Ferrari

Ferrari ni kampuni ya Italia inayotengeneza magari. Kampuni ya Ferrari ilianzishwa na Enzo Ferrari mwaka wa 1939 kutoka divisheni ya Alfa Romeo ya magari ya mashindano ikitwa Auto Avio Costruzioni, kampuni hiyo ilijenga gari lake la kwanza mwaka wa 1940. Hata hivyo, kuanzishwa kwa kampuni kama mtengenezaji wa magari kwa kawaida ilijulilikana mwaka wa 1947, wakati gari la kwanza la Ferrari limekamilishwa.

Mwaka wa 2014, Ferrari ililipimwa na Brand Finance kuwa gari lenye bei kubwa zaidi duniani. Mnamo Mei 2012 Ferrari ya 250 GTO ya 1962 ikawa gari la gharama zaidi katika historia baada ya kuuzwaa kwa dola za Marekani 38.1 milioni kwa mfanyabiashara wa Marekani Craig McCaw.

Fiat S.p.A. ilipewa asilimia 50 ya Ferrari mwaka 1969 na kupanua hisa zake kwa asilimia 90 mwaka 1988. Mnamo Oktoba 2014 Magari ya Fiat Chrysler yalitangaza nia zake za kutenganisha Ferrari S.p.A kutoka FCA; na kutangazwa FCA inamiliki asilimia 90 ya Ferrari. Ugawanyiko ulianza mnamo Oktoba 2015 na marekebisho yaliyoanzishwa Ferrari NV (kampuni iliyosajiliwa Uholanzi) kama kampuni mpya ya kampuni ya Ferrari na uuzaji uliofuata na FCA ya asilimia 10 ya hisa katika na orodha ya kawaida ya kushiriki kwenye New York Stock Exchange. Kupitia hatua zilizobaki za kujitenga, riba ya FCA katika biashara ya Ferrari iligawanywa kwa wanahisa wa FCA, na asilimia 10 inaendelea kuwa inayomilikiwa na Piero Ferrari. Kuondolewa kukamilika tarehe 3 Januari 2016. [9]

Katika historia yake yote, kampuni hiyo imejulikana kwa ushiriki wake kuendelea katika mashindano, hasa katika katika mashindano ya Formula One, ambako ni timu ya mashindano yenye mafanikio zaidi, ikiwa na ubingwa wa ujenzi zaidi ya(16) na ikazalisha idadi kubwa zaidi ya madereva wanaoshinda . Magari ya barabarani Ferrari kwa ujumla huonekana kama ishara ya kasi, anasa na mali.

Ferrari in Marbella 2004
Ferrari

Viungo vya Nje

Historia ya Italia

Historia ya Italia inahusu eneo la rasi ya Italia, hasa linalounda leo Jamhuri ya Italia.

Akiolojia imethibitisha uwepo wa Homo neanderthaliensis miaka 200,000 hivi iliyopita. Homo sapiens sapiens alifika miaka 40,000 hivi iliyopita.

Kufikia milenia ya 1 KK wakazi wengi walikuwa wa jamii ya Kizungu na kutumia lugha za Kihindi-Kiulaya.

Peninsula ya Italia iliunganishwa mara ya kwanza na Jamhuri ya Roma (509-27 KK), lakini hiyo ilipoenea Ulaya kusini na magharibi, Afrika ya Kaskazini na Asia ya Magharibi ikawa na sura ya kimataifa kama Dola la Roma.

Umoja ulipotea kuanzia uvamizi wa jiji la Roma uliofanywa na Wagermanik (476 BK) na hasa baada ya ufalme wa Karolo Mkuu aliyetawala sehemu ya kaskazini tu.

Juhudi za kuurudisha umoja zilifanywa hasa katika karne ya 19, ambapo Ufalme wa Sardinia uliteka sehemu kubwa ya Italia (hasa miaka 1860, 1866 na 1870) na kubadilika kuwa Ufalme wa Italia wenye makao makuu Roma.

Baada ya vita vikuu vya pili iligeuka Jamhuri yenye katiba inayotia mamlaka kuu mikononi mwa bunge.

Ni kati ya nchi sita zilizoanzisha Umoja wa Ulaya mwaka 1957 ikaendelea kuunga mkono ustawi wake hadi uanzishaji wa pesa ya pamoja (Euro).

Julián Gil

Julián Gil (jina halisi: Imanol Julián Elías Gil Beltrán, 13 Juni 1970) ni mwigizaji wa filamu

Kipandauso

Kipandauso ni tatizo linalotambulika kwa maumivu ya kichwa yanayojirudia tena makali hadi kiasi cha kupindukia na ambayo wakati mwingi huambatana na dalili nyingi za mfumo wa neva.

Jina la Kiingereza "Migraine" limetoka katika neno la Kigiriki ἡμικρανία (hemikrania), "uchungu kwa upande mmoja wa kichwa", kutoka ἡμι- (hemi-), "nusu", na κρανίον (kranion), "fuvu la kichwa".Kwa kawaida, maumivu hayo huathiri sehemu moja ya kichwa, huku kikidunda kwa muda wa saa 2 hadi 72. Dalili zinazohusiana na hali hii ni pamoja na kichefuchefu, kutapika, fotofobia, fonofobia (ongezeko la usikivu dhidi ya sauti) na uchungu wake kwa kawaida huzidishwa na shughuli za kimwili. Hadi thuluthi moja ya watu wenye ugonjwa wa kipandauso kinachoandamana na maumivu ya kichwa hupata aura: ishara bandia ya matatizo ya macho, hisia, lugha au mwendo inayoashiria kuwa maumivu ya kichwa yatatokea punde.Kipandauso huaminika kutokea kufuatia mchanganyiko wa masuala ya kimazingira na kijeni.Thuluthi mbili za kesi hizo zinahusika na familia.Kiwango cha homoni kinachoshuka na kupanda pia kinaweza kuwa kisababishi cha ugonjwa huu: kipandauso huathiri wavulana kwa kiwango cha juu kidogo kuliko wasichana kabla ya kubalehe, ingawa kinawaathiri wanawake mara mbili hadi tatu kuliko wanaume, ila ujauzito unakipunguza.Utaratibu wa ugonjwa huu haujatambulika. Hata hivyo, hali hii inaaminika kuwa tatizo la mfumo wa neva. Nadharia ya msingi inahusiana na kuongezeka kwa uchangamfu wa koteksi ya serebramu na udhibiti usio wa kawaida wa maumivu ya nyuroni kwa kiiniseli cha trijemia cha mfumo wa ubongo.Matibabu ya kwanza yanayopendekezwa ni dawa za kuondoa maumivu kama vile ibuprofen na acetaminophen ili kutuliza maumivu ya kichwa na antiemetic ili kutuliza kichefuchefu na kuepuka vichocheo. Dawa maalumu kama vile triptan au ergotamine zinaweza kutumika kwa watu wasiosaidiwa na dawa za kawaida za kuondoa maumivu. Zaidi ya asilimia 10 ya watu wote ulimwenguni huathiriwa na kipandauso wakati fulani maishani mwao.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.