Anwani ya kijiografia

Anwani ya kijiografia (pia majiranukta ya kijiografia, majiranukta, kwa Kiingereza coordinates) ni namna ya kutaja mahali duniani. Anwani ya kijiografia huelezwa kwa kutaja longitudo na latitudo za mahali fulani.

Dunia hugawiwa katika gredi 360 za longitudo na gredi 180 za latitudo (90° za kaskazini na 90° za kusini).

Latitudo za kaskazini na kusini kwa ikweta zinatofautishwa ama kwa kuongeza herufi "N" (=north au kaskazini) na "S" (south au kusini) au kwa alama za "+" (kaskazini) na "-" (kusini).

Gredi za longitudo zinaanza kuhesabiwa kwenye meridiani ya 0° iliyokubaliwa ni mstari kutoka ncha ya kaskazini hadi ncha ya kusini unaopita katika mji wa Greenwich (karibu na London, mji mkuu wa Uingereza).

Kwa mfano, anwani ya National Theater mjini Accra (Ghana) ni: 5°33'14"N (latitudo) na 0°12'2"W (longitudo).

Anwani inaandikwa mara nyingi kwa njia ya desimali pia na hapa inawezekana kutaja mahali kikakilifu zaidi. Hapo majiranukta vya Ikulu jijini Dar es Salaam ni: -6.815592,39.298204.

FedStats Lat long sw
Maelezo ya latitudo na longitudo.

Matumizi ya anwani ya kijiografia kwenye wikipedia

Wahariri wengi wanaongeza anwani ya kijiografia katika makala zinazohusu miji, kata, majengo au mahali pengine. Katika wikipedia hii tunaweza kutumia kigezo:coord. Inatosha kunakili mfano kutoka ukurasa wa kigezo hiki na kubadilisha tarakimu zilizopo kwa namba zinazopatikana kwa kutumia GeoNames, Google Earth au ramani nyingine inayotuhusu kuona anwani ya kijiografia.

Sciences de la terre.svg Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Anwani ya kijiografia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.

Buffalo, New York

Buffalo ni mji mkubwa wa pili katika New York baada ya New York City. Mji wa Buffalo uko kando la Mto Niagara.

Anwani ya kijiografia ni 42°54'N na 78°50'W. Idadi ya wakazi ni 272,632 (2007). Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mnamo mwaka wa 2007, mji una wakazi wapatao milioni 1.3 wanaoishi katika mji huu. Mji upo m 183 kutoka juu ya usawa wa bahari.

Meya wa mji ndiye Byron Brown aliyechguliwa mwaka wa 2005.

Daraja la Kikwete

Daraja la Kikwete ni daraja la kuvuka Mto Malagarasi nchini Tanzania lililofunguliwa rasminna rais Jakaya Kikwete tarehe 16 Septemba 2015.

Daraja la Kirumi

Daraja la Kirumi ni daraja linalovuka Mto Mara nchini Tanzania.

Daraja la Kyaka

Daraja la Kyaka ni daraja linalovuka mto Kagera nchini Tanzania.

Daraja la Mbutu

Daraja la Mbutu ni daraja chini ya ujenzi nchini Tanzania.

Daraja la Mkapa

Daraja la Mkapa ni daraja linalovuka mto Rufiji nchini Tanzania.

Daraja la Rusumo

Daraja la Rusumoni daraja la kimataifa linalovuka Mto Kagera na kuunganisha nchi jirani za Rwanda na Tanzania.

Daraja la Selander

Daraja la Selander ni daraja ambayo linalovuka mkondo wa Msimbazi nchini Tanzania.

Daraja la Songwe

Daraja la Songwe ni daraja la kimataifa linalovuka Mto Songwe na kuunganisha nchi jirani za Malawi na Tanzania.

GeoNames

GeoNames ni jina la hazinadata ya kijiografia kwenye intaneti. Hadi mwaka 2018 ilikuwa imekusanya tayari majina milioni 25 ya miji, vijiji, vitongoji, mikoa, milima, mito, misitu au maeneo mengine. Kati ya hizo ni sehemu milioni 4.8 zinazokaliwa na binadamu .

Data hizi zimekusanywa kutokana na zile zinazopatikana kutoka ofisi za serikali kote duniani lakini pia na hazinadata za taasisi nyingine kama BBC au Greenpeace. Zinapatikana katika intaneti kwa laiseni huria ya Creative Commons. Data hizo zinaweza kuwa na makosa kwa sababu haijawezekana bado kusanifisha hazinadata zote zilizotumiwa kama vyanzo.

Hata hivyo ni mkusanyo mkubwa wa data kati ya ile inayopatikana kwa umma kimataifa bila mashariti ya kibiashara.

Programu yake inatafuta jina na kuonyesha jina, nchi ambako jina hili linapatikana, "feature class" yaani ni aina gani ya mahali panapotajwa, na anwani ya kijiografia kwa umbo la majiranukta ya digrii, dakika na sekondi. Kutoka hapo ukurasa kwa kila mahali unafunguliwa ukionyesha pia majiranukta ya desimali halafu inawezekana kufungua ramani.

Kanisa la ELCK Kenyoro

Kanisa la ELCK Kenyoro ni mojawapo kati ya makanisa ya kwanza ya Walutheri nchini Kenya.

Kisiwa cha Pasaka

Kisiwa cha Pasaka (kwa Kirapanui: Rapa Nui; kwa Kihispania: Isla de Pascua) ni kisiwa cha Chile katika Pasifiki ya mashariki takriban 3,526 km kutoka mwambao wa Chile.

Anwani ya kijiografia ni 27°09′S 109°25′W.

Mji mkuu ni Hanga Roa.

Kuna wakazi 5,761 (2012).

Majiranukta

Majiranukta (pia: mfumo majiranukta; mfumo majira katesia kufuatana na Rene Descartes) ni mbinu ya hisabati unaoeleza nafasi ya kila nukta katika seti ya namba.

Majiranukta ya kawaida hueleza nafasi ya nukta katika tambarare.

Nafasi zote zinapangwa kwa njia ya majira (majiranukta) 2 yanaoitwa

jira-x jiramlalo

jira-y au jirawimaMajiranukta hupatikana kwa kueleza mistari miwili sulubi, moja ukipita kwenye jira-y na mwingine kwenye jira-x. Inapokutana ni nafasi ya nukta inayoelezwa.

Meridiani ya sifuri

Meridiani ya sifuri (kwa Kiingereza: Prime Meridian, Null meridian, Zero meridian) ni mstari wa meridiani unaokubaliwa kuwa mstari wa rejeo kwa kutaja longitudo za mahali duniani. Tangu mwaka 1884 meridiani hiyo ni mstari unaopita kutoka ncha ya Kaskazini hadi ncha ya Kusini kupitia paoneaanga pa Greenwich mjini London, Uingereza. Mstari wa Greenwich ni sifuri, na mistari zenye umbali wa nyuzi moja hutajwa kuwa nyuzi za longitudo upande wa mashariki au magharibi za sifuri, yaani Greenwich.

Moroni (Komori)

Moroni (Mwandiko wa Kiarabu: موروني) ni mji mkuu pia mji mkubwa wa Komori mwenye wakazi 60,200.

Mji uko upande wa magharibi wa kisiwa cha Ngazija (Grande Comore). Kuna bandari kwa usafiri kwa meli kwenda visiwa vingine vya bahari Hindi pia bara la Afrika ya Mashariki pamoja na uwanja wa kimataifa wa ndege.

Anwani ya kijiografia ni 11°45′S 43°12′E.

Paramaribo

Paramaribo (jina fupi: Par'bo) ni mji mkuu wa Surinam. Ina wakazi 250,000. Iko kando la mto Surinam takriban 20 km kutoka mwambao wa Bahari ya Karibi. Anwani ya kijiografia ni 5°52' N, 55°10' W.

Skopje

Skopje (Kimasedonia: Скопје; tamka: Skopye) ni mji mkuu pia mji mkubwa wa Jamhuri ya Masedonia Kaskazini. Zaidi ya robo ya wakazi wote wa nchi hiyo kukaaa hapa.

Skopje ni kitovu cha uchumi, utamaduni na siasa wa nchi.

Anwani ya kijiografia ni 42°0′N 21°26′E.

Mto Vardar hupita katika mji.

Washington, D.C.

kwa maana mbalimbali ya jina "Washington" tazama Washington (maana)

Washington D.C. ni mji mkuu wa Marekani mwenye wakazi 553,523. Kifupi "D.C." baada ya jina chamaanisha "District of Colombia" ambayo ni mkoa wa shirikisho yaani eneo lililotengwa moja kwa moja kwa vyombo vya shirikisho la Marekani kwa sababu maeneo mengine ya Marekani yako chini ya majimbo mbalimbali yanayojitawala.

Jina la mji mkuu limechaguliwa kwa heshima ya kiongozi wa uhuru na rais wa kwanza George Washington. Jina la "District of Colombia" likachaguliwa kwa heshima ya Kristoforo Kolumbus mpelelezi wa Amerika.

Mji wa Washington uko kando la mto Potomac kati ya majimbo ya Maryland na Virginia. Uko karibu na pwani la mashariki la Marekani. Hori ya Chesapeake ya Atlantiki iko 35 km kutoka mji. Anwani ya kijiografia ni 38°53'42"N na 77°2'12"W.

Washington D.C. ni tofauti na jimbo la Washington lililopo upande wa magahribi wa Marekani.

Hapa ni makao rasmi ya Bunge la Marekani, ya Rais pamoja na serikali yake na makao ya mahakama kuu. Kuna pia majengo ya kihistoria hata kama Marekani haina historia ndefu pamoja na makumbusho mazuri.

Zagreb

Zagreb ni mji mkuu wa Kroatia. Ina wakazi 973,667 2005. Iko katika kaskazini ya nchi kando la mto Sava kwenye kimo cha 120 m juu ya UB na anwani ya kijiografia ni 45°48′N 15°58′E.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.