Chokoleti


Chokoleti ni pipi au chakula kitamu kinachotengezewa kwa kutumia kakao, sukari na mafuta. Jina latumiwa pia kwa kinywaji cha kakao.

Chocolate
Aina mbalimbali za chokoleti
Cacao-pod-k4636-14
Mbegu za kakao ni chanzo cha chokoleti
JesusChocolate
Chokoleti hupokea kila umbo: Picha ya Yesu kwenye chokoleti

Historia ya chokoleti

Asili yake ni kinywaji wa watu wa Mexiko wa kale waliochemsha unga la kakao katika maji pamoja na viungo. Wahispania waliikuta kwa Azteki na kuipeleka Ulaya. Wakitumia hapa jina la Kiazteki "xocolātl" lenya maana ya "maji chungu".

Katika Ulaya ilitumiwa muda mrefu kama kinywaji na wakati wa karne ya 19 Wajerumani walianza kutengeneza pipi jinsi inavyojulikana leo.

Chokoleti huyeyuka haraka kwa sentigrefi 40-50 hivyo ni rahisi kuifinga kwa maumbo mbalimbali.

Hatua za kutengeneza chokoleti

 • Chanzo ni mbegu za kakao.
 • Hizi zinakaushwa, kukaangwa na kusagwa. Mbegu zinazosagwa zina kiasi kikubwa cha mafuta ndani yake.
 • Yote yakandamizwa na mafuta ya kakao yanatoka kando.
 • Keki ya kakao inabaki huwa ni msingi wa chokoleti.
  • Chokoleti nyeupe hutengenezwa kwa kutumia mafuta ya kakao pekee.
  • Chokoleti ya kawaida huongezwa tena kiasi fulani cha mafuta yake.
  • Chokoleti nyeusinyeusi hubaki bila nyongeza ya mafuta ya kakao.
  • Chokoleti hukorogwa mara nyingi na maziwa na sukari kuwa pipi inayopendwa.
Hydrox

Hydrox ni aina ya kuki iliyojazwa chokoleti ambayo ilianzishwa katika mwaka wa 1908 na ikatayarishwa na Kampuni ya Sunshine Biscuits. Jina lake la Hydrox linatokana na vipengele vya atomu vinavyounda maji: hasa haidrojeni na oksijeni. Baadhi ya ripoti kadhaa ,inasemekana kuwa Oreo ,iliyoanzishwa baadaye katika mwaka wa 1912, ilikuwa imeundwa ikiiga mfano wa Hydrox. Ingawaje, Hydrox imeshambuliwa na wengi kuwa bidhaa hii ilikuwa ikiiga Oreo. Ikilinganishwa na Oreo, kuki ya Hydrox ilikuwa inaonja "tamu kidogo" na ilikuwa ngumu na bora kuliwa na maziwa.

Kafeini

Kafeini (kutoka Kiingereza caffeine) ni dutu ya alkaloidi katika mimea mbalimbali hasa mbuni na mchai. Inaathiri neva za mwanadamu ikiondoa uchovu na kuamsha ubongo.

Matumizi yake ni hasa katika vinywaji vya kahawa, chai na kinywaji cha mate ya Amerika Kusini, lakini pia katika madawa ya tiba na vinywaji nishati (energy drinks).

Keebler (kampuni)

Kampuni ya Keebler ni kampuni ya pili kwa ukubwa ya kuzalisha kuki katika nchi ya Marekani.

Ilianzishwa katika mwaka wa 1853, imezalisha baadhi ya vitafunio vingi sana vya kuokwa. Keebler inauza bidhaa kama:

Cheez-Its(ambayo ina nembo ya Sunshine Biscuits)

Chips Deluxe,

Club Crackers,

EL Fudge Cookies,

Famous Amos Cookies,

Fudge Shoppe Cookies,

Murray,

Austin, Plantation,

Vienna Fingers,

Town House Crackers ,

Wheatables,

Sandie's Shortbread,

Zesta Crackers, miongoni mwa zingine.Kaulimbiu ya Keebler ni "Uncommonly Good" ikimaanisha nzuri sana kawa nji isiyoya kawaida. Tom Shutter na Leo Burnett ndio walioandika wimbo wa matangazo ya Keebler unaojulikana sana.

Kinahuatl

Kinahuatl (nāhuatl, mexìcatlàtōlli) ni kati ya lugha asilia za Mexiko zilizopo tangu wakati kabla ya kufika kwa Wahispania. Idadi ya wasemaji wa lahaja zake ni takriban milioni moja na nusu.

Ilikuwa lugha ya Waazteki, Watolteki na wengine wa nyanda za juu za Mexiko. Tangu kufika kwa ukoloni lahaja mbalimbali zilijitokeza si wasemaji wote wanaoelewa wasemaji wote wengine.

Maneno ya Nahuatl yalitaja mazao yaliyopelekwa kote duniani pamoja na majina yao. Kati ya maneno ya Nahuatl yaliyosambaa duniani ni:

(āhuacatl) avocado (parachichi)

(cacahuatl) kakao

(chīlli) chili (pilipili kali)

(xōchiyōcacahuatl) chokoleti

tequila (pombe kali ya kimeksiko)

(tomātl) tomato (nyanya)Majina ya nchi za Mexico, Guatemala na Nikaragua yana asili za Nahuatl.

Korosho

Korosho ni mbegu wa mkorosho ni mmea wa jamii ya mimea itoayo maua ya familia ya Anacardiaceae.

Korosho yenyewe inakua pamoja na tunda linaloitwa bibo ilhali mbegu unaonekana nje ya bibo.

Mmea huu ni wa asili ya kaskazini mashariki mwa Brazili, lakini sasa hukua sana maeneo ya tropiki, kwa ajili ya mbegu yake ya korosho na bibo zake.

Jina lake la Kiingereza limetokana na neno la Kireno ambalo lina asili ya Tupi.

Makala za msingi - orodha ya meta Feb 2008

Hii ni tafsiri ya orodha ya Kiingereza ya makala 1,000 za msingi kutoka meta:wikipedia ya Februari 2008.

Hadi sasa (2019) idadi kubwa imetafsiriwa, pia orodha imebadilishwa mara kadhaa. Mapengo ya sasa ni machache, kwenye Septemba 2019 ni yafuatayo: , physical chemistry , conservation of energy , classical mechanics , strong interaction , weak interaction , quantum mechanics , general relativity , mathematical analysis , differential equation , numerical analysis , function , infinity , mathematical proof , set theory , capacitor , inductor , operating system , programming language , video game

Pamoja na haya ya juu, inafaa tuangalie sasa orodha ya orodha ya makala 10,000 za msingi kutoka meta:wikipedia. Hapo tumeshapata karibu makala 4,000, lakini bado zaidi kidogo ya 6,000 zinakosekana. Hata kama si kila moja ni mada ya kuvutia sana, bado makala hizi ni kiunzi cha elimu ya msingi! Karibuni kuchangia. Wanaopenda jiografia, basi mtumie orodha ya sehemu yake iliyoswahilishwa kisehemu Mtumiaji:Kipala/10000_list_Geography na jitahidini kumaliza maneno mekundu. Kipala (majadiliano) 22:25, 21 Septemba 2019 (UTC)

Milo (kinywaji)

Milo (IPA / maɪləʊ /) ni kinywaji kilicho na maziwa, chokoleti na malt, zilizotayarishwa na kampuni ya Nestlé na asili yake ni Australia. Ilitengenezwa mara ya kwanza na Thomas Mayne mwaka 1934. Milo pia inatayarishwa katika nchi nyingine zikiwemo Singapore, Malaysia, China, Thailand, Indonesia, Ufilipino, Vietnam, New Zealand, Hong Kong, Japan, Jamaika, Guyana, Trinidad na Tobago, Chile, Kolombia, Peru, Nigeria, Kenya, Ghana , Papua Guinea Mpya, Afrika ya Kusini, Sri Lanka, Syria, Taiwan na Uingereza.

Jina lilitokana na Mgiriki mwanamichezo maarufu Milo wa Croton kwa sababu ya nguvu yake.

Mkakao

Mkakao (Theobroma cacao) ni mti ambao maua na kwa hivyo matunda yake yamea juu ya shina au matawi. Kokwa hutumika kwa kutengeneza chokoleti.

Mto Suir

Mto Suir Irish pronunciation: [ʃuːr] Irish An tSiúr au Abhainn na Siúire) ni mto nchini Ireland ambao unatiririka hadi katika Atlantiki karibu na Waterford baada ya umbali wa kilomita 184 ( maili 114 ).Ukubwa kwa jumla ni3526 km2. Maarufu kwakujikunja,una hifadhi nyingi za aina wa samaki wa traut wa kahawia . Pia Suir inashikilia rekodi ya Salmoni walioshikwa kutoka mto huu wa irelando, (uzito wa kilo 57 lb/26 , katika mwaka 1874) kama ilivyo katika mito mingine ya Atlantiki , Idadi ya salmoni imekuwa ikipunguka katika miaka iliyopita.

Unaoanzia katika miteremko ya Mlima wa Ibilisi, kaskazini ya Templemore katika Kata ya Tipperary, mto Slur huelekea kusini kupitia kupitia Loughmore, Thurles, Holycross, Golden na Knockgraffon. Huungana na Mto Aherlow katika Kilmoyler na baadaye na Tar, hupinduka mashariki katika milima ya Comeragh na kutengeneza mpaka kati ya kata ya Waterford na kata ya Kilkenny. Baadaye hupitia Cahir, Clonmel na Carrick-on-Suir kabla ya kufika Waterford. Hapa,hupatana na Mto Barrow na Mto Nore kuunda kinywa pana kinacho uwezo wa kupitiwa na vyombovya majini.

Pamoja na Nore na Barrow, mto ni huu ni moja wa mito inayojulikana kama Dada Watatu.

Suir inajulikana i katika ireland kama Siúr na hudhaniwa katika matamshi yake ya kisasa ya Kiingereza yakiwa na u na i kupinduliwa kulitokana na makosa. Basi, baadhi ya watuhuhisi kwamba matamshi katika Kiingereza yanafaa kuwa Siur na matamshi haya huonekana mara kwa mara.. Edmund Spenser (1552-1599) mwandishi wa The Fairie Queene, katika maandiko yake wakati wa Kipindi cha Elizabethan katika kata ya Cork, yaliashiria'mpole Shure', pengine matamshi sahihi zaidi na sahihi zaidi katika kipindi hicho.

Katika miaka ya kwanza ya karne ya 21, mabakishi ya makazi yaViking yalipatikana katika ufuko wa mto huu juu ya Waterford.

Katika Clonmel, Suir huwa na mafuriko katika eneo la mtaa baada ya mvua kubwa sana katika vyanzo vya juu vya 2,173 km2. Ofisi ya kazi za umma, kwa kimombo (OPW), ilikamilisha na kuweka mfumo wa kutabiri mafuriko ambao ulitumika kutabiri mafuriko katika Januari mwaka wa 2008 na Januari mwaka wa 2009, mafuriko ya Januari mwaka wa 2009 kuwa tukio 1 katika kipindi cha miaka 5. Awamu ya 1 ya ulinzi wa mafuriko ya Clonmel (1-100 mwaka) ambayo ilitajwa katika mwaka wa 2007 ilipangiwa kumalizika mwishoni mwa mwaka wa 2009 na awamu ya pili na tatu kama mkataba mmoja wa 2011/2012. Ulinzi wa Gharika unahusisha vikwazo, kuta na ufuko wa ardhi. Daraja Gashouse , Coleville Road, Davis Road, ya quays na Old Bridge ni ujumla maeneo yaliyoathirika zaidi.

Clonmel Haina mawimbi. Mawimbi hupindukia juu ya kiwanda cha chokoleti cha Miloko katika Carrick-on-Suir. Maji ya mafuriko hutapakaa kwenye ardhi juu Miloko katika upande Waterford ya mto kwenye nchi.

Carrick-katika-Suir ni wimbi na lina miaka 1-50 ya ulinzi wa mafuriko. Ofisi ya kazi za umma (OPW) ina mpango wa kuweka ulinzi wa mwaka 1-200 mafuriko ambapo mto Suir unapitia Waterford mji.

Ambapo mto unapita katika Kata ya Kilkenny kusini, karibu na mji wa Mooncoin, ulijulikana kama moja ya baladi maarufu zaidi iitwayo, The Rose wa Mooncoin, ambayo inajumuisha "ufuko wa Suir,unaenda chini hadi kwa Mooncoin".

Penguin (Biskuti)

Biskuti ya Penguin ni aina za biskuti zilizopakwa chokoleti ndani na nje. Zinatayarishwa na sehemu ya kampuni ya United Biscuits ya McVitie's. Biskuti za Tim Tam zilizotayarishwa na Arnott's,Australia ilipikwa kwa njia moja na zile za Australia na ikazua mjadala mkali kuhusu biskuti gani ndizo bora zaidi kati ya hizo mbili.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.