Alfabeti

Alfabeti ni kiasi cha alama zinazotumiwa kuandika sauti za lugha fulani. Alama hizi hupatikana kama orodha kwa ufuatano uliokubaliwa, kwa mfano katika Kiswahili: "a, b, ch, d, dh, e, f, g, gh, h, i, j, k, kh, l, m, n, ny, ng', o, p, r, s, sh, u, t, th, v,w, y, z".

Jina la "alfabeti" hutokana na mwandiko wa Kigiriki ambamo herufi mbili za kwanza ni α "alfa" na β "beta".

Alfabeti ni mtindo wa mwandiko uliosambaa duniani kote. Kwa lugha nyingi imechukua nafasi ya miandiko ya awali.

Alfabeti huonyesha sauti si maneno kamili - hii ni tofauti na mwandiko kama Kichina wenye alama kwa ajili ya neno lote.

Mifano ya Alfabeti

Alfabeti inayotumiwa zaidi kimataifa ni alfabeti ya Kilatini (au "alfabeti ya Kirumi"). Lakini kuna alfabeti nyingine kadhaa zinazojulikana kimataifa kama vile:

Mengine ni alfabeti kama vile ya Kikopti, ya Kigeorgia, ya Kiarmenia n.k.

Abugida

Aina za pekee za alfabeti ni miandiko ya "abugida". Hii inamaanisha namna ya kuandika ambako hakuna alama za pekee kwa ajili ya vokali. Kila alama ya konsonanti ina namna mbalimbali ya kuonekana kwa kuongeza alama ndogo inayoonyesha ni vokali ipi inayofuata. Mifano yake ni

  • Devanagari au alfabeti ya Kihindi
  • Alfabeti ya Kiethiopia
Globe of letters.svg Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Alfabeti kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Mifumo ya mwandishi duniani
Mifumo ya mwandishi duniani
Alfabeti:  Kilatini ,  Kikirili ,  Kilatini pamoja na Kikirili ,  Kigiriki ,  Kigeorgia na Kiarmenia 
Abjadi:  Kiarabu ,  Kiarabu pamoja na Kilatini ,  Kiebrania pamoja na Kiarabu 
Abugida:  Kihindi ya Kaskazini ,  Kihindi ya Kusini ,  Kiethiopia ,  Kithaana   Mwandiko wa kizalendo wa Kanada ,
Alama kwa neno lote na alama za silabi:  Alama za neno lote ,  Mchanganyiko wa alama za maneno na silabi ,  Mchanganyiko alfabeti na silabi   Mchanganyiko alfabeti na silabi 
Alfa

Alfa (kwa Kiingereza: alpha) ni herufi ya kwanza ya Alfabeti ya Kigiriki. Inaandikwa Α (herufi kubwa ya mwanzo) au α (herufi ndogo ya kawaida).

Katika Ugiriki ya Kale ilihesabiwa pia kama namba "1".

Jinsi ilivyo kawaida na herufi mbalimbali za Kigiriki inatumiwa kama kifupi kwa ajili ya dhana mbalimbali katika hesabu na fisikia. Kundinyota hili limejulikana hasa kama jina la pembe ya kwanza katika pembetatu.

Katika astronomia inatumiwa kuanza hesabu ya nyota katika kundinyota. Kwa mfano nyota yetu jirani katika ulimwengu inaitwa "Alfa Centauri". Imeitwa hivyo kwa sababu inang'aa kushinda nyota zote za kundinyota ya Centaurus. Inayofuata ni "beta Centauri" na kadhalika.

Alfa ikiwa herufi ya kwanza ya alfabeti ya Kigiriki hutumiwa pia kwa kutaja mwanzo. Hivyo ni kinyume cha mwisho au omega. Usemi wa Biblia ya Kikristo hujulikana kuhusu Mungu kuwa ni "Alfa na Omega, mwanzo na mwisho" (Ufunuo wa Yohane 21:6).

Alfabeti ya Kigiriki

Alfabeti ya Kigiriki ni mwandiko maalumu wa lugha ya Kigiriki. Herufi zake zilitumika pia kama tarakimu na sasa hutumiwa kimataifa kama alama za kisayansi.

Alfabeti ya Kilatini

Alfabeti ya Kilatini (pia: Alfabeti ya Kirumi) inatumiwa kwa lugha nyingi duniani. Hata Kiswahili huandikwa siku hizi kwa herufi za Kilatini kama kwa mfano kwenye ukurasa huu wa wikipedia.

Beta

Beta (Kigiriki: Βήτα, Β/β) ni herufi ya pili katika alfabeti ya Kigiriki. Ilikuwa pia na maana ya alama kwa namba 2. Inaandikwa Β (herufi kubwa ya mwanzo) au β (herufi ndogo ya kawaida).

Katika Kigiriki cha kale ilitaja sauti ya "B". Katika Kigiriki cha kisasa imekuwa alama ya sauti "V".

Jinsi ilivyo kawaida na herufi mbalimbali za kigiriki inatumiwa kama kifupi kwa ajili ya dhana mbalimbali katika hesabu na fizikia. Imejulikana hasa kama jina la pembe ya pili katika pembetatu.

Katika falaki inatumiwa sana kwa hesabu ya nyota katika kundinyota. Katika mfumo wa Bayer inataja nyota angavu ya pili katika kundinyota fulani. Kwa mfano nyota yetu jirani katika ulimwengu inaitwa "Alfa Centauri". Imeitwa hivyo kwa sababu inang'aa kushinda nyota zota za kundinyota la Centaurus. Inayofuata ni "Beta Centauri" na kadhalika. Hivyo Rasi Madusa (en:Algol) ilipokwa jina la Bayer "Beta β Persei" kwa sababu ni nyota angavu ya pili katika kundinyota laFarisi (Perseus).

Katika programu za komyuta "toleo la beta" (=beta-version) humaanisha toleo la awali la programu. Wahariri wanaitoa kama imeshakamilika lakini kabla ya kuiuza wanatoa nakala kwa majaribio ili makosa yaonekana.

Gamma

Gamma ni herufi ya tatu katika Alfabeti ya Kigiriki. Inaandikwa Γ (herufi kubwa ya mwanzo) au γ (herufi ndogo ya kawaida). Zamani ilikuwa pia alama kwa namba 3.

Asili ya gamma ni herufi ya Kifinisia ya gimel (tazama makala ya G). Matamshi yake ni kama G ya Kiswahili.

Jinsi ilivyo kawaida na herufi mbalimbali za kigiriki inatumiwa kama kifupi kwa ajili ya dhana mbalimbali katika hesabu na fizikia. Imejulikana hasa kama jina la pembe ya tatu katika pembetatu.

Katika fizikia gamma ni alama kwa fotoni hasa mnururisho mkali aina miali ya gamma.

Katika astronomia inatumiwa kuanza hesabu ya nyota katika kundinyota. Katika mfumo wa Bayer inataja nyota angavu ya tatu katika kundinyota fulani.

Herufi

Herufi ni alama katika mwandiko unaofuata alfabeti. Kila herufi ni alama ya sauti au fonimu fulani kama vile A - B - C. . Kifinisia na Kigiriki zilikuwa lugha za kwanza zinazojulikana zilitumia mtindo huu.

Miandiko iliyotangulia muundo huu ilikuwa na alama moja kwa silabi moja yaani mwandiko wa silabi.

Muundo mwingine tena ni alama moja kwa neno moja jinsi ilivyo hadi leo katika Kichina. Faida ya herufi za alfabeti ni ya kwamba alama chache zinatosha kwa kuandika lugha yote. Katika mwandiko wa Kichina mwanafunzi anahitaji kujifunza alama mamia kabla hajaanza kuandika kitu.

Herufi zinazotumiwa zaidi duniani ni zile za alfabeti ya Kilatini. Alfabeti nyingine zinazotumiwa kimataifa ni hasa alfabeti ya Kiarabu na alfabeti ya Kikirili. Herufi zao zatofautiana kwa jumla ingawa kuna pia herufi zinazofanana katika kundi la alfabeti. Kwa mfano alfabeti za Kilatini na Kikirili zote zimetokana na alfabeti ya Kigiriki.

Vilevile alfabeti ya Kiarabu ina herufi za nyongeza ikitumiwa kwa kuandika lugha kama Kiajemi, Kiurdu au lugha za Kiturki.

K

K ni herufi ya 11 katika katika alfabeti ya Kilatini ambayo ni pia mwandiko wa Kiswahili cha kisasa. Asili yake ni Kappa ya alfabeti ya Kigiriki.

Kigiriki

Kigiriki (pia: Kiyunani) ni lugha ya Kihindi-Kiulaya inayotumiwa hasa nchini Ugiriki. Maandishi yake yamejulikana tangu miaka 3500 iliyopita. Hakuna lugha nyingine duniani inayozungumzwa hadi leo yenye historia ndefu kuliko hii, isipokuwa Kichina.

Kigiriki ni muhimu sana kwa utamaduni wa kisasa kwa sababu ya kutoa michango mingi kwa lugha ya sayansi, teknolojia na utamaduni. Fikra nyingi muhimu zilionekana mara ya kwanza kwa Kigiriki na falsafa iliyojadiliwa na kuandikwa kwa lugha hii. Istilahi nyingi za kisayansi zimetoka katika Kigiriki.

Alfabeti ya Kigiriki ilikuwa msingi wa alfabeti nyingine mbili, za Kilatini na Kikirili, pia kwa miandiko ya abijadi kama herufi za Kiarabu au za Kiebrania. Kiswahili huandikwa leo kwa herufi za Kilatini.

Kati ya maandiko muhimu ya Kigiriki ni yale ya wanafalsafa kama Plato na Aristoteles na pia baadhi ya maandiko ya Biblia ya Kikristo (Agano Jipya pamoja na Deuterokanoni), mbali ya tafsiri ya kwanza ya Biblia ya Kiebrania maarufu kwa jina la Septuaginta (karne ya 2 KK).

Kati ya karne ya 3 KK hadi karne ya 6 BK Kigiriki kilikuwa lugha ya kimataifa katika eneo kubwa la kandokando ya bahari ya Mediteranea pamoja na Mashariki ya Kati.

Lugha imeendelea kubadilika kisarufi, kimatamshi na pia kimsamiati. Hivyo Kigiriki cha kale kimekwisha, hakizungumzwi tena na watu, lakini bado kinafundishwa katika shule na vyuo vingi, hasa Ulaya.

Leo hii katika nchi ya Ugiriki kuna lugha ya Kigiriki Kipya kinachoendela kuandikwa kwa herufi zilezile.

Kikyrili

Kikyrili ni aina ya mwandiko au alfabeti inayotumiwa kuandika lugha mbalimbali za Ulaya ya Mashariki na Asia ya Kati, kwa mfano Kirusi, Kiserbia, Kitajiki.

Jina limetokana na mmonaki na mtalaamu Mgiriki Mt. Kyrilo (827 - 14 Februari 869) aliyesemekana aliunda namna hiyo ya mwandiko kwa ajili ya lugha za Kislavoni pamoja na mdogo wake Mt. Methodio.

Kilatini

Kilatini ni lugha ya kihistoria ambayo siku hizi haina tena wasemaji kama lugha ya kwanza, lakini bado hufundishwa katika shule na vyuo na hata kutumiwa kama lugha ya pili. Ilikuwa pia lugha ya kimataifa ya elimu na istilahi nyingi za kisayansi zimetoka katika Kilatini.

Kilatini kilikuwa lugha hai takriban kati ya miaka 500 KK na 600 BK na baadaye lahaja zake mbalimbali ziliendelea na kukomaa kuwa lugha za pekee zinazojulikana kama lugha za Kirumi.

Kilatini ni pia jina la mwandiko au aina ya herufi (alfabeti ya Kilatini) inayotumika kwa lugha nyingi duniani. Hata Kiswahili huandikwa siku hizi kwa herufi za Kilatini kama kwa mfano ukurasa huu wa Wikipedia.

Kilikuwa

lugha ya Dola la Roma (angalia pia Roma ya Kale)

lugha mama ya lahaja zilizoendelea kuwa lugha za Kirumi kama Kiitalia, Kifaransa, Kihispania, Kireno, Kiromania n.k.

lugha ya elimu na sayansi katika Ulaya kwa karne nyingi

lugha rasmi ya serikali katika nchi nyingi za Ulaya kati ya mwisho wa Dola la Roma mwaka 476 BK hadi mnamo 1700 BK

lugha pekee ya liturgia katika Kanisa la Kilatini hadi mwaka 1965Hadi leo ni

lugha ya kidini katika Kanisa Katoliki

lugha rasmi katika nchi ya Vatikano.

Kilatini ina athira kubwa katika lugha ya sayansi na elimu. Hadi leo hufundishwa mashuleni hasa Ulaya.

Kiswahili kimerithi maneno yenye asili ya Kilatini hasa kupitia Kiingereza kilichopokea karibu asilimia hamsini ya maneno yake yote kutoka Kilatini kupitia hasa Kifaransa. Maneno mengine ya Kilatini yameingia Kiswahili kupitia Kireno, Kifaransa n.k.

Kilatini huendelezwa na kukuzwa na wapenzi wa lugha. Kuna misamiati ya "Kilatini cha Kisasa" yenye maneno kwa ajili ya mitambo ya kisasa, mtandao n.k. Wikipedia ya Kilatini ilifikia makala zaidi ya 130,000 kwenye mwaka 2019.

Kirusi

Kirusi (русский язык russkii yazik) ni moja kati ya lugha za Kislavoni cha Mashariki yenye wasemaji wengi kati ya lugha zote za Kislavoni. Kirusi huandikwa kwa alfabeti ya Kikyrili.

Kirusi ni lugha rasmi katika Urusi na pia katika nchi jirani za Belarus, Kazakhstan na Kirgizia. Wasemaji wa Kirusi wako katika nchi zote zilizokuwa sehemu ya Umoja wa Kisovyeti hadi 1991. Kuna pia Warusi katika nchi za magharibi kwa sababu wakati wa Ukomunisti kulikuwa na wakimbizi waliotoka nje ya Urusi kwa sababu za kisiasa.

Watu wengi duniani wamejifunza Kirusi kwa sababu ilikuwa lugha ya kimataifa kati ya nchi zilizoshikamana na Umoja wa Kisovyeti. Wanafunzi wengi kutoka nchi mbalimbali za Afrika walipata elimu ya juu kwenye vyuo vikuu vya Umoja wa Kisovyeti kwa lugha ya Kirusi.

Kituruki

Kituruki (Türkçe) ni lugha rasmi nchini Uturuki. Ni lugha yenye wasemaji milioni 80. Hivyo ni lugha yenye wasemaji wengi kati ya Lugha za Kiturki zinazozungumzwa na watu milioni 170 katika Asia ya Magharibi na Asia ya Kati.

Kuna wasemaji nchini Uturuki, kwenye kisiwa cha Kupro, Bulgaria, Ugiriki, Masedonia na katika nchi kadhaa zilizokuwa sehemu za Dola la Uturuki. Kutokana na uhamiaji wa Waturuki kuna pia wasemaji mamilioni katika nchi za Umoja wa Ulaya.

Wasemaji wa kituruki huelewana kwa kiasi kikubwa na wasemaji wa Kiazerbaijan, Kiturkmen na Kiqashgai.

Wasemaji wa lugha za kiturki ziliingia katika eneo la Uturuki ya leo tangu mwaka 1000. Wakati wa Dola la Uturuki lugha yao ilikuwa lugha ya utawala na fasihi andishi.

Hadi Atatürk Kituruki kile kilitumia maneno mengi ya Kiarabu na Kiajemi kikaandikwa pia kwa Alfabeti ya Kiarabu. Tangu mwaka 1923 lugha imeandikwa kwa alfabeti ya Kilatini na maneno yenye asili ndani ya Kituruki yalitafutwa.

M

M ni herufi ya 13 katika alfabeti ya Kilatini ambayo ni pia mwandiko wa Kiswahili cha kisasa. Asili yake ni Mi ya alfabeti ya Kigiriki.

Maandishi

Maandishi (pia: mwandiko) ni tendo la kushika sauti za lugha kwa njia ya alama zinazoandikwa.

Mikoa ya Uturuki

Uturuki imegawanyika katika mikoa ya takriban 81, inaitwa il kwa Kituruki (wingi wake ni iller, tazama alfabeti ya Kituruki kwa maelezo zaidi).

Namba za Kiroma

Namba za Kiroma (kwa Kiingereza: Roman numerals) ni mfumo wa tarakimu kwa kuandika namba jinsi ulivyokuwa kawaida wakati wa Roma ya Kale na katika mwandiko wa Kilatini. Mfumo huu unaendelea kutumika hadi leo kwa namba za pekee, hasa katika muundo wa orodha ambako mgawanyo ni wa ngazi mbalimbali. Ni kawaida kwa kutofautisha watu wenye jina lilelile, kwa mfano wafalme au mapapa: Malkia Elizabeth II (= wa pili) au Papa Benedikto XVI (= wa kumi na sita).

Orodha ya mito nchini Tanzania

Orodha ya mito nchini Tanzania inaitaja zaidi ya 2,000, lakini hiyo ni baadhi tu.

Imepangwa kwa taratibu mbalimbali kama ifuatavyo:

kadiri inavyoelekeza maji yake katika Bahari ya Hindi mashariki mwa nchi ama moja kwa moja ama kwa kuchangia Mto Zambezi kupitia Ziwa Nyasa, lakini kuna pia mito michache inayochangia Bahari ya Kati kupitia Ziwa Viktoria na mto Naili, na mingine tena Bahari Atlantiki kupitia Ziwa Tanganyika, huku mingine inaishia katika mabonde nchini kama la Ziwa Rukwa;

kadiri ya mikoa inapopatikana;

kadiri ya alfabeti.

Orodha ya mito ya Ethiopia

Mito ya Ethiopia ni mingi; humu imeorodheshwa baadhi tu pamoja na matawimto:

kulingana na beseni lake (kadiri inavyoelekeza maji yake katika Bahari ya Kati au katika Bahari ya Hindi au katika maziwa na mabonde ya ndani)

kadiri ya alfabeti.

Ugiriki

Ugiriki (pia: Uyunani; kwa Kigiriki: Ελλάδα, Ellada, au Ελλάς, Ellas) ni nchi ya Ulaya Kusini-Mashariki katika kusini ya rasi ya Balkani.

Imepakana na Albania, Masedonia Kaskazini, Bulgaria na Uturuki.

Upande wa kusini-magharibi na kusini-mashariki kuna pwani ndefu kwenye Bahari ya Mediteranea.

Baharini huko kuna visiwa vingi sana ambavyo ni sehemu za Ugiriki.

Ugiriki ni nchi yenye historia ndefu na maarufu sana, hata inaitwa "nchi mama ya Ulaya".

Lugha ya Kigiriki inaendelea kuandikwa kwa Alfabeti ya Kigiriki inaotumiwa tangu miaka 3000 iliyopita, lakini lugha yenyewe imebadilika. Wagiriki wa leo hawaelewi tena Kigiriki cha Kale moja kwa moja.

Wakazi wengi wanafuata dini ya Ukristo, hasa katika Kanisa la Kiorthodoksi la Kigiriki (97%). 1.3% ni Waislamu.

Ugiriki ni nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya tangu 1981.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.