wakati mbu anapofyonza mlo wake mwingine wa damu, vimelea hivyo huchanganyika na mate ya mbu na kuingia katika mfumo wa damu ya anayeng'atwa.

Vimelea hivyo huzaa ndani ya seli nyekundu za damu, na kusababisha dalili kama vile anemia, maumivu kidogo ya kichwa, shida ya kupumua, takikadia, n.k., aidha kuna dalili nyingine za jumla kama vile homa, baridi, kichefuchefu, ugonjwa kama mafua, na katika hali mbaya zaidi kupoteza fahamu na hata kifo.

Maambukizi ya malaria yanaweza kupunguzwa kwa kuzuia kung'atwa na mbu kutumia vyandarua, dawa za kuzuia wadudu, au hatua za kudhibiti maenezi ya mbu kama vile kunyunyizia dawa za kuua wadudu ndani ya nyumba na kupiga mifereji kuondoa maji yaliyosimama ambapo mbu hutaga mayai yao.

Majaribio yamefanywa kuibuka na chanjo ya malaria bila mafanikio makuu, pamoja na kuibua mbinu za udhibiti wa kiajabu zaidi, kama vile kubadili viini tete vya mbu ili kuwafanya sugu kwa vimelea pia umefikiriwa. Ingawa utafiti unaendelea, hakuna chanjo inayopatikana sasa inayotoa ulinzi wa hali ya juu dhidi ya malaria ; mwaka 2015 ile pekee iliyoruhusiwa kutumika nje ya majaribio ni RTS,S, ambayo inatolewa kwa kudunga sindano mara nne, na hata hivyo ina ufanisi mdogo (26%-50%) kulingana na chanjo nyingine. Hivyo dawa za kuzuia lazima zitumiwe bila kukoma ili kupunguza hatari ya kuambukizwa. Madawa haya ya kuzuia maambukizi mara nyingi huwa ghali mno kwa watu wengi wanaoishi katika maeneo ambapo ugonjwa huu hupatikana kwa wingi. Watu wazima wengi wanaoishi katika maeneo ambayo ugonjwa huo umeenea huwa na maambukizi ya muda mrefu ambayo hujitokeza mara kwa mara, na pia huwa na kinga kidogo; kinga hiyo hupunguka kadri muda unavyosonga, watu wazima kama hao wanaweza kuambukizwa malaria kali ikiwa wameishi muda mrefu katika maeneo ambapo ugonjwa huo haujaenea. Wanashauriwa kuchukua tahadhari kamili wanaporejea katika maeneo ambapo ugonjwa huo umeenea.

Maambukizi ya malaria hutibiwa kwa kutumia dawa ya malaria, kama vile kwinini au vizalika vya atemisinin. Hata hivyo, vimelea vimekuwa sugu kwa nyingi ya dawa hizo. Kwa hivyo, katika baadhi ya maeneo ya dunia, dawa chache tu ndizo zilizo na uwezo wa kutibu malaria kwa ufanisi.

Mýa

Mýa Marie Harrison (amezaliwa tar. 10 Oktoba 1979) ni mwimbaji muziki wa R&B, mtunzi wa nyimbo, menguaji, mtayarishaji wa rekodi, na mwanamitindo kutoka nchini Marekani. Alizaliwa na kukulia mjini Washington, D.C., labamu yake ya kwanza iliitwa jina sawa na lake. Ilitolewa mnamo mwezi wa Aprili 1998 kupitia Interscope Records, na kuuza zaidi ya nakala milioni mbili nchini Marekani, na kupelekea kupata dhahabu kwa single ya "It's All About Me" akishirikiana na Sisqo.Albamu yake ya pili, yenye mauzo ya platinamu Fear of Flying, ilitolewa mnamo 2000 na kupata mafanikio kadha wa kadha nchini Marekani na pande zingine za dunia, kwa single ya "Case of the Ex" ikawa kibao kikali na kilichovuma zaidi cha Mýa, kwa kufikia nafasi ya kwanza kwenye Australian Singles Chart. Baada ya mwaka, Harrison amejishindia tuzo yake ya kwanza ya Grammy Award kwa kibao kikali cha "Lady Marmalade", toleo la marudio ambalo amefanya na Christina Aguilera, Lil' Kim, na Pink kwa ajili ya kibwagizo cha filamu ya Moulin Rouge! (2001).

Albamu yake ya tatu, Moodring, ilitolewa mnamo mwezi wa Julai 2003 nchini Marekani na kutunukiwa Dhahabu na RIAA. Kwa kufuatia kubadili-badili studio kadhaa, ilipelekea kuchelewesha kutolewa kwa albamu ya nne ya Mýa, Liberation (2007), ilitolewa kwa mtindo wa upakuzi kupitia intaneti huko nchini Japani pekee na kumfanya atoe 2008 Japan-albamu babkuwa ya Sugar & Spice.Kuongoza ujuzi wake katika uigizaji na kazi za uungaji mkono bidhaa, Harrison ameweza kujiingiza kwenye utangazaji wa mabishara na makapuni kama vile Coca-Cola, Gap, Iceberg, Tommy Hilfiger, na Motorola na amepta kuwa na uhusika mfupi kwenye filamu kama vile Dirty Dancing: Havana Nights (2004), Shall We Dance? (2004), na Cursed (2005). Mnamo mwaka wa 2002, amecheza kwenye filamu ya Chicago ambayo ni tengenezo la pili la filamu ya mwaka wa 1975 ya Broadway-muziki Chicago, ambayo amejishindia tuzo la Screen Actors Guild Award.Harrison alikuwa mshiriki kwenue msimu wa tisa wa Dancing with the Stars. Billboard wamempa Mýa nafasi ya 97 katika orodha Wasanii Hot 100 wa miaka ya 2000.

Vita ya Marekani dhidi Hispania

Vita ya Marekani dhidi ya Hispania ilitokea mwaka 1898. Ilianza kwa shambulizi la Marekani tarehe 25 Aprili dhidi ya Puerto Rico iliyokuwa koloni la Hispania na kuishia tarehe 12 Agosti 1898, jeshi la Hispania katika Manila (Ufilipino) lilipojisalimisha.

Hivyo Marekani ilitwaa makoloni ya Hispania ya Puerto Rico, Kuba na Ufilipino.

Vita hii ilikuwa mwanzo wa Marekani kufuata siasa ya nje ya upanuzi hata katika maeneo ya mbali. Kabla ya vita hii Marekani ilishughulika kupanua eneo lake kwenye bara la Amerika ya Kaskazini dhidi ya wakazi asilia na dhidi ya Mexiko.

Marekani ilitumia nafasi ya ghasia ya wenyeji wa Kuba dhidi ya utawala wa kikoloni wa Hispania. Baada ya mlipuko kwenye manowari ya Marekani USS Maine katika bandari ya Havana, Marekani ilitangaza vita dhidi ya Hispania ingawa sababu ya mlipuko haijajulikana hadi leo ilikuwa nini.

Hispania haikuweza kushindana na manowari na silaha za Marekani zilizokuwa zimeendelea kiteknolojia. Pia Marekani ilikuwa karibu na mahali pa vita na Hispania ilishindwa kuongeza wanajeshi na silaha.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.