Brazil


Brazil ni nchi kubwa ya Amerika ya Kusini na pia ni nchi yenye wakazi wengi kushinda nchi zote za bara hilo. Eneo lake ni karibu nusu ya bara lote.

Imepakana na Uruguay, Argentina, Paraguay, Bolivia, Peru, Kolombia, Venezuela, Guyana, Surinam na eneo la Guyana ya Kifaransa.

Brazil ina pwani ndefu kwenye bahari ya Atlantiki.

Mji mkuu ni Brasilia, uliopangwa na kujengwa kati ya 1957 na 1960. Mji mkubwa ni Sao Paulo.

República Federativa do Brasil
Shirikisho la Jamhuri ya Brazil
Bendera ya Brazil Nembo ya Brazil
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Ordem e Progresso
(Kireno kwa "Utaratibu na Maendeleo")
Wimbo wa taifa:
Ouviram do Ipiranga as margens plácidas
("Kando ntulivu za Ipiranga zilisikia...")
Lokeshen ya Brazil
Mji mkuu Brasília
15°45′ S 47°57′ W
Mji mkubwa nchini São Paulo
Lugha rasmi Kireno
Serikali
Rais
Shirikisho la Jamhuri
Jair Bolsonaro
Uhuru
Ilitangazwa
Ilitambuliwa
Jamhuri

7 Septemba 1822
29 Agosti 1825
15 Novemba 1889
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
8,515,767 km² (ya 5)
0.65
Idadi ya watu
 - 2014 kadirio
 - 2000 sensa
 - Msongamano wa watu
 
202,768,562 (ya 5)
169,799,170
23.8/km² (ya 182)
Fedha Real (BRL)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC-2 to -5 (Official: -3))
(UTC)
Intaneti TLD .br
Kodi ya simu +55

-

Jiografia

Misitu mipana ya dunia inapatikana Brazil katika beseni ya mto Amazonas. Misitu hii inafunika takriban 40% ya eneo la nchi.

Idadi kubwa ya wakazi hukalia maeneo karibu na pwani ya Atlantiki.

Kitovu cha kilimo ni nyanda za "cerado" au savana katika magharibi ya kati ya Brazil.

Milima

Corcovado statue01 2005-03-14
Mlima wa Corcovado na sanamu ya Yesu Mwokozi (Rio de Janeiro)

Mlima mkubwa ni Pico da Neblina (mita 3,014 juu ya UB) pamoja na Pico 31 de Março (mita 2,992) ulio karibu nao kwenye mipaka ya Brazil, Venezuela na Guyana.

Mlima mkubwa wa kusini ni Pico da Bandeira (mita 2.891).

Mlima unaojulikana zaidi si mkubwa lakini uko ndani ya mji wa Rio de Janeiro: ni Corcovado wenye mita 710. Juu yake kuna sanamu ya Yesu Kristo ambayo ni ishara ya mji.

Mito muhimu

Amazonas
Ramani ya mwendo wa Amazonas inayovuka bara lote.

Brazil ina mto mkubwa na mrefu wa dunia ambayo ni Amazonas wenye urefu wa takriban kilometa 7000. Tawimito yake muhimu ni Río Purús, Rio Negro na Rio Tapajós.

Katika mashariki kuna mto Iguaçu wenye maporomoko ya Iguaçu ambayo ndiyo makubwa duniani.

Iguacu-001
Maporomoko ya Iguaçu karibu na mpaka wa Argentina/Brazil/Paraguay
Caminhada com Maria
Fortaleza

Parana (3.998 km) ni mto mrefu duniani baada ya Amazonas. Unalisha kituo kikubwa cha nishati ya maji duniani cha Itaipú.

Lagoa dos Patos karibu na Porto Alegre ni wangwa kubwa la Brazil lenye 10.000 km².

Ipiranga si mto mkubwa, hata kama jina lake linapatikana katika wimbo wa taifa.

Visiwa

Brazil ina visiwa vichache vidogo katika Atlantiki kama vileː

  • Penedos de São Pedro e São Paulo (miamba ya Mt. Petro na Mt. Paulo)
  • Kisiwa cha matumbawe cha Rocas
  • Fernando de Noronha
  • Trindade e Martim Vaz

Visiwa hivyo ni sehemu ya mgongo kati wa Atlantiki; hali halisi ni vilele vya milima inayoanza kwenye msingi wa bahari.

Kisiwa kikubwa cha Brazil hakipo baharini bali kati ya mto Amazonas: ni Marajó, chenye eneo la km² 48.000 (kubwa kushinda eneo la Uswisi).

Hali ya hewa

Hali ya hewa ni ya kitropiki isipokuwa kusini.

Beseni ya Amazonas ina mvua nyingi. Kwenye milima ya kusini usimbishaji unaweza kutokea kama theluji.

Miji muhimu

Centro SP2
São Paulo inazidi wakazi milioni 20
Rio night
Rio de Janeiro
ViewCuritiba.BotanicalGarden.Day
Curitiba, kusini mwa Brazil

Jiji kubwa ni São Paulo linalofikia (pamoja na mitaa ya jirani) kwenye idadi ya wakazi milioni 20.5.

Majiji ya kufuata ni Rio de Janeiro (wakazi milioni 11.4), Belo Horizonte (wakazi milioni 4.3), Curitiba (wakazi milioni 4), Recife (wakazi milioni 3.6), Brasilia (wakazi milioni 2.9), Salvador da Bahia (wakazi milioni 2.9), Fortaleza (wakazi milioni 2.6).

São Paulo ni jiji kubwa kabisa linalokua haraka sana. Ni moyo wa uchumi wa Brazil wenye viwanda vingi.

Rio de Janeiro ilikuwa mji mkuu wa nchi hadi kuanzishwa kwa Brasilia. Imejulikana kote duniani kutokana na uzuri wa mazingira yake na sherehe ya Kanivali. Ina pia viwanda muhimu na ni kitovu cha utamaduni wa nchi.

Mji mkuu wa Brasilia ulijengwa kama ishara ya umoja wa nchi katika miaka mitatu tu.

Jumla ya asilimia 70 za wakazi hukalia miji mikubwa. (Angalia Orodha ya miji ya Brazil.)

Historia

Brazil imekaliwa na watu tangu miaka 10,000 iliyopita. Waindio waliingia kutoka kaskazini. Hakuna taarifa za kimaandishi lakini akiolojia imeweza kufumbua makazi mbalimbali ya wenyeji asilia.

Ukoloni

Brazil ilikuwa koloni la Ureno hadi mwaka 1822 kutokana na mkataba wa Tordesillas ambamo Hispania na Ureno zilipatana tarehe 5 Septemba 1494 kuhusu ugawaji wa dunia kati yao baada ya fumbuzi za Kolumbus.

Mreno wa kwanza aliyefika mwambao wa Brazil tarehe 22 Aprili 1500 alikuwa Pedro Alvares Cabral. Makazi ya kwanza ya Wareno ni mji wa São Vicente mwaka 1532. Mji mkuu wa kwanza ulikuwa bandari ya Salvador da Bahia tangu 1549.

Wareno walianzisha kilimo cha miwa wakiwalazimisha Waindio kuwafanyia kazi. Walianza kuingia ndani ya bara wakitafuta watumwa kwa ajili ya mashamba na dhahabu.

Hali ya Waindio

Wenyeji walipungua haraka kwa sababu ya kuambukizwa magonjwa ya kigeni wakikosa kinga dhidi yake, halafu kutokana na kutendewa vibaya kama watumwa mashambani.

Wareno walianza kutafuta wafanyakazi penginepo kwa kuchukua watumwa kutoka Afrika.

Mapadri Wajesuiti

Katika hali hiyo wamisionari Wakristo wa Shirika la Yesu walisimama upande wa Waindio. Walijipatia tamko rasmi la Papa wa Roma la kuwa Waindio ni binadamu kamili, hivyo hawafai kutendewa kinyama. Wakibatizwa na kuwa Wakristo walitakiwa kukubaliwa kama raia yeyote wa Ureno – amri ambayo mara nyingi haikukubaliwa na wavindaji wa watumwa na wenye mashamba.

Mapadri wa Shirika la Yesu walianzisha „reduciones“ yaani vijiji na miji kwa ajili ya Waindio walioishi chini ya ulinzi wao na kutetewa dhidi ya wavindaji wa watumwa. Katika makazi hayo Waindio walifundishwa shule kwa lugha za kienyeji na Kireno, na kupata mafunzo wa ufundi mbalimbali. Kwa namna hiyo mapadri hao walitawala maeneo makubwa ndani ya bara.

Hali hiyo ilisababisha hasira ya wanasiasa Wareno walioendelea kuwapinga hadi Ureno penyewe. Hatimaye mwaka 1767 hao mapadre Wajesuiti walilazimishwa kuondoka katika Ureno na makoloni yake yote.

Upanuzi wa Brazil

Karne ya 17 na ya 18 iliona kuanzishwa kwa miji mizuri kwa sababu dhahabu na almasi zilivumbuliwa katika misitu ya beseni ya Amazonas. Misafara ya kutafuta hazina hizi zilipanua eneo la Brazil kuelekea magharibi.

Mji mkuu ulihamishwa kwenda Rio de Janeiro mwaka 1763.

Uhuru 1822

Uhuru wa Brazil ulisababishwa na siasa za Ulaya. Mwaka 1807 Ureno ilivamiwa na Ufaransa ya Napoleon Bonaparte. Mfalme wa Ureno João VI alikimbilia Brazil, Rio de Janeiro ikawa mji mkuu wa dola la Ureno.

Mfalme aliporudi Ureno mwaka 1821 alimwachia mtoto wake Pedro utawala wa Brazil. Mwaka 1822 Pedro aliyeona mabadiliko ya kimapinduzi katika makoloni ya Hispania kote Amerika ya Kusini aliamua kutangaza uhuru wa Brazil akiwa mwenyewe mfalme kwa cheo cha Kaisari.

Watu

Kutokana na historia ya nchi, wakazi wengi wana asili ya Ulaya (47.7%) au ni machotara (43.1). Asilimia 7.6 wana asili ya Afrika tu.

Wakazi walio wengi hutumia lugha ya Kireno, lakini kuna lugha nyingi kwa sababu ya vikundi vya wenyeji asilia (Waindio) na wahamiaji kutoka pande zote za dunia.

Asilia 64.6 ya wananchi wanafuata imani ya Kanisa Katoliki. Ndiyo nchi yenye Wakatoliki wengi kuliko zote duniani. Waprotestanti ni asilimia 22.2.

Tazama pia

Viungo vya nje

Nchi na maeneo ya Amerika Kusini

Argentina | Bolivia | Brazil | Chile | Ekuador | Guyana | Guyana ya Kifaransa | Kolombia | Paraguay | Peru | Surinam | Uruguay | Venezuela

Map of Brazil with flag.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Brazil bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Brazil kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
1990

Makala hii inahusu mwaka 1990 BK (Baada ya Kristo).

Amerika ya Kusini

Amerika ya Kusini ni bara la magharibi ambalo kwa kiasi kikubwa sana linaenea upande wa kusini wa Ikweta.

Inapakana na Bahari ya Pasifiki upande wa Magharibi, na Bahari ya Atlantiki upande wa Mashariki.

Kaskazini inaunganika na Amerika ya Kaskazini kwa njia ya shingo ya nchi ya Panama.

Argentina

Argentina ni nchi kubwa ya pili ya Amerika Kusini. Ina eneo la km² 2,780,400 kati ya milima ya Andes upande wa magharibi na Bahari ya Atlantiki upande wa mashariki.

Imepakana na Paraguay, Bolivia, Brazil, Uruguay na Chile.

Kuna madai dhidi ya Uingereza juu ya visiwa vya Falkland (Malvina), Visiwa vya South Georgia na South Sandwich na sehemu ya Antaktika.

Atlantiki

Atlantiki ni bahari kubwa inayotenganisha Amerika upande wa magharibi na Afrika na Ulaya upande wa mashariki. Eneo lake ni kilometa za mraba 106,200,000 au sehemu ya tano ya uso wa dunia pamoja na bahari za pembeni kama bahari ya Baltiki na Mediteranea. Hivyo ni bahari kubwa ya pili duniani baada ya Pasifiki. Bila bahari hizi za pembeni eneo lake ni kilometa za mraba 82,400,000.

Beseni yake ina umbo kama "S". Kina ya wastani ni mita 3,332; kina kikubwa katika mfereji wa Puerto Rico kinafikia mita 8,605. Upana wa bahari ni kati ya km 2,648 kati ya Brazil na Liberia hadi km 4,830 kati ya Marekani na Afrika ya Kaskazini.

Kuna ghuba nyingi pamoja na bahari za pembeni. Atlantiki inabadilishana maji yake na Pasifiki na Bahari Hindi hasa kusini ya mabara ya Afrika na Amerika ya Kusini.

Bolivia

Bolivia (jina linatokana na shujaa Simon Bolivar) ni nchi isiyo na mwambao wa bahari katika Amerika Kusini.

Imepakana na Brazil, Paraguay, Argentina, Chile na Peru.

Kaskazini

Kaskazini ni moja kati ya mielekeo minne mikuu ya dira. Mwelekeo wake ni ncha ya kaskazini ya dunia. Kinyume chake ni kusini.

Jina "kaskazini" limetokana na neno la Kiarabu "قيظ qiz" joto na "قيظ قائظ qiz qaez" hali ya hewa lenye joto sana; kutoka sehemu za Zanzibar au Uswahilini kwenda kaskazini kuelekea Somalia joto linaongezeka sana; upepo wa joto latokea huko.

Kaskazini kawaida huwa juu zaidi kwenye ramani. Kanada ipo kaskazini mwa nchi ya Marekani, Venezuela ipo kaskazini mwa nchi ya Brazil, na Urusi ipo kaskazini mwa nchi ya India. Ncha ya kaskazini ni kaskazini ya mbali unayoweza kwenda.

Kiitalia

Kiitalia ("Lingua italiana" au "Italiano") ni lugha inayozungumzwa na watu milioni 85, hasa katika Rasi ya Italia.

Ni lugha rasmi ya Italia, San Marino, Vatikano, Uswisi na katika sehemu za Slovenia na Kroatia.

Inatumika pia katika Monako, Malta, Albania na visiwa kadhaa vya Ugiriki), halafu bado kama lugha ya elimu katika nchi zilizokuwa makoloni ya Italia kama Eritrea, Libya, Ethiopia na Somalia.

Watu wengi wanaokitumia kama lugha mama wamekisambaza katika nchi zote walikohamia, kama vile Ujerumani, Ufaransa, Ubelgiji, Marekani, Kanada, Brazil, Uruguay, Argentina, Venezuela, Australia n.k.

Ni ya 4 kati ya lugha za kigeni zinazosomwa zaidi duniani, hasa kwa sababu ya umuhimu wake katika ustaarabu, kuanzia muziki, lakini pia katika biashara, k.mf. ya bidhaa za utamaduni wa Italia.

Kihistoria asili yake ni lugha ya Kilatini, hivyo pamoja na Kifaransa, Kihispania, Kireno, Kiromania na lugha nyingine ndogo ni moja ya lugha za Kirumi. Kati ya lugha hizo, Kiitalia ndicho kinachofanana zaidi na Kilatini, labda baada ya Kisardinia.

Imegawanyika katika lahaja nyingi, hasa za Kaskazini na za Kusini mwa rasi hiyo. Imesanifiwa kwa msingi wa lahaja ya Firenze (mkoa wa Toscana, Italia ya Kati).

Kijerumani

Kijerumani (pia: Kidachi, kwa Kijerumani: Deutsch au (die) deutsche Sprache) ni lugha ya Kigermanik ya magharibi katika jamii ya lugha za Kihindi-Kiulaya.

Huzungumzwa hasa katika nchi za Ujerumani, Austria, Uswisi, Liechtenstein na Luxemburg.

Kuna pia wasemaji asilia katika nchi jirani za Ujerumani / Austria kama Ubelgiji, Uholanzi, Ufaransa, Denmark, Poland na Italia ya kaskazini. Nchi nyingi za Ulaya ya Mashariki zilikuwa na wasemaji wa Kijerumani lakini wengi walifukuzwa au kuondoka wakati wa vita kuu ya pili ya dunia; vikundi vimebaki hasa katika Hungaria, Romania, Uceki, Urusi na Kazakhstan.

Vikundi vidogo vya watu waliohamia katika karne za 19 na 20 wanaoendelea kutumia Kijerumani wako katika Amerika ya Kaskazini (Marekani, Kanada), Amerika Kusini (Brazil, Chile) na Afrika (hasa Namibia na Afrika Kusini).

Kijerumani huzungumzwa na watu milioni 100 katika Ulaya. Ni lugha ya pili katika Ulaya baada ya Kirusi kushinda Kifaransa na Kiingereza.

Kolombia

Kolombia (kwa Kihispania: República de Colombia) ni nchi kwenye pembe la kaskazini la Amerika ya Kusini.

Imepakana na Venezuela, Brazil, Ekuador, Peru na Panama. Ina pwani mbili, kwenye Pasifiki na Atlantiki.

Jina la nchi limeteuliwa kwa heshima ya Kristoforo Kolumbus (Kihisp.: Cristóbal Colón; kwa Kiitalia: Cristoforo Colombo) aliyegundua njia kati ya Hispania na Amerika mwaka 1492.

Mji mkuu

Mji mkuu kwa kawaida ni mji wenye makao makuu ya serikali ya nchi fulani. Katika nchi nyingi mji huo ni pia mji mkubwa na muhimu zaidi kushinda miji mingine nchini. Huo ni sehemu yenye maendeleo makubwa sana katika nchi yoyote: ina kila huduma muhimu na miundombinu iliyo bora. Mfano: nchini Tanzania mji mkubwa ni Dar es Salaam, ingawa makao makuu ni Dodoma.

Kuna nchi ambako mji mmoja umeteuliwa kuwa mji mkuu katika katiba au kwa sheria fulani. Kumbe kuna nchi nyingine ambako hakuna sheria yoyote lakini makao makuu yanaeleweka yapo mji fulani.

Nchi kadhaa zimeteua mji fulani kuwa mji mkuu kwa shabaha ya kubadilisha mwendo wa nchi au kama jaribio la kusahihisha historia yake.

Orodha ya Makardinali

Orodha ya makardinali wa Kanisa Katoliki huonyesha makardinali wote ambao walikuwepo tarehe 24 Novemba 2007.

Papa ana haki ya kumteua kardinali bila ya kutangaza jina lake. Uteuzi huu huitwa "in pectore" (kilatini "moyoni"). Hii inaweza kutokea hasa kama ni kardinali kutoka nchi pasipo uhuru wa kidini au nchi ambayo haina uhusiano mzuri na kanisa katoliki. Tarehe hii hakuwepo yeyote wa namna hiyo.

Majina yamepangwa kufuatana na bara na nchi.

Peru

Peru (pia Peruu) ni nchi ya Amerika Kusini upande wa magharibi ya bara.

Imepakana na Ekuador, Kolombia, Brazil, Bolivia na Chile. Kuna mwambao wa Pasifiki.

Rio de Janeiro

Rio de Janeiro ni jiji kubwa la pili nchini Brazil baada ya São Paulo.

Ilikuwa mji mkuu wa nchi hadi tarehe 21 Aprili 1960. Leo ni mji mkuu wa jimbo la shirikisho la Rio de Janeiro. Mwaka 2000 rundiko la jiji lilikuwa na wakazi 5,473,909.

Rio de Janeiro ni jiji la Brazil linalojulikana zaidi kote duniani. Ni kitovu cha utalii na cha utamaduni. Kanivali yake inavuta wageni wengi kila mwaka. Mlima wa Corcovado unabeba Sanamu ya Mwokozi ambayo ni sanamu kubwa ya Yesu yenye kimo cha mita 30.

Sinop

Sinop inaweza kutaja maana zifuatazo:

Sinop (Uturuki), ni mji uliopo karibu na Bahari Nyeusi huko nchini Uturuki.

Jimbo la Sinop, ni jimbo la nchini Uturuki ambalo mji wake mkuu ni huo uliotajwa hapo juu.

Sinop, Mato Grosso, mji uliopo katika jimbo la Mato Grosso huko nchini Brazil

São Paulo

São Paulo (Kireno: Mt. Paulo) ni jiji kubwa la Brazil pia jiji kubwa katika nusudunia ya kusini lenye wakazi zaidi ya milioni 10 jijini au karibu milioni 20 katika rundiko la jiji.

Venezuela

Venezuela ni nchi kaskazini mwa Amerika ya Kusini.

Imepakana na Brazil, Guyana na Kolombia.

Mbele ya pwani ya Bahari ya Karibi kuna madola ya visiwani ya Aruba, Antili za Kiholanzi na Trinidad na Tobago.

Venezuela ilikuwa koloni la Hispania hadi mwaka 1811 na lugha ya Kihispania ni lugha ya kitaifa.

Kikatiba Venezuela ni shirikisho la jamhuri.

Mji mkuu ni Caracas.

Jumuia ya Nchi za Lugha ya Kireno (CPLP)
Members
Observers
In Process

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.