Berkeley, California

Berkeley ni mji wa Marekani katika jimbo la California. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mnamo mwaka wa 2000, mji una wakazi wapatao 100,000 wanaoishi katika mji huu. Mji upo m 0-400 kutoka juu ya usawa wa bahari.

California blank map.svg Makala hii kuhusu maeneo ya California bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Berkeley, California kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Berkeley
Berkeley, California
Berkeley, California
Berkeley is located in Marekani
Berkeley
Berkeley
Mahali pa Berkeley katika Marekani
Majiranukta: 37°52′18″N 122°16′22″W / 37.87167°N 122.27278°W
Nchi Marekani
Jimbo California
Wilaya Alameda
Idadi ya wakazi
 - 102,743
Tovuti: www.CityofBerkeley.info
Alameda County California Incorporated and Unincorporated areas Berkeley Highlighted
Mahali pa Berkeley katika California
Telegraph-Ave-Berkeley
Telegraph Avenue
Amfetamini

Amfetamini ni dawa ya kuchochea akili inayojulikana kusababisha ukosaji wa usingizi na kupunguza uchovu na hamu ya chakula.

Amfetamini inahusiana kikemikali na metamfetamini na lisdeksamfetamini, kategoria ya dawa zenye nguvu zinazofanya kazi kwa kuongeza viwango vya dopamini na norepinephrine katika ubongo, na kusababisha furaha nyingi. Kategoria hii inashirikisha dawa zinazotumiwa kwa maagizo ya daktari za CNS ambazo kwa kawaida hutumiwa kutibu ugonjwa wa kutomakinika na hamasa ya kupindukia (ADHD). Aidha, dawa hizi hutumiwa kutibu dalili za majeraha ya ubongo yanayotokana na mgongano (TBI) na dalili za kusinzia mchana zanarkolepsi, tatizo la mkao la orthostatiki takikadia (POTS) na dalili za uchovu sugu (CFS). Hapo awali, amfetamini ilitumiwa na watu wengi kupunguza hamu ya chakula na kudhibiti uzito wa mwili. Majina chapa ya dawa ambazo zina amfetamini, au zinazabadilika na kuwa amfetamini ni pamoja na Adderall, Vyvanse, na Dexedrine, pamoja na Benzedrine hapo mbeleni.

Dawa hii pia hutumiwa kama kiburudisho na kiimarisha utendaji. Wale wanaoitumia dawa hii kujiburudisha wawameibunia majina mengi ya mitaani, kama vile speed na crank. Kituo cha Ufuatiliaji wa Dawa na Dawa za Kulevyacha Ulaya kinaripoti kuwa bei ya kawaida ya rejareja ya amfetamini katika Ulaya ni kati ya €3 na €15 (USD $4 hadi $21.55 ) kila gramu katika nusu ya nchi zinazoripoti. Jina amfetamini lina asili yake katika jina la kemikali zilizo kwenye dawa hii: a-m ethyl lpha pH et en hyl amini.

Maana yake ni aina ya madawa ya kulevya yenye kuchangamsha na kusisimua mwili. Licha ya hiyo, inashauriwa wanajamii wasitumie dawa za namna hiyo katika maisha yao kwa kuwa huweza kuathiri ubongo wa binadamu kwa kiasi kikubwa.

Berkley

Berkley au Berkeley ni jina la:

Berkley:

Berkley, Massachusetts

Berkley, MichiganBerkeley:

Berkeley, California

Xander Berkley

Kaboni 14

Kaboni 14 ni isotopi ya mionzi ya kaboni na kiini cha atomi ambacho kina protoni 6 na neutroni 8. Kuwepo kwake katika vifaa vya kikaboni ni msingi wa mbinu ya rediokaboni iliyopangwa na Willard Libby na wenzake (1949) kupimia umri wa sampuli za akiolojia, jiolojia na hidrojiolojia.

Kaboni-14 iligunduliwa na Martin Kamen na Sam Ruben tarehe 27 Februari 1940, katika Radiation Laboratory ya Chuo Kikuu cha California huko Berkeley, California, Marekani. Hata hivyo uwepo wake uliwahi kupendekezwa na Franz Kurie mwaka wa 1934.

Kuna isotopi tatu za asili zinazotokea duniani:

99% ya kaboni ni kaboni-12,

1% ni kaboni-13, na

kaboni-14 hutokea kwa kiasi cha kufuatilia, yaani, juu ya 1 au 1.5 atomi kwa atomi 1012 ya kaboni katika anga.Kaboni-12 na kaboni-13 ni imara, wakati nusu ya maisha ya kabon-14 ni miaka 5,730 ± 40. Kuoza kwa kaboni-14 katika nitrojeni-14 kwa kuharibika kwa beta. Gramu ya kaboni yenye atomu 1 ya kaboni-14 kwa atomi 1012 itatoa chembe za beta 0.2 kwa pili.

Chanzo cha asili cha kaboni-14 duniani ni athari ya mionzi kutoka angani juu ya nitrojeni ya anga, na hivyo ni "nuclide cosmogenic". Hata hivyo, kupima kwa nyuklia kati ya 1955-1980 ilichangia kwenye bwawa hili.

Khoikhoi

Khoikhoi (kwa lugha yao maana ni "watu watu", "watu halisi") ni wakazi asili wa Kusini mwa Afrika pamoja na Wasan, ambao kwa jumla wanaitwa Khoisan.

Tofauti kati yao ni hasa utamaduni, kwa maana Wasan wanaendelea kwa kiasi kikubwa kuishi kwa uwindaji, wakati Khoikhoi toka muda mrefu wanategemea ufugaji na kilimo.

Kadiri ya akiolojia walifikia eneo la Cape Town miaka 2,000 iliyopita wakitokea kaskazini (Botswana ya leo).

Kuanzia karne ya 3 BK walifikiwa na wavamizi wa Kibantu waliojitwalia maeneo mazuri zaidi.

Manga

Manga (ja: 漫画 kanji: まんが katakana: マンガ English: /ˈmɑːŋɡə/) ni hadithi zinazotungwa kwa kutumia michoro (wakati mwingine pia hujulikana kama komikku katika lugha ya Kijapani. Hufuata jinsi ya kuchora ulioendelezwa Ujapani mwishoni mwa karne ya 20. Katika namna zake za kisasa, manga zilianza muda mfupi baada ya Vita vikuu vya pili , lakini aina hii ya sanaa ina historia ndefu katika miaka awali ya sanaa ya Ujapani.

Katika Ujapani, watu wa umri wote husoma manga. Manga ni aina ya sanaa inayojumuisha mapana ya mada kama vile: "action-adventure", mapenzi (kWa Kiingereza romance), michezo (sports and games), drama za kihistoria (historicsl dramas), vichekesho (comedy), hadithi ya chuku yanayohusu sayansi (science fiction), fumbo (mystery), hadithi ya kutisha (horror), ngono (sexuality), na biashara (business and commerce), miongoni mwa nyingine. Tangu miaka ya 1950, manga imekua na kujiendeleza hadi sasa inawakilisha sehemu kubwa ya sekta ya kuchapisha humo Ujapani, ni sekta iliyowakilisha yen bilioni 406 katika soko nchini Japan mnamo mwaka 2007 (wastani wa dola bilioni 3.6). Manga imekuwa maarufu duniani kote pia. Mwaka wa 2008, soko la manga katika nchi za Marekani na Kanada ilikuwa $ milioni 175.

Manga kwa kawaida huchapishwa bila rangi, yaani huwa nyeusi-na-nyeupe, ingawa kuna baadhi ya manga zinazochapishwa kutumia rangi zote. Katika Ujapani, manga kawaida huchapishwa katika vitabu vyenye kurasa nyingi, huenda vitabu hivi huhusisha hadithi tofauti, na kila hadithi huendelezwa katika suala la kufuata. Mfululizo ukiwa na mafanikio, sura zilizokusanywa zinaweza kuchapishwa tena katika vitabu viitwayo tankōbon. Msanii wa manga (mangaka kwa Kijapani) kawaida hufanya kazi na wasaidizi wachache katika studio ndogo na pamoja na mhariri kutoka kampuni ya kuchapisha. Manga ikiwa maarufu inaweza kubadilishwa kuwa kipindi kinachoweza kutazamwa katika runinga baada au hata wakati ambako inachapishwa, Wakati mwingine manga zinazohusisha filamu zilizopo awali hutunzwa (k.m. Star Wars).

Neno "Manga" hutumika nje ya Ujapani kumaanisha vitabu vya michoro viliyochapishwa nchini Ujapani. Hata hivyo, vitabu vya michoro vilivyoshawishiwa kutoka manga vipo katika maeneo mengine ya dunia, hasa katika Taiwan (manhua), Korea ya Kusini (manhwa) na Jamhuri ya Watu wa China, hasa Hong Kong (manhua). Katika Ufaransa, la Nouvelle manga ina maendeleo kama aina ya bande dessinée (yaani drawn strip) inayotolewa katika mitindo iliyoshawishiwa na manga kutoka Ujapani. Katika Marekani, watu hurejelea vitabu vinavyofanana na manga kama Amerimanga, manga ya dunia, au manga yenye asili ya lugha ya Kiingereza ("original english language manga" - OEL manga).

Orodha ya miji ya Marekani

Hii ni orodha ya miji ya nchi ya Marekani yenye angalau idadi ya wakazi 100,000 (2008).

Peace Corps

Peace Corps (Kiingereza: Kikosi cha Amani; tamka pis kor) ni taasisi ya serikali ya Marekani inayotuma kutuma wananchi wa kujitolea katika nchi za nje kusaidia mambo mbalimbali. Wanaojitolea au voluntia wa Peace Corps, ni raia wa Marekani walio tayari kufanya kazi nje ya nchi katika zoezi kwa shirika kwa kipindi ya miezi ishirini na saba. Kwa ujumla, kazi zao zinahusiana na maendeleo ya kimataifa. Kuna shughuli za elimu, biashara, teknolojia ya habari, kilimo, na mazingira zinazotekelezwa hasa.

Utume wa Peace Corps inajumuisha shabaha tatu, ambayo ni

kutoa misaada ya kiufundi,

kuwasaidia watu nje ya Marekani kuelewa utamaduni wa Marekani,

kuwawezesha watu wa Marekani kuelewa utamaduni wa nchi nyingine.

Ni iliundwa na Mtendaji Order 10924 tarehe 1 Machi 1961, na aliyeidhinishwa Congress 22 Septemba 1961, na kifungu cha Sheria ya Peace Corps (Public Sheria 87-293). Sheria ya Peace Corps asema madhumuni ya Peace Corps kuwa:

"Ili kukuza amani na urafiki duniani kupitia Peace Corps, ambayo inapatikana kwa atafanya nia ya nchi na maeneo ya wanaume na wanawake wa Marekani kwa ajili ya huduma waliohitimu ng'ambo na nia ya kutumikia, chini ya hali ya ugumu ikiwa ni lazima, ili kuwasaidia watu wa kama nchi na maeneo katika mkutano mahitaji yao kwa mafunzo ya wafanyakazi. "

au, kwenye Kiingereza

"To promote world peace and friendship through a Peace Corps, which shall make available to interested countries and areas men and women of the United States qualified for service abroad and willing to serve, under conditions of hardship if necessary, to help the peoples of such countries and areas in meeting their needs for trained manpower."

Tangu mwaka 1961, karibu Wamarekani 200.000 walijiunga na Peace Corps, kuwahudumia katika nchi 139. Sasa hivi mavoluntia elfu 7 wanajitolea duniani. Kwenye EAC, Shirika la Peace Corps linafanya kazi Kenya, Tanzania, Rwanda, na Uganda. Kuna mavoluntia zaidi ya 500 kwa jumla. Wanafanya kazi (na wanaishi kama wafrika wenyeji) kila siku karibu na kila sehemu ya EAC iliotajwa, hata kwenye vijijini vidogo porini kwa muda ya mkataba ya miaka miwili. Kwa 2009 ndani ya Tanzania, Mavoluntia wanafanya kazi mikoa 15.

Mradi mkubwa ya Tanzania na Kenya ni kwa kuleta waliumu wa Sekondari kwa hisabati, scienci, na komputa na kuleta wakufunzi wa Vyuo vya Uelimu kwa komputa na ICT. Tanzania, miradi mingine linahusika mavoluntia wa kufundisha kuhusu afya na mazingira vijijini. Kenya, wankuwana na mradi wa biashara. Miradi yanatengamea na maombi la serekali ya nchi wanapowasiliana serekali ya Merikani. Kwa mfano, Mei 2009, Rais Kikwete alipokutana na Rais Obama kwenye Nyumba Nyupe, akaanza mwanzoni ya mazungumzo kwa kuomba mavoluntia wa Peace Corps mia tatu zaidi kwa nchi yake. Peace Corps inakuwa na historia ndefu na Tanzania: Rais Kennedy alipeleka kikuni cha kwanza ya mavoluntia mpaka Tanzania na Ghana tarehe 28 Agosti 1961 kujibu maombi la Rais Nyerere kwa usaidizi.

Shule ya Afrika Mashariki yoyote inaweza kuomba voluntia kujitolea. Wasiliane ofisi kuu wa Peace Corps kwa nchi yake.

Wapentekoste

Wapentekoste ni jina linalojumuisha Wakristo wanaofuata tapo la Kipentekoste linalolenga kuleta upyaisho katika Kanisa kwa kutia maanani tukio la sikukuu ya Pentekoste ya mwaka uleule wa kifo na ufufuko wa Yesu.Tapo hilo linaungana na Waprotestanti wengine katika kushikilia Biblia ya Kikristo tu na kwa njia yake kumkiri Yesu kuwa Bwana na kumpokea kama mwokozi, lakini pia linasisitiza mang'amuzi binafsi ya Roho Mtakatifu katika maisha ya muumini kama yalivyotokea mwanzoni kadiri ya Matendo ya Mitume ili kuwezeshwa kuishi Kikristo kweli kwa upako wa Roho.

Kwa kuwa wanajitangaza "wameokoka", yaani wameachana na dhambi, kwa Kiswahili wanaitwa pia "Walokole".

Tangu tapo hilo lilipoanza mwaka 1907 huko Marekani, Wapentekoste wameshakuwa zaidi ya milioni 279, mbali ya Wakristo wa madhehebu ya zamani walioathiriwa nalo ambao wanaitwa mara nyingi Wakarismatiki na ambao idadi yao inalingana na hiyo.

Wolfgang Amadeus Mozart

Wolfgang Amadeus Mozart alikuwa mtunzi mashuhuri wa opera na mpigaji wa ajabu sana wa piano kutoka nchini Austria alipolizaliwa katika jiji la Salzburg tarehe 27 Januari 1756.

Enzi za maisha yake mafupi, aliandika zaidi ya tungo 600 za muziki. Watu wanaamini kwamba huyu ni moja kati ya watunzi bora wa muda wote. Alitunga nyimbo kadhaa zikiwemo opera (muziki wenye hadithi) Don Giovanni na Die Zauberflöte (Filimbi ya Ajabu).

Kazi zake alizianza na minuet (dansi) aliyoitunga akiwa na umri wa miaka minne, na alizimalizia kwa kipande chake cha mwisho, Requiem, ambacho alikiacha hajakimaliza.

Mozart alikuja kufariki tarehe 5 Desemba 1791, akiwa na umri wa miaka 35.

Wushu - (Kung Fu)

Wushu (/ˌwuːˈʃuː/), au Kungfu ya Kichina, ni mchezo wa upiganaji ulioanzishwa nchini China. Jina "Wushu" linatokana na maneno ya Kichina (武 "Wu" = kijeshi, kwa Kiingereza military or martial, na 術 "Shu" = Sanaa, kwa Kiingereza arts).

Wushu umekuwa mchezo wa kimataifa kupitia Shiririkisho la Kimataifa la Wushu (IWUF - International Wushu Federation). Shirikisho hili ndilo huendeleza michezo ya kimataifa ya wushu kama vile Michuano ya Dunia ya Wushu inayofanyika kila baada ya miaka miwili tangu shindano la kwanza mwaka wa 1991 Beijing, China.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.