Dakika

Dakika ni kipimo cha wakati. Si kipimo cha SI kamili kama ilivyo sekundi. Dakika ni sehemu ya 60 ya saa moja. Dakika yenyewe hugawiwa kwa sekundi 60.

Science-symbol-2.svg Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Dakika kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
24 (msimu wa 4)

Msimu wa Nne (pia unajulikana kama Siku ya 4) ya mfululizo wa televisheni wa 24 ulioanza kurushwa hewani mnamo tar. 9 Januari 2005 na kipengele cha mwisho kuishia 23 Mei 2005.

Mstari wa hadithi ya msimu wa nne inaanza na kuisha saa 1:00 Asubuhi.

Kipande cha kwanza cha dakika 10 kilikuwa kinapatikana hata katika DVD ya msimu wa tatu. Msimu ulianza kutangazwa kupitia Sky One nchini Uingereza kabla ya kuanza kuonyeshwa nchini humo. Pia DVD ya msimu wa nne ilikuwa ikipatika nchini Uingereza.

24 (msimu wa 5)

Msimu wa Tano (pia unajulikana kama Siku ya 5) ya mfululizo wa kipindi cha televisheni cha 24 kilichoanza kurushwa hewani kuanzia tar. 15 Januari 2006 na kumalizia msimu wake kunako tar. 22 Mei 2006.

Hadithi ya Msimu wa Tano inaanza na kushia 7:00 asubuhi. Muda wake uko sawa na ule wa msimu uliopita.

Dakika 10 za mwanzo zilikuwa zikipatikana kwenye DVD ya msimu uliopita. Ilikuwa ikirushwa kwenye Sky One huko nchini Uingereza kabla ya kuanza rasmi kwa msimu wa tano.

Kalenda ya Gregori

Kalenda ya Gregori ni kalenda ambayo leo inatumiwa zaidi kimataifa. Jina limetokana na Papa Gregori XIII aliyeamua kutumia kalenda hiyo tangu tar. 15 Februari 1582 badala ya Kalenda ya Juliasi.

Latitudo

Latitudo (kwa ing.: latitude) ni mahala pa mchoro wa dunia au ramani huonyesha kwa mistari iliolazwa ni njia ya kuonyesha mahali duniani kwa kutaja umbali wake kutoka ikweta kwa kipimo cha digrii (°).

Mahali penye ikweta kamili (kwa mfano Nanyuki katika Kenya) ina latitudo ya "0". Mahali pa mbali ni ncha ya kaskazini au ya kusini zinazotajwa kwa 90°. Pamoja na kipimo cha longitudo inataja mahali kamili duniani.

Latitudo za kaskazini na kusini ya ikweta zinatofautishwa ama kwa kuongeza herufi "N" (=north) na "S" (south) au kwa alama za "+" (kaskazini) na "-" (kusini).

Digrii za latitudo hugawiwa katika umbali wa 60 dakika au minuti; dakika ya latitudo ni mita 1852 au maili moja ya kibahari. Dakika hugawiwa katika nukta au sekondi. Mfano: 13°19.717′ N.

Latitudo muhimu ni:

1. Ikweta (0°)

2. Tropiki ya kansa (23½°Kas)

3. Tropiki ya kaprikoni (23½°Kus)

4. Duara la aktiki (66½°Kas)

5. Duara la antaktika (66½°Kus)

Pamoja na namba ya longitudo inaonyesha mahali kamili kwenye uso wa dunia.

Longitudo

Longitudo (ing.: longitude) katika ramani au mchoro wa dunia ,ni njia ya kuonyesha mahali duniani kwa kutaja umbali wake kutoka mstari wa meridiani ya sifuri kwa kipimo cha digrii (°). Kwenye msingi wa digrii 360 za duara digrii hizi za latitudo huehesabiwa hadi +180° (kwenda mashariki) au hadi -180° (kwenda magharibi). Ni kawaida vilevile kutaja tofauti kati ya longitudo za mashariki au magharibi kwa kuongeza herufi za "E" (east) na "W" (west) badala ya +/-. Pamoja na kipimo cha latitudo inataja kamili kila mahali duniani.

Meridiani ya 0° imekubaliwa ni mstari kutoka ncha ya kaskazini hadi ncha ya kusini unaopita katika mji wa Greenwich (karibu na London / Uingereza).

Digrii za longitudo hugawiwa katika umbali wa 60 dakika au minuti; dakika hugawiwa katika nukta au sekondi. Umbali huu hauna kipimo kamili cha urefu kwa sabau ya umbo la dunia. Kwenye ikweta umbali kati ya longitudo ni 111 km, katika ncha penyewe ni sifuri kwa sababu longitudo zote hukutana hapa.

Mji wa Kiafrika karibu kwenye longitudo ya sifuri ni Accra (Ghana). Vipimo vyake ni : 5°30' N (latitudo) na 0°10' W (longitudo).

Mauti

Mauti (kutoka Kiarabu موت, maut) au kifo (kutoka kitenzi cha Kibantu kufa) ni mwisho wa uhai; kwa lugha ya biolojia mwisho wa michakato yote ndani ya kiumbehai ambayo ni dalili za uhai.

Mazoezi ya mwili

Mazoezi ya mwili (kwa Kiingereza "physical exercises") ni vitendo vinavyofanywa aghalabu na watu au mtu ili kuuweka mwili katika hali ya afya nzuri na kuwa tayari kwa ajili ya jambo maalumu.

Inafaa uanze mazoezi hayo kwa dakika kumi kama mwili wako haujazoea kufanya mazoezi. Polepole, ongeza wakati huo uwe dakika mia na hamsini.

Mwanaanga

Mwanaanga ni mtu anayerushwa katika anga-nje yaani anga lililo nje ya angahewa ya dunia. Majina mengine yaliyokuwa kawaida ni "kosmonauti" (kwa [Kirusi]]: космонавт) kwa wanaanga Warusi na "astronauti" (kwa Kiingereza astronaut) kwa wanaanga kutoka Marekani. Wachina wametumia neno "taikonauti".

Mwanaanga wa kwanza katika historia ya binadamu alikuwa Mrusi Yuri Gagarin kutoka Umoja wa Kisovyeti aliyerushwa tarehe 12 Aprili 1961 kwa chombo cha angani Vostok akizunguka dunia yote mara moja katika muda wa dakika 108.

Alifuatwa tarehe 5 Mei 1961 na Alan Shepard kutoka Marekani aliyetumia chombo cha angani cha Mercury .

Mwanamke wa kwanza angani alikuwa Mrusi Valentina Tereshkova mwaka 1963.

Wanaanga wa kwanza waliofika kwenye uso wa Mwezi walikuwa Wamarekani Neil Armstrong na Buzz Aldrin tarehe 20 Julai 1969.

Hadi Machi 2008 jumla ya watu 477 kutoka nchi 39 walifika kwenye kimo cha kilomita 100 juu ya uso wa dunia ambacho ni kimo ambako anga-nje linaanza kulingana na maelezo ya Shirikisho la Kimataifa kwa Usafiri wa Angani (Fédération Aéronautique Internationale (FAI)).

Kati ya hawa ni 24 waliofika mbali kuliko kilomita 2,000 juu ya uso wa dunia hadi njia ya mwezi kwenye anga.

Mwanaanga aliyekaa muda mrefu angani alkuwa Mrusi Sergei Krikalyov aliyefika angani mara sita akakaa jumla ya siku 803, saa 9 na dakika 39 kwenye anga-nje.

Baina ya miaka 2001 hadi 2009 watu saba walifika kwenye anga-nje kama watalii yaani wageni waliolipia nafasi ya kusafiri pamoja na wanaanga hadi Kituo cha Anga cha Kimataifa (ISS) walipokaa kwa wiki moja. Walilipa zaidi ya dolar milioni 20. Mmojawao alikuwa Mark Shuttleworth wa Afrika Kusini.

NASA

NASA ni kifupi cha Kiingereza cha "National Aeronautics and Space Administration" (Mamlaka ya Marekani ya Usafiri wa Anga). Mamlaka hii ilianzishwa 1958. Wajibu wake ni kusimamia miradi ya serikali ya Marekani ya kuendesha utafiti na uchunguzi wa anga. NASA inasimamia utengenezaji wa roketi za kurusha vyombo vya angani na utengenezaji wa vyombo vya angani vyenyewe.

Miradi ya NASA ilianzishwa kutokana na Mshtuko wa Sputnik yaani baada ya Warusi kushtusha dunia kwa kupeleka vyombo vya angani vya kwanza katika mradi wao wa Sputnik. Uliofuatiwa na mradi wa "Vostok" ambao tarehe 12 Aprili 1961 ulimfikisha Yuri Gagarin angani akiwa mtu wa kwanza kwenda angani.

Mradi wa kwanza wa NASA ulikuwa Mradi wa Mercury uliotakiwa kuonyesha ya kwamba wanaanga wanaweza kukaa angani kwa muda fulani. Alan B. Shepard Jr. alikuwa Mmarekani wa kwanza angani kwa muda wa dakika 15; John Glenn alikuwa Mmarekani wa kwanza wa kuzunguka dunia tarehe 20 Februari 1962 kwa chombo cha angani "Friendship 7".

Mradi huo ulifuatiwa na Mradi wa Gemini kuanzia mwaka 1965 ulionyesha ya kwamba watu wanaweza kukaa angani kwa muda wa siku kadhaa hata kutekeleza shughuli fulani. Gemini iliandaa Mradi wa Apollo uliopeleka watu wa kwanza mwezini. Chombo cha angani "Apollo 11" kilifikisha wanaanga Neil Armstrong na Buzz Aldrin kwenye uso wa mwezi tarehe 20 Julai 1969 na kuwarudisha dunia tena.

Tangu mwanzo ule kuna miradi mingi iliyofuata.

Ndoto

Ndoto ni mfululizo wa picha, mawazo, mihemko na hisia ambao unatokea akilini, kwa kawaida bila makusudi, katika hatua fulanifulani za usingizi.Yaliyomo na malengo ya ndoto hayajaeleweka vizuri, ingawa tangu zamani yamejadiliwa sana katika sayansi (hasa elimunafsia) na katika dini. Fani inayochunguza ndoto kisayansi inaitwa onirolojia.Kwa kiasi kikubwa ndoto zinatokea wakati usingizini macho yanapogeukageuka zaidi, ambapo utendaji wa akili ni mkubwa karibu sawa na mtu anapokuwa macho. Zikitokea wakati mwingine wa usingizi, ndoto hazikumbukwi sana baada ya kuzinduka.Muda wa ndoto unaweza kuwa tofauti sana: tangu sekunde chache hadi dakika 20–30.Kwa wastani watu wanapata ndoto 3 hadi 5 kwa usiku, wengine hadi 7; lakini nyingi zinasahaulika mara au mapema. Watu wanaweza kukumbuka zaidi ndoto zao wakiamshwa wakati wa usingizi wa macho kugeukageuka.

Ndoto zinaelekea kudumu zaidi kadiri muda wa usiku unavyozidi kwenda.Ndoto zinaweza kuwa za aina mbalimbali: nje za uwezekano katika maisha ya kawaida, za ajabuajabu, za kutisha, za kusisimua, za kishirikina, za kidini, za kusikitisha, za kijinsia, n.k. Zinaweza pia kumsaidia msanii kubuni kitu.Kwa kawaida ziko nje ya udhibiti wa mtu, isipokuwa anapoota akiwa anajitambua (ndoto za mchana).Rai kuhusu maana ya ndoto zimetofautiana sana kadiri ya nyakati na utamaduni.Kumbukumbu za zamani zaidi kuhusu ndoto ni za miaka 5000 hivi iliyopita huko Mesopotamia, ambapo zilichorwa katika vigae.

Katika Ugiriki wa Kale na Roma ya Kale, watu walisadiki ndoto zinaleta ujumbe kutoka kwa mungu fulani au marehemu fulani na kwamba zinatabiri ya kesho.

Nyuzi

Nyuzi (pia: digrii kutoka neno la Kiingereza) ni kizio cha kupimia pembe . Msingi wake ni mzunguko kamili wa duara unaogawiwa kwa sehemu 360. Kwa kawaida nyuzi moja huandikwa kama 1°.

Nusuduara ina 180°. Pembemraba ina 90°. Jumla ya pembe ndani ya pembetatu ni 180°, ndani ya mstatili ni 360°.

Nyuzi inaweza kugawiwa tena kwa dakika na sekunde ya tao. Dakika ya tao ni sehemu ya 60 na sekunde ya tao ni sehemu ya 3600 ya nyuzi moja.

Peter Petrelli

Peter Petrelli, imechezwa na Milo Ventimiglia, ni jina la kutaja uhusika katika mfululizo wa ubunifu wa kisayansi kupitia televisheni ya NBC - maarufu Heroes. Ni mwuguzi wa jumba la watu mahututi ambaye amegeukia udaktari usaidizi akiwa katikati mwa miaka 20 akiwa na nguvu za kufyonza na kugezea nguvu za watu wengine wenye vipawa.

Mwepesi kuona jambo na vilevile ana huruma mno, awali uhusika ulionekana kuwa na uhusiano mgumu sana na ndugu yake ambaye ni Nathan. Tangu hapo, Peter Petrelli amekuwa akikabiliana na matokeo dhidi ya maamuuzi yanayotokana na vipawa vyake vinamtaka afanye. Mwanzoni mwa mfululizo wa "Heroes" Peter alifyonza kipawa cha mtu mwenye uwezo wa kuwa bomu linasubiri kulipuka.

Katika hekaheka za wahusika wote wa mfululizo walikuwa katika mbio za kuukoa mji New York City kwa hofu ya Peter atalipuka kama bomu la nyuklia. Dakika kadhaa kabla ya tukio ghafula anatokea ndugu yake Peter ambaye ni Nathan na kupaa nae angani na kuokoa watu wa jiji la New York City.

Saa

Kwa chombo cha kupimia wakati tazama saa (ala)

Saa ni kipimo cha wakati. Si kipimo cha SI kamili kama ilivyo sekunde lakini ni kawaida kote duniani pia katika matumizi ya kisayansi.

Saa inagawiwa kwa dakika 60 na sekundi 3,600. Siku ina takriban masaa 24.

Safari

Safari (kutoka Kar. ‏سفر‎ safar) ni neno la kutaja mwendo au harakati ya watu kutoka mahali fulani kwenda mahali pa mbali angalau kiasi. Safari inaweza kufanywa ama kwa miguu au kwa chombo cha safari au usafiri fulani. Kama safari inazidi muda wa siku mmoja vituo vya safari yaani mahali ambapo msafiri anakaa au analala hadi kuendelea ni sehemu za safari yake. Kuna safari ndefu na safari fupi. Harakati inayotumia muda mfupi tu kama dakika chache au kwa umbali mdogo huitwi safari isipokuwa kwa lugha ya kutaania.

Sauti

Sauti (kutoka Kiarabu صوت saut) inamaanisha kile tunachosikia kwa masikio yetu.

Kifizikia sauti ni uenezaji wa mabadiliko ya densiti na shinikizo katika midia kama kiowevu, gesi au gimba manga kwa njia ya wimbisauti.

Sekunde

Sekunde (alama: s; pia: nukta, sekundi, sekondi) ni kipimo cha wakati na kati ya vipimo vya kimsingi wa SI.

Kiasili ilihesabiwa kama sehemu ya 60 ya dakika moja lakini kisayansi inapimwa sasa kulingana na mwendo wa mnurulisho wa atomi za sizi -133.

Sekunde sitini (60) ni dakika moja, na sekunde elfu tatu na mia sita (3,600) ni saa moja.

Kisasili siku iligawiwa kwa masaa, masaa kwa dakika na dakika kwa sekundi. Imeonekana ya kwamba hesabu hii haitoshi kwa matumizi ya kisayansi kwa sababu muda wa siku si sawa kamili kutokana na mwendo wa dunia yetu. Hivyo kipimo kamili cha sekunde ilitafutwa kinachopimika katika fizikia na sasa muda wa vipimo vingine vya wakati inahesabiwa kwenye msingi wa sekunde siyo kinyume. Tokeo mojawapo ni ya kwamba siku hailingani tena kamili na masaa 24.

Kwa vipimo vya kisayansi ni muhimu kutaja sehemu za sekunde na hapa viambishi awali vya vipimo sanifu hutumiwa: milisekunde, nanosekunde, femtosekunde. Viambish awali kwa uwingi wa sekunde si kawaida.

Sekunde ya tao

Sekunde ya tao (ing. arc second) ni kipimo cha pembe. Inataja sehemu ya 3600 ya nyuzi moja.

Sekunde 60 za tao zinalingana na dakika moja ya tao. Dakika 60 za tao zinalingana na nyuzi moja. Nyuzi 360 ni sawa na duara kamili.

Kifupi chake ni arcsec au alama ya ".

Katika astronomia na upimaji wa Dunia pia kuna migawanyo midogo zaidi ya sekunde ya tao:

milisekunde ya tao au mas ni sehemu ya elfu moja (0.001″) ya sekunde moja ya tao

mikrosekunde ya tao au µas ni sehemu ya milioni moja ya sekunde ya tao.Kipimo cha kawaida cha umbali katika astronomia (pamoja na kizio astronomia na mwakanuru) ni parsek inayofafanuliwa kuwa umbali kati ya Jua na gimba la angani linaoonekana kwa pembe la paralaksi la sekunde moja ya tao (1 arcsecond).

Tony Almeida

Anthony "Tony" Almeida ni jina la uhusika wa kipindi cha televisheni cha Kimarekani maarufu kama 24. Uhusika ulichezwa na Carlos Bernard. Almeida, ni mmoja kati ya watu ambao Jack Bauer bado anawaamini hadi hapo ilipofikia umauti wake katika Msimu wa Tano. Tony anaonekana akifa mikononi mwa Bauer katika sehemu ya kumi na tatu ya msimu tano, lakini alifufuliwa baada ya dakika kumi kwa kutumia sindano ya hypothermic, na kurejea katika msimu wa saba.

Wakati

Wakati ni neno la kutaja ama ufuatano wa matokeo au muda ama kipindi ambamo jambo latokea.

Tunaishi katika wakati na tunapanga maisha yetu kufuatana na wakati lakini si rahisi kusema wakati ni kitu gani. Sayansi, fizikia, falsafa na dini zote zina njia mbalimbali za kuangalia na kueleza wakati.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.