Bahari ya Aegean

Majiranukta kwenye ramani: 39°N 25°E / 39°N 25°E

Aegeansea
Bahari ya Aegean.

Bahari ya Aegean (pia: Aegeis; tamka a-e-ge-is) ni moja kati ya sehemu za Bahari ya Mediteranea. Ipo kati ya Ugiriki na Anatolia (Uturuki).

Kupitia mlangobahari wa Dardaneli imeungana na Bahari ya Marmara, Bosporus na Bahari Nyeusi.

Jina

Jina la bahari hii kwa Kigiriki wanaliita Αἰγαῖον Πέλαγος (Aigaion Pelagos), Kigiriki cha kisasa: Αιγαίο Πέλαγος (Aigaio Pelagos). Kwa jina la Kituruki ni Ege Denizi.

Watu wengi wa kale walikuwa wakifikiria tofauti kuhusu jina hili, kwa nini wameiita Aegean.

Labda lilitolewa kufuata mji wa Aegae, au Aegea, ambaye ni malkia wa Amazoni aliyekufa katika bahari hiyo.

Labda lilitolewa kufuata Aegeus, baba wa Theseus shujaa wa Ugiriki ya Kale. Hadithi za kale zinasema kwamba Aegeus alijiua pale alipofikiria kuwa mtoto wake wa kiume amekufa katika bahari hiyo.

Kuna baadhi ya watu wanasema kwamba jina hili linatoka chimbuko la lugha ndogondogo (neno) αἶγες (aiges) au "mawimbi" .

Historia

Europa Mapa.png Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Bahari ya Aegean kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Aleksander Mashuhuri

Aleksander Mashuhuri (au Aleksanda Mkuu, kwa Kigiriki Μέγας Αλέξανδρος, inayoandikwa kwa alfabeti yetu Megas Aleksandros) aliishi tangu Julai 356 KK hadi tarehe 11 Juni 323 KK.

Mfalme wa Masedonia (336 – 323 KK), anajulikana kama mmoja kati ya amiri jeshi waliofanikiwa kupita wote wengine katika historia ya dunia. Kabla hajafariki kwa umri wa miaka 33 aliteka sehemu kubwa ya dunia iliyojulikana na Wagiriki wa zamani zake, kuanzia Ulaya hadi Bara Hindi na Misri.

Aydın

Aidın (Kigiriki: Αϊδίνιο) ni mji mkuu wa Mkoa wa Aydın wa nchini Uturuki.

Aidın ni kitovu cha mabonde madogo ya Mto Meander kuelekea chini ya Bahari ya Aegean. Mji unafahamika toka zama za kale kwa kuwa na rutuba na mazao mengi. Leo hii zao kubwa lifahamikalo kwa huko ni ile miti ya mifigi, japokuwa eneo linaweza kuotesha baadhi ya kilimo cha mazao mengine tofauti na hayo.

Mji pia una viwanda vidogovidogo na maeneo kadhaa ya kihistoria na vitovu vya utalii. Hali ya hewa ya huko kwa kipindi cha kiangazi huwa na joto sana.

Bahari ya Marmara

Bahari ya Marmara (Kituruki Marmara denizi, Kigiriki: Propontis) ni gimba la maji ya chumvi kati ya Ulaya na Asia ndani ya nchi ya Uturuki. Imezungukwa na nchi kavu pande zote isipokuwa kuna milango miwili miembamba ya kuiunganisha na [Mediteranea] upande wa kusini na Bahari Nyeusi upande wa kaskazini. Milango hii ni Dardaneli upande wa Mediteranea na Bosporus upande wa Bahari Nyeusi.

Urefu wake ni hadi 282 km na upana 80 km. Kina cha maji hufikia mita 1,300 chini ya UB. Eneo lake ni 11,655 km² na 182 km² ni visiwa ndani yake.

Mji mkubwa kando lake ni Istanbul.

Bahari ya Mediteranea

Bahari ya Mediteranea (pia: Bahari ya Kati) ni bahari ya pembeni ya Atlantiki kati ya mabara ya Afrika, Ulaya na Asia ya Magharibi. Eneo lake ni takriban milioni 2,5 km². Kina chake kirefu ni 5,267 m. Ina kanda ya hali ya hewa ya pekee pamoja na mimea na wanyama.

Neno "Mediteranea" limetokana na lugha ya Kilatini likiunganisha maneno ya "medium" (inamaanisha "kati ya, katikati") na "terra" (inamaanisha "bara"). Kwa hiyo neno lenyewe linamaanisha "Bahari katikati ya bara".

Katika lugha ya Biblia Kiebrania iliitwa "Bahari ya Magharibi" au "Bahari Kuu"; Waroma wa Kale waliotwala nchi zote zinazopakana na Bahari ya Mediteranea waliita "mare nostrum" yaani "bahari yetu". Waarabu na Waturuki wanaiita "Bahari Nyeupe" (kwa Kituruki: Akdeniz; kwa Kiarabu: البحر الأبيض al-baHr-al-abyaD)

Dardaneli

Dardaneli (Kituruki Çanakkale boğazi) ni mlango wa bahari katika Uturuki. Zamani za Ugiriki ya Kale na Roma ya Kale ulijulikana kwa jina la Hellespont.

Dardaneli iko kati ya rasi ya Gallipoli upande wa Ulaya na Asia bara. Mlango unaunganisha Bahari ya Mediteranea na bahari ya Marmara. Urefu wa mlango ni 65 km mwenye upana kati ya 1.3 hadi 6 km. Jina la Kituruki hutokana na mji wa Canakkale upande wa mwambao wa Asia.

Wakati wa vita kuu ya kwanza ya dunia Uingereza na Ufaransa walijaribu kushambulia Uturuki hapa. Walishindwa na jeshi lililoongozwa na Mustafa Kemal. Mapigano haya yamejuikana kwa jina la "Gallipoli".

Tangu 1936 mkataba wa Montreux umetawala haki za matumizi kwa meli za mataifa yote.

Kanda ya Aegean

Kanda ya Aegean (Kituruki: Ege Bölges) ni moja kati ya kanda 7 za Uturuki ambazo zimetengwa kwa ajili ya kuhesabia sensa ya wakazi. Ipo kwenye upande wa mgharibi mwa nchi, imepakana na Bahari ya Aegean (Ege Denizi) katika upande wa kaskazini, kanda ya Marmara katika kaskazini, kanda ya Mediterranea katika kusini na kusini-magharibi ni kanda ya Anatolia ya Kati mashariki mwake.

Krete

Krete (kwa Kigiriki Κρήτη, Kríti, matamshi ya kale, Krḗtē) ni kisiwa kikuu na chenye watu wengi zaidi cha Ugiriki, na ni cha tano katika Bahari ya Kati, baada ya Sicily, Sardinia, Cyprus na Corsica.

Pamoja na visiwa vya jirani vya bahari ya Aegean kinaunda mkoa wa Krete (Περιφέρεια Κρήτης), mmoja kati ya 13 ya nchi nzima. Mwaka 2011, mkoa huo ulikuwa na wakazi 623,065.

Mji mkuu na mji mkubwa ni Heraklion.

Krete ni sehemu muhimu ya ustaarabu na uchumi wa Ugiriki ukidumisha upekee wake katika utamaduni (kwa mfano upande wa ushairi na muziki).

Mkoa wa Denizli

Denizli ni jina la kutaja moja kati ya Mikoa ya Uturuki uliopo mjini magharibi mwa Anatolia, nyanda za juu katika pwani ya Bahari ya Aegean. Mikoa ya karibu kabisa na mjini hapa ni pamoja na Uşak kwa upande wa kaskazini, Burdur, Isparta, Afyon kwa upande wa mashariki, Aydın, Manisa kwa upande wa magharibi na Muğla kwa upande wa kusini. Mji upo kati ya ramani hizi za kijiografia 28° 30’ na 29° 30’ E na 37° 12’ na 38° 12’ N. Unachukua eneo za kilomita za mraba zipatazo 11,868, na idadi ya wakazi wapatao 882,938. Hapo awali idadi ya wakazi wa hapa ilikuwa 750,882 kunako miaka ya 1990. Mji mkuu wake ni Denizli.

Mkoa wa Muğla

Muğla ni jina la kutaja mkoa uliopo nchini Uturuki, kwenye upande wa kusini-magharibi mwa nchi, katika pwani ya Bahari ya Aegean. Mji wake ni Muğla.

Mkoa wa İzmir

İzmir ni jina la kutaja moja kati ya Mikoa ya Uturuki uliopo mjini magharibi mwa Anatolia kwenye pwani ya Bahari ya Aegean. Mji mkuu wa mkoani hapa ni Izmir. Mji huu ulianzishwa na Wagiriki Smyrna (Kigiriki: Σμύρνη) kunako karne ya 11 KK. Kwa upande magharibi umezungukwa na Bahari ya Aegean, na imefungamana kabisa na Ghuba ya İzmir. Mkoa umechukua eneo la kilomita za mraba zipatazo 11,973. Takriban watu 3,769,000 wanaishi mjini hapa (makisio ya 2007). Idadi ya wakazi wa hapa ilikuwa 3,370,866 kunako mwaka wa 2000. Mikoa ya jirani na mkoa ni pamoja na Balıkesir katika upande wa kaskazini, Manisa kwa upande wa mashariki, na Aydın kwa upande wa kusini.

Muğla

Muğla ni jina la mji uliopo nchini Uturuki. Huu ni mji mkuu wa Jimbo la Muğla, ambayo imekuja hadi katika pwani ya Bahari ya Aegean upande wa kusini-magharibi mwa nchi. Mji upo m 660 kutoka juu ya usawa wa bahari.

Shingo ya nchi

Shingo ya nchi (ing./gir. isthmus) ni kanda nyembamba ya nchi kavu yenye maji kila upande inayounganisha sehemu mbili kubwa zaidi ya nchi.

Mfano bora ni shingo ya nchi ya Panama inayounganisha Amerika ya Kati na Amerika ya Kusini. Mifano mengine mashihuri ni shingo ya nchi ya Suez baina Afrika (Misri) na Asia halafu shingo ya nchi ya Korintho kati ya rasi ya Peloponesi na Ugiriki bara.

Mara nyingi shingo ni mahali panapofaa kwa kujenga mfereji kwa sababu hapo umbali kati ya magimba mawili ya maji ni ndogo zaidi.

Kwa hiyo shingo za nchi zilizotajwa juu huwa na mifereji yao:

Mfereji wa Panama kati ya Atlantiki na Pasifiki

Mfereji wa Suez kati ya Mediteranea na Bahari ya Shamu (Bahari Hindi)

Mfereji wa Korintho kati ya Bahari ya Adria na Bahari ya AegeanKwa namna ya kinyume shingo la nchi huligana na mlangobahari ambayo ni sehemu nyembamba ya bahari kati ya bara na kisiwa, kwa mfano mlango wa Gibraltar.

İzmir

İzmir, kwa jina la kihistoria Smyrna, ni mji wa tatu kwa ukubwa katika Uturuki, na ndiyo mji wenye bandari kubwa baada ya Istanbul. Upo katika eneo la maji yatokayo Ghuba ya İzmir, katika Bahari ya Aegean.

Huu ni mji mkuu wa Mkoa wa İzmir, ambao una eneo la kilomita za mraba zipatazo 7350.

Mji wa İzmir una wilaya zipatazo kumi. Wilaya hizo ni pamoja na (Balçova, Bornova, Buca, Çiğli, Gaziemir, Güzelbahçe, Karşıyaka, Konak, Menemen, na Narlıdere), ambazo kila moja ni tofauti sana na nyingine.

Kanisa la Smirna ni kati ya yale saba ambayo yaliandikiwa barua katika Ufunuo wa Yohane, kitabu cha mwisho cha Agano Jipya na cha Biblia ya Kikristo. Ndilo linalosifiwa zaidi, hasa kutokana na kiongozi wake, askofu Polikarpo wa Smirna.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.