Dola la Roma

Dola la Roma (kwa Kilatini "Imperium Romanum") lilikuwa milki kubwa lililoenea kwa karne kadhaa katika nchi zote zinazopakana na bahari ya Mediteranea (ambayo kwa sababu hiyo iliitwa "Mare Nostrum", yaani "Bahari yetu") na nyinginezo.

Lilianza kwenye mji mkuu wa Roma na rasi ya Italia ikaendelea kuunganisha makabila na mataifa ya nchi nyingi kwenye mabara matatu ya Ulaya, Afrika na Asia.

Kuanzia karne ya 1 KK Watawala wa Dola wakaitwa makaisari: Kaisari wa kwanza alikuwa Augusto.

Nchi nyingi za sasa ziliwahi kuwa sehemu ya Dola la Roma kama vile Uingereza, Ufaransa, Hispania, Italia, Ugiriki na nchi za Balkani upande wa Ulaya, Moroko, Algeria, Tunisia, Libia na Misri upande wa Afrika, na Uturuki, Syria, Lebanon, Palestina, Jordan na hata Irak upande wa Asia.

Idadi ya wakazi imekadiriwa kuwa ilifikia milioni 50-90, yaani asilimia 20 hivi za watu wote duniani wakati huo.

Lugha ya Dola la Roma ilikuwa Kilatini, ila katika sehemu za mashariki pamoja na Kigiriki cha Kale.

Sehemu ya magharibi ya Dola la Roma iliishia mwaka 476 baada ya mapinduzi ya kijeshi dhidi ya Kaisari wa mwisho Romulus Augustulus aliyefukuzwa na jemadari wa Kigermanik wa jeshi la Roma.

Upande wa mashariki Dola la Roma likaendelea hadi mwaka 1453 kwa majina kama "Roma ya Mashariki" au Bizanti.

Map of the Roman Empire at its height
Dola la Roma lilipofikia kilele cha uenezi wake mwaka 117.
Roman Republic Empire map edited
Upanuzi wa eneo la Roma kuanzia mwaka 510 KK hadi 480 BK;
nyekundu = Jamhuri ya Roma 510 KK - 40 KK
zambarau= Dola la Roma 20 BK - 360
Buluu = Dola la Roma la Magharibi 405 - 480
Njano = Dola la Roma la Mashariki (Bizanti) 405 - 480

Dola-mji

Chanzo cha dola la Roma kilikuwa dola-mji mjini penyewe.

Mji uliundwa katika karne ya 9 KK hivi kwenye vilima kando ya mto Tiber katikati ya rasi ya Italia. Waroma wenyewe walipenda kutaja mwaka 753 KK walioutumia kama chanzo cha kalenda yao "ab Urbe Condita" (a.U.C. = tangu kuundwa kwa Roma). Lakini akiolojia imeonyesha dalili za makazi ya mapema zaidi katika eneo la mji.

Mji ulitawaliwa awali na wafalme. Mwaka 509 KK mfalme wa mwisho alifukuzwa na kipindi cha jamhuri ya Roma kilianza.

Mji wa Roma ulieneza athira yake kwa njia ya mapatano au vita na miji na makabila jirani.

Katiba ya jamhuri

Kwa karne zilizofuata Waroma walifuata katiba iliyolenga kuzuia asitokee mfalme mpya. Vyeo vyote vilitolewa kwa muda tu kwa njia ya uchaguzi. Madaraka yaligawiwa kati ya ngazi na vyeo mbalimbali. Vyeo vingi vilitolewa kwa watu wawili kwa kipindi kilekile kwa sharti la kwamba hao wapatane na kuangaliana.

 • Kila mtu aliruhusiwa kuwa na cheo fulani kwa muda wa mwaka 1 pekee
 • Hakuruhusiwa kuwa na kipindi cha pili kwenye cheo kilekile
 • Aliyechaguliwa kupata cheo hakuruhusiwa kugombea cheo kingine mara moja
 • Kila cheo kilikuwa na nafasi mbili. Hao watendaji wawili waliochanga cheo kimoja walipaswa kupatana; kila mmoja aliweza kufuta maazimio ya mwenzake.
 • Mgombea wa cheo fulani alipaswa kutangulia katika utendaji wa cheo cha chini kabla ya kupanda juu
 • Kati ya kugombea vyeo viwili mgombea alipaswa kupumzika mwaka mmoja.

Kulikuwa na cheo kimoja pekee kilichotekelezwa na mtu mmoja tu: dikteta. Dikteta aliweza kuchaguliwa katika kipindi cha dharura kama vita kwa muda wa miezi sita. Katika kipindi hiki alifanya maazimio peke yake. Kwa kawaida watendaji wakuu walikuwa makonsuli ("consules") waliochaguliwa kwa muda wa mwaka 1.

Upanuzi katika Italia

Dola la Roma lilianza kupanuka katika Italia. Mwaka 396 KK mji jirani wa Veio ulitwaliwa na kuharibiwa. Katika karne ya 4 KK vilitokea vita kati ya Roma na majirani na eneo lote la Lazio likatawaliwa na Roma.

Roma ilianzishwa utaratibu wa ushirikiano na majirani. Mara chache tu wapinzani walimalizwa kabisa kama Veio. Mara nyingi walilazimishwa kutia sahihi mikataba ya ushirikiano walimopaswa kuwasaidia Waroma kwa wanajeshi na kutokuwa na uhusiano wowote na makabila ya nje. Makabila na miji iliyoshirikiana vizuri na Roma walipewa uraia wa Roma sawa na wenyeji wa mji wenyewe.

Katika karne ya 3 KK Waroma waliendelea kutwaa sehemu kubwa ya rasi ya Italia. Katika vita dhidi ya Pyrrho wa Epirus (eneo kati ya Albania na Ugiriki wa leo) miaka ya 280 KK - 275 KK Roma ilishinda mara ya kwanza dhidi ya jeshi lililotoka nje ya Italia. Vita hii ilisababisha ubwana wa Roma juu ya miji ya Kigiriki kusini mwa Italia ilipaswa kukubali ubwana wa Roma tangu 275 KK pia makabila ya milimani.

CarthageMapDe
Eneo la Karthago mnamo 264 kabla ya vita za Kipuni

Vita za Wapuni na kipaumbele katika Mediteranea ya magharibi

Ushindi huo ulisababisha ugomvi na Karthago iliyotawala pwani za Mediteranea pamoja na kisiwa kikubwa cha Sisilia. Hali ya vita ilianza tangu mwaka 264 KK kati ya Roma na watu wa Karthago ("Wafinisia" au "Wapuni" jinsi walivyoitwa na Waroma). Vita hii ya kwanza ilikwisha mwaka 241 KK na Karthago ilipaswa kuwaachia Waroma Sisilia yote. Katika vita hii Waroma waliendelea kushinda baharini pia, si kwenye nchi kavu tu.

Vita ya pili dhidi ya Wapuni (218 KK - 201 KK) ilianzishwa na Karthago. Jemadari Hanibal alitaka kulipiza kisasi akavuka milima ya Alpi kwa tembo zake wa kivita. Alishinda mara kadhaa jeshi la Waroma lakini Waitalia wengine walisimama imara upande wa Roma. Mwishowe Roma ilishinda mara ya pili na Karthago ilipaswa kuwaachia Waroma pwani yote ya kaskazini-magharibi ya Mediteranea pamoja na Gallia (leo Ufaransa) ya kusini, Hispania na visiwa vya Mediteranea. Karthago ilibaki upande wa Afrika tu.

Mabaki ya himaya ya Karthago, pamoja na mji wenyewe, yalimalizwa na Roma katika vita ya tatu dhidi ya Wapuni kati ya miaka 149 KK na 146 KK. Karthago iliharibiwa kabisa na wakazi wote wasiouawa waliuzwa kama watumwa.

Upanuzi katika Ugiriki

Wakati wa vita ya pili ya Wapuni mfalme Filipo V wa Makedonia aliwahi kuwasaidia Karthago. Roma ilitumia nafasi ya ushindi kupinga upanuzi wa Makedonia katika Ugiriki kwa kusaidia madola madogo za Ugiriki ya kusini dhidi ya Filipo V. Vita hizi kati ya Roma na Makedonia zilikuwa na shabaha za kuzuia kipaumbele cha ufalme wowote wa Ugiriki. Roma likabaki katika siasa ya Ugiriki zaidi kama mtazamaji.

Mwaka 192 KK mfalme Antioko III wa milki ya Waseleuko aliingia kijeshi katika Ugiriki. Roma ikajibu kwa kutuma legioni zake na kuanzisha mfululizo wa vita zilizoendelea hadi mwaka 146 KK. Waseleuko walipaswa kujiondoa kabisa katika Ugiriki. Uwezo wa Makedonia ukapunguzwa na sehemu kubwa ya Ugiriki kuwa majimbo ya Kiroma ya Akaya, Epirus na Makedonia.

Jaribio la mwisho la Wagiriki kutetea mabaki ya uhuru wao lilisababisha uangamizi wa mji wa Korintho mwaka 146 KK pamoja na uharibifu wa Karthago.

Kuingia Asia

Mwaka 133 KK mfalme wa Pergamon katika Asia Ndogo (Uturuki wa leo) aliyeogopa fitina kati ya warithi wake aliamua kukabidhi milki yake kwa jamhuri ya Roma baada ya kifo chake. Milki hii ikawa jimbo la Kiroma la Asia lililoonekana kuwa jimbo tajiri kabisa. Tukio hili likawa mlango wa Roma kupanua zaidi himaya yake katika mashariki ya Mediteranea.

Jimbo jipya la "Asia" likavuta wanasiasa Waroma wenye hamu ya kujitajirisha likawa kitovu cha ufisadi katika milki ya Roma. Mwanasiasa aliyepata nafasi ya kuwa gavana alikuwa mtu tajiri sana baada ya miaka 2 au 3.

Upanuzi wa Dola la Roma lilileta faida lakini matatizo pia:

 • nafasi ya kujitajirisha katika utumishi kwenye majimbo mapya ya nje kulisababisha kuongezeka kwa gharama za kugombea. Maana wanasiasa waliolenga kupata nafasi hizi walikopa na kutumia pesa nyingi ili wapate kura nyingi. Waliamini ya kwamba baada ya ushindi wangeweza kurudisha madeni. Hali hii ilisababisha kuongezeka kwa kiwango cha pesa kilichotumiwa kwa kampeni za uchaguzi kwa jumla.
 • baada ya kuingiza maeneo mengi ya mbali Waroma waliona athira za tamaduni za kigeni. Waroma wa miaka ya kwanza ya jamhuri walijivunia maisha bila anasa. Walidharau mapambo na matumizi ya pesa kwa mahitaji ya anasa. Lakini sasa walivuta katika jamii yao watu wa Ugiriki na Asia waliopenda anasa.

Kipindi cha mgogoro

Mafanikio na upanuzi wa jamhuri ya Kiroma vilileta mabadiliko makubwa. Vilisababisha pia kipindi cha mgogoro kilichoanza kuonekana kwa nguvu pamoja na upanuzi huko Asia.

Tatizo kuu lilikuwa suala la ardhi pamoja na mfumo wa jeshi.

Mfumo wa jeshi ulisimama juu ya msingi wa kila raia kushiriki vitani. Kila raia wa Roma alipaswa kubeba silaha na kujiunga na jeshi kama dola liliamua kuwa vita ni lazima. Kila raia alipaswa kujipatia na kugharimia silaha zake.

Upanuzi wa dola lilileta matatizo. Hasa wakulima wengi wadogo walishuka kiuchumi. Kadiri dola lilivyopanuka na jeshi lilivyopaswa kupiga vita katika maeneo ya mbali, hao wakulima wadogo walipaswa kuondoka kwa muda mrefu zaidi kutoka nyumbani na shambani mwao. Utekelezaji wa kazi ulibaki kwa wazee, wanawake na watoto pekee. Wanaume wenyewe, wenye uwezo wa kazi hasa, waliondoka kwenda vitani na kukaa mbali na kaya kwa vipindi vilivyozidi kuongezeka.

Kinyume chake matajiri hawakupata matatizo hayo. Wakiwa na mashamba makubwa waliweza kununua watumwa wa kutosha walioweza kulima na kutawala mashamba yao pamoja na wazee na wanawake hadi wenyewe waliporudi. Vilevile matajiri walikuwa na uwezo wa kununua silaha bora, pia farasi za kupandia na hivyo kushika vyeo vya juu zaidi jeshini. Vyeo vya juu viliwapa sehemu kubwa zaidi ya mali ya maadui iliyoporwa baada ya ushindi. Kutokana na mapato hayo makubwa zaidi waliweza kununua mashamba makubwa zaidi.

Tokeo lake lilikuwa mabadiliko la kilimo katika Italia: wakulima wadogo walizidi kushuka chini, walipaswa kukopa pesa kwa kujidumu na kuwa na madeni. Mwishowe walipaswa kuuza mashamba yao na kutafuta kazi kama vibarua. Kinyume chake tabaka la wenye mashamba makubwa liliongezewa nguvu na utajiri. Tofauti za kijamii ziliongezeka. Tofauti hizo zilisababisha kutokea kwa kipindi cha machafuko ya kisiasa na ya kijamii ambayo yalipeleka Roma hadi vipindi vya vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Marejeo

 • Frank Frost Abbott (1901). A History and Description of Roman Political Institutions. Elibron Classics. ISBN 0-543-92749-0.
 • J. A. Crook, Law and Life of Rome, 90 BC–AD 212, 1967 (ISBN 0-8014-9273-4).
 • Arther Ferrill, The Fall of the Roman Empire: The Military Explanation, Thames and Hudson, 1988 (ISBN 0-500-27495-9).
 • Goldsworthy, Adrian. The Complete Roman Army, Thames and Hudson, 2003 (ISBN 0-500-05124-0).
 • Benjamin Isaac, "The Limits of Empire: the Roman Army in the East" Oxford University Press, 1992 (ISBN 0-19-814926-3).
 • Andrew Lintott, Imperium Romanum: Politics and administration, 1993 (ISBN 0-415-09375-9).
 • Edward Luttwak, The Grand Strategy of the Roman Empire, Johns Hopkins University Press, 1976/1979 (ISBN 0-8018-2158-4).
 • Ritti, Tullia; Grewe, Klaus; Kessener, Paul (2007), "A Relief of a Water-powered Stone Saw Mill on a Sarcophagus at Hierapolis and its Implications", Journal of Roman Archaeology 20: 138–163
 • Schnitter, Niklaus (1978), "Römische Talsperren", Antike Welt 8 (2): 25–32
 • Smith, Norman (1970), "The Roman Dams of Subiaco", Technology and Culture 11 (1): 58–68, doi:10.2307/3102810
 • Smith, Norman (1971), A History of Dams, London: Peter Davies, pp. 25–49, ISBN 0-432-15090-0

Marejeo mengine

 • John Bagnell Bury, A History of the Roman Empire from its Foundation to the death of Marcus Aurelius, 1913, ISBN 978-1-4367-3416-5
 • Duncan B Campbell, The Rise of Imperial Rome, AD 14-193, Osprey, 2013, ISBN 978-1-78096-280-1
 • Winston Churchill, A History of the English-Speaking Peoples, Cassell, 1998, ISBN 0-304-34912-7
 • Edward Gibbon, The History of the Decline and Fall of the Roman Empire, 1776–1789
 • Adrian Goldsworthy. In the Name of Rome: The Men Who Won the Roman Empire, Weidenfield and Nicholson, 2003, ISBN 0-297-84666-3
 • Michael Grant, The History of Rome, Faber and Faber, 1993, ISBN 0-571-11461-X
 • Antonio Santosuosso, Storming the Heavens: Soldiers, Emperors and Civilians in the Roman Empire, Westview Press, 2001, ISBN 0-8133-3523-X

Viungo vya nje

Hourglass.svg Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Dola la Roma kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
238

Makala hii inahusu mwaka 238 BK (Baada ya Kristo).

Algiers

Algiers (kwa Kiarabu مدينة الجزائر, madīnat al-djazā'ir, "mji wa visiwa"; kwa Kifaransa Alger) ni mji mkuu pia mji mkubwa kabisa wa nchi ya Algeria ikiwa na wakazi milioni 2 (mwaka 2005), pamoja na mitaa ya nje takriban milioni 5. Iko mwambaoni mwa bahari ya Mediteranea.

Algiers ni makao ya serikali na kitovu cha uchumi, biashara, utamaduni na mawasiliano nchini.

Ankara

Ankara ni mji mkuu wa Uturuki. Iko katika kitovu cha Anatolia kwenye kimo cha 938 m juu ya UB. Huu ndiyo mji mkuu wa Mkoa wa Ankara.

Ankara ni mji mkubwa wa pili nchini baada ya Istanbul. Kuna wakazi 4,319,167 (2005).

Athens

Athens (kwa Kigiriki Αθήνα "Athina") ni mji mkuu wa Ugiriki (Uyunani), mji mkubwa wa nchi hii, na mojawapo kati ya miji mashuhuri ya dunia yenye historia ndefu tangu miaka elfuelfu.

Siku hizi mji una wakazi milioni 3.

Dayosisi

Dayosisi (kwa Kilatini dioecesis, kutokana na Kigiriki διοίκησις, dioikesis, yaani "utawala") ni jina linalotumika katika madhehebu mbalimbali ya Ukristo (kwa mfano Walutheri na Waanglikana kumaanisha kitengo kilichopo chini ya usimamizi wa askofu katika eneo fulani.

Wakatoliki wanaoongea Kiswahili wanaiita jimbo, lakini kwa lugha nyingine wanatumia neno kama hilo bila ya kulitafsiri; kwa mfano "diocese" (Kiingereza), "diocesi" (Kiitalia) au "diocèse" (Kifaransa).

Diokletian

Gaius Aurelius Valerius Diocletianus (takriban 245 – takriban 312) alikuwa Kaizari wa Dola la Roma kuanzia 20 Novemba 284 hadi 1 Mei 305 alipojiuzulu. Alimfuata Numerian.

Kwanza alitawala dola zima, lakini 1 Machi 286 alimteua Maximian kutawala sehemu za Magharibi.

Ni maarufu kwa kuendesha dhuluma kali zaidi ya serikali ya Dola la Roma dhidi ya Wakristo.

Dola la Roma Magharibi

Dola la Roma Magharibi ni sehemu ya Dola la Roma upande wa Magharibi iliyo na mji mkuu wa Roma. Kuanzia mwaka wa 285 Dola la Roma lilikuwa na makaisari wawili ili kurahisisha utawala wa en eneo lililokuwa kubwa mno.

Chini ya Konstantin Mkuu, mji wa Konstantinopoli ulitangazwa mji mkuu wa pili. Baada ya kifo cha Theodosius Mkuu, utawala uligawanywa kati ya wana wake na kweli kulikuwa na madola mawili yenye miji mikuu miwili.

Katika magharibi wanajeshi Wagermanik katika utumishi wa Waroma walipata uwezo zaidi hadi wakamua kushika madaraka wenyewe. Mtawala wa mwisho wa Roma Magharibi alikuwa Kaisari Romulus Augustus aliyeondoshwa madarakani mwaka wa 476. Mkuu wa jeshi Odoaker alimpindua Romulus akajitangaza kama mfalme wa magharibi hata akiendelea kuheshimu kipaumbele wa makaisari wa mashariki mjini Konstantinopoli.

Watawala Wagermanik wa Italia waliendelea kutawala katika jina la makaisari lakini hali halisi Dola la Roma Magharibi lilikuwa limekwisha.

Enzi ya kati

Enzi ya Kati (pia: Zama za Kati; kwa Kiingereza: "Middle Ages", pia "mediaevo" au "medievo") ni kipindi cha katikati cha historia ya Ulaya katika mgawanyo wa “zama” tatu: ustaarabu wa

Zama za Kale,

Zama za Kati, na

Wakati wa Kisasaama:

Enzi ya Kale,

Enzi ya Kati na

Enzi ya Kisasa.Hata kama ugawaji huo umetokana na mazingira ya Ulaya tu, hutumiwa pia kwa maeneo mengine ya dunia. Wataalamu wengi huamini ya kwamba haufai sana kidunia lakini hadi sasa hakuna mpangilio mwingine kwa dunia yote unaoeleweka kirahisi hivi.

Kwa kawaida, Zama za Kati za Ulaya Magharibi huhesabiwa toka mwisho wa Dola la Roma Magharibi (karne ya 5) hadi kuanza kwa falme za kitaifa, mwanzo wa uvumbuzi wa ng’ambo ya Ulaya, kipindi cha mwamko-sanaa, na Matengenezo ya Waprotestanti kuanzia mwaka 1517.

Mabadiliko hayo yalionesha mwanzo wa kipindi cha Zama za Kisasa ambacho kilitangulia mapinduzi ya viwanda.

Kaizari

Kaizari ni cheo cha mfalme mkuu. Neno la Kiswahili limetokana na lugha ya Kijerumani "Kaiser", lakini asili yake ni Kilatini "Caesar".

Karthago

Karthago (kwa Kilatini Carthago; kwa Kigiriki Καρχηδών Karchēdōn; katika lugha asilia ya Kifinisia Qart-Hadašt, yaani "mji mpya") zaidi ya miaka 2000 iliyopita ulikuwa mji mkubwa katika Afrika ya Kaskazini karibu na Tunis ya leo nchini Tunisia.

Kilatini

Kilatini ni lugha ya kihistoria ambayo siku hizi haina tena wasemaji kama lugha ya kwanza, lakini bado hufundishwa katika shule na vyuo na hata kutumiwa kama lugha ya pili. Ilikuwa pia lugha ya kimataifa ya elimu na istilahi nyingi za kisayansi zimetoka katika Kilatini.

Kilatini kilikuwa lugha hai takriban kati ya miaka 500 KK na 600 BK na baadaye lahaja zake mbalimbali ziliendelea na kukomaa kuwa lugha za pekee zinazojulikana kama lugha za Kirumi.

Kilatini ni pia jina la mwandiko au aina ya herufi (alfabeti ya Kilatini) inayotumika kwa lugha nyingi duniani. Hata Kiswahili huandikwa siku hizi kwa herufi za Kilatini kama kwa mfano ukurasa huu wa Wikipedia.

Kilikuwa

lugha ya Dola la Roma (angalia pia Roma ya Kale)

lugha mama ya lahaja zilizoendelea kuwa lugha za Kirumi kama Kiitalia, Kifaransa, Kihispania, Kireno, Kiromania n.k.

lugha ya elimu na sayansi katika Ulaya kwa karne nyingi

lugha rasmi ya serikali katika nchi nyingi za Ulaya kati ya mwisho wa Dola la Roma mwaka 476 BK hadi mnamo 1700 BK

lugha pekee ya liturgia katika Kanisa la Kilatini hadi mwaka 1965Hadi leo ni

lugha ya kidini katika Kanisa Katoliki

lugha rasmi katika nchi ya Vatikano.

Kilatini ina athira kubwa katika lugha ya sayansi na elimu. Hadi leo hufundishwa mashuleni hasa Ulaya.

Kiswahili kimerithi maneno yenye asili ya Kilatini hasa kupitia Kiingereza kilichopokea karibu asilimia hamsini ya maneno yake yote kutoka Kilatini kupitia hasa Kifaransa. Maneno mengine ya Kilatini yameingia Kiswahili kupitia Kireno, Kifaransa n.k.

Kilatini huendelezwa na kukuzwa na wapenzi wa lugha. Kuna misamiati ya "Kilatini cha Kisasa" yenye maneno kwa ajili ya mitambo ya kisasa, mtandao n.k. Wikipedia ya Kilatini ilifikia makala zaidi ya 130,000 kwenye mwaka 2019.

Konstantinopoli

Konstantinopoli (kwa Kigiriki: Κωνσταντινούπολις - Konstantinupolis, yaani "mji wa Konstantino") ni mji ulioanzishwa na Wagiriki wa kale kwa jina la Bizanti mnamo 660 KK ukapewa na Kaisari Konstantino jina lake mwenyewe na kufanywa mji mkuu wa Dola la Roma kuanzia mwaka 330 BK.

Baadaye ukabaki mji mkuu wa Dola la Roma la Mashariki au milki ya Bizanti kati ya 395 hadi 1453.

Baada ya kutwaliwa na Waturuki Waosmani ulikuwa mji mkuu wa milki ya Osmani hadi 1922.

Mji ulianzishwa upande wa Ulaya wa mlangobahari wa Bosporus kati ya hori ya "pembe ya dhahabu" na Bahari ya Marmara.

Leo hii mji huo wa Kituruki umevuka Bosporus ukienea hata upande wa Asia.

Ulibadilishiwa jina mara kadhaa katika historia yake ndefu: Bizanti, Roma Mpya (kwa Kigiriki: Νέα Ῥώμη), Konstantinopoli, tena Bizanti, Stambul, halafu Istanbul (tangu mwaka 1930).

Katika Ukristo ni muhimu kama makao ya Askofu wa pili kwa heshima kati ya Maaskofu wote duniani, kadiri ya orodha iliyotolewa na mitaguso mikuu ya karne ya 4.

Monasteri

Monasteri (kutoka Kiingereza "monastery") katika Ukristo ni jengo au majengo ya pamoja ambapo inaishi jumuia ya wamonaki, chini ya mamlaka ya abati. Kila moja inaweza kujitegemea, ingawa pengine yameundwa mashirikisho ili kusaidiana na kuratibu malezi na masuala mengine ya pamoja.

Monasteri ni tofauti na konventi, zilizoanzishwa na mashirika ya ombaomba, ambayo wanajumuia wake si wamonaki bali wanaitwa "ndugu".

Monasteri za Kikristo zilianza kujengwa baada ya kwisha kwa dhuluma za Dola la Roma dhidi ya Ukristo, ingawa hata kabla ya hapo kulikuwa na waamini wanaoishi namna fulani ya maisha ya kitawa.

Kwa karne nyingi monasteri zilikuwa kama mji mdogo unaojitegemea kiuchumi pia kutokana na mkazo uliowekwa katika kusali na kufanya kazi.

Kuna monasteri hata katika ya baadhi ya dini nyingine, hasa Ubuddha.

Orodha ya Makaizari wa Roma

Orodha hii inataja makaisari wa Dola la Roma kuanzia Kaizari Augustus hadi mwisho wa Dola la Roma Magharibi mwaka wa 476.

Papa Nikolasi I

Papa Nikolasi I au Nikolasi Mkuu (takriban 820 – 13 Novemba 867) alikuwa papa kuanzia 24 Aprili 858 hadi kifo chake.

Alimfuata Papa Benedikto III akafuatwa na Papa Adriano II.

Anakumbukwa kwa kuimarisha mamlaka wa Papa wa Roma, akichangia ustawi wa cheo hicho hasa katika Ulaya Magharibi. Alisisitiza kuwa mamlaka hiyo iko juu ya watawala pia katika masuala ya imani na maadili.

Alikataa kutangaza ubatili wa ndoa ya mfalme Lothari II wa Lotharingia na mke wake, ingawa mfalme aliudai ili kumuoa Waldrada, mtaguso fulani uliukubali na jeshi la Wafaranki lilizingira Roma.

Mahusiano na Dola la Roma Mashariki yaliharibika kwa sababu aliunga mkono Patriarki Ignas wa Konstantinopoli aliyekuwa ameondolewa madarakani ili kumpisha Fosyo.

Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu. Sikukuu yake ni tarehe 13 Novemba.

Roma ya Kale

Roma ya Kale ni ustaarabu uliokua kutoka katika mji Roma, ulioanzishwa katika rasi ya Italia kabla ya karne ya 9 KK.

Katika kipindi cha karne kumi na mbili cha uhai wake, ustaarabu wa Roma ulibadilika toka kuwa dola-mji, kwanza ufalme halafu jamhuri ya Roma yenye athira katika Italia, na hadi kuwa milki kubwa. Roma ya Kale ilikuja kutawala Ulaya Magharibi na eneo zima linalozunguka bahari ya Mediteranea kwa njia ya vita au kwa njia ya maungano na maeneo.

Baada ya karne za upanuzi uhamiaji wa mataifa mapya ya Wagermanik pamoja na mashambulio kutoka Asia zilisababisha hatimaye kuanguka kwa Dola la Roma kuanzia karne ya 5 BK.

Sehemu ya magharibi ya milki dola liliporomoka kabisa likiendelea na umoja wa kiutamaduni lililotunzwa hasa na Kanisa Katoliki chini ya uongozi wa Papa wa Roma.

Sehemu ya mashariki ya Dola iliyoongozwa kutoka Konstantinopoli iliendelea. Tabia yake ilibadilika polepole kuwa milki ya Wagiriki ikaitwa baadaye Milki ya Byzanti ikiendelea hadi mwaka 1453, Waturuki walipotwaa mji wa Konstantinopoli na kuimaliza.

Senati

Senati (pia Seneti kutoka Kiingereza "Senate") ilikuwa baraza kuu katika Dola la Roma. Jina lake limetokana na neno la Kilatini senes (= mzee), kwa hiyo senati ilikuwa baraza la wazee ("Senatus").

Wakati wa Jamhuri ya Kiroma senati ilikuwa chombo kikuu cha dola; wakati wa makaisari tangu Augusto umuhimu wake ulipungua lakini kwa muda mrefu makaisari walijitahidi kuheshimu baraza hilo hata kama mamlaka zake zilipungua zaidi na zaidi.

Sheria zilitangazwa kwa jina la senati; wakati wa fitina kati ya senati na mtawala kulikuwa pia na amri za Kaisari zilizotangazwa bila idhini ya senati, lakini kwa jumla makaisari hawakutumia jina "sheria" kwa amri hizo.

Kimsingi senati ilijumlisha wote waliowahi kuwa maafisa wakuu wa dola. Katika utaratibu wa Kiroma maafisa wote walichaguliwa kwa muda wa mwaka mmoja. Wenye vyeo hawakupata mishahara, kwa hiyo walikuwa hasa matajiri walioweza kugombea nafasi hizo. Kwa sababu hiyo senati kama mkutano wa maafisa wa kale ilijumlisha hasa watu kutoka familia za makabaila au familia tajiri nyingine.

Wakati wa Jamhuri ya Kiroma senati ilikuwa na maseneta 100 walioongezeka baadaye kuwa 300. Gaius Julius Caesar aliongeza vyeo hivi hadi wajumbe 900.

Senati ilidumu hadi mwisho wa Dola la Roma. Katika Dola la Roma Magharibi heshima yake ilikubaliwa ndani ya mji wa Roma tu na habari za mwisho wa senati zimepatikana hadi mwaka 600 BK. Katika Dola la Roma Mashariki (Bizanti) senati ilidumu hadi mwisho kabisa, mnamo mwaka 1453, lakini karne za mwisho haikuwa na athira yoyote.

Senati ya Roma ilikuwa mfano kwa nchi nyingi; katika lugha za Ulaya taasisi mbalimbali huitwa kwa jina hili.

Uario

Uario (au Uariani) ni msimamo wa teolojia ambao unamuita Yesu "Mwana wa Mungu" lakini kwa kukanusha imani ya Wakristo karibu wote kuhusu Utatu mtakatifu, yaani uwemo wa nafsi tatu za milele katika Mungu pekee: Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.

Hivyo unafafanua kwamba Yesu Kristo si sawa na Mungu Baba wala si wa milele, bali ni kiumbe tu, ingawa bora kuliko wote.Jina linatokana na lile la Ario (250 hivi – 336), padri wa Aleksandria, Misri. Ingawa yeye hakuwa wa kwanza kufafanua hivyo maneno ya Yoh 14:28, mafundisho yake yalivuruga kabisa Kanisa kwa muda mrefu na kuhitaji mitaguso mikuu miwili ili kuyakomesha katika Dola la Roma.Kwa ajili hiyo, katika mitaguso hiyo ya kiekumeni ya kwanza (Mtaguso wa kwanza wa Nisea na Mtaguso wa kwanza wa Konstantinopoli) ilitungwa ikapanuliwa kanuni ya imani ya Nisea-Konstantinopoli iliyotakiwa kufuatwa na maaskofu wote, hata kwa nguvu ya serikali ya Dola la Roma.

Juhudi hizo hazikuzuia Uario kuendelea nje ya dola hilo, hasa kati ya makabila ya Kijerumani ambayo muda mfupi baadaye wakavamia Dola la Roma na kudhulumu Wakatoliki, hasa Hispania na Afrika Kaskazini.

Mwanzoni mwa karne za kati, Uario uliachwa kabisa, lakini ukatokea tena na tena, hasa nchini Marekani.

Hivyo Uario unafuatwa hata leo na madhehebu kadhaa ya Ukristo, ambayo kwa sababu hiyo yanatazamwa na wengine wote kama si Wakristo ama walau ni Wakristo wa pembeni (kwa Kiingereza "Marginal Christians"). Mfano wake ni Mashahidi wa Yehova, Wamormoni, lakini pia baadhi ya Wapentekoste.

Ufalme wa Byzanti

Ufalme wa Byzanti (kwa Kigiriki: Βυζαντινή Αυτοκρατορία) ni neno linalotumika kutaja Dola la Roma lilivyoendelea mashariki mwa eneo la kandokando ya bahari ya Mediteranea katika Zama za Kati, ukiwa na makao yake makuu kwenye mji wa Konstantinopoli (ulioitwa pia Bizanti) na kutumia lugha ya Kigiriki.

Katika baadhi ya maana, hasa baada ya kuanguka kwa Dola la Roma Magharibi na mjini Roma penyewe, hujulikana pia kama Dola la Roma Mashariki.

Wabizanti wenyewe walijiona ni bado Dola la Roma likiendelea tu. Watawala walitumia cheo cha "Kaisari" kama awali.

Hata hivyo, kwa wakati mwingi wa historia yake, ulifahamika na wenzao wa Ulaya magharibi kama “Ufalme wa Wagiriki” au “Ufalme wa Konstantinopoli” au "Rhômania".

Lakini majirani wa mashariki kama Waarabu waliendela kuwaita "Waroma" (kwa Kiarabu روم rum).

Bizanti ilipata mapigo mawili makubwa katika historia yake:

Uvamizi wa Waarabu Waislamu kuanzia mwaka 636 uliosababisha kupotea kwa majimbo ya Afrika ya Kaskazini, Misri na Shamu

Uvamizi wa jeshi la Wakristo la Vita vya msalaba walioteka mji wa Konstantinopoli mwaka 1204. Shambulio hili lilisababisha nguvu za ufalme kufifia kabisa. Hata baada ya watawala wa Bizanti kurudi Konstantinopoli walikosa nguvu ya kujihami dhidi ya Waturuki Waosmani. Hatimaye hao waliteka Konstantinopoli mwaka 1453 na kumaliza kabisa Bizanti uliokuwa umetunza urithi wa Roma ya Kale hadi wakati ule.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.