Agano la Kale

Agano la Kale ni mkusanyo wa vitabu vya sehemu ya kwanza ya Biblia ya Kikristo inayotumiwa na waumini wa Ukristo duniani kote. Pengine mkusanyo huu unagawanywa katika makundi kadiri ya mada au mtindo: sheria, historia, ushairi na unabii, ambayo ni tofauti kiasi na kawaida ya Tanakh ya Uyahudi wa leo.

Vitabu vyote vya Agano la Kale viliandikwa kabla ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Kwa mujibu wa wanahistoria wa Biblia, vitabu vya Agano la Kale viliandikwa kati ya karne ya 11 KK na karne ya 1 KK.

Entire Tanakh scroll set
Vitabu vyote vya Biblia ya Kiebrania.

Orodha tofauti za vitabu vya Agano la Kale

Katika mapokeo ya Kikristo kuna orodha tofauti za vitabu vya Agano la Kale. Hasa kuna matoleo yenye vitabu 39 na kuna matoleo yenye vitabu 46.

Biblia ya Kiebrania au Biblia ya Kigiriki?

Asili ya mahesabu haya mawili ni hasa desturi tofauti ndani ya Uyahudi wakati wa Yesu na karne mbili za kwanza BK. Kanuni ya Biblia ilikuwa haijafungwa wakati ule. Hivyo palikuwa na mikusanyo tofauti kati ya Wayahudi wenye lugha ya Kiebrania au ya Kiaramu kwa upande mmoja na Wayahudi waliotumia lugha ya Kigiriki kwa upande mwingine.

Wayahudi wenye lugha ya Kigiriki (waliokaa nje ya Palestina, hasa katika nchi mbalimbali za Dola la Roma na kuzidi idadi ya Wayahudi katika Palestina Israeli yenyewe) walitumia toleo la Kigiriki la Septuaginta. Wakristo wa kwanza walizoea toleo hilo hasa kwa sababu lugha ya mawasiliano kati ya Wakristo ilikuwa Kigiriki kama lugha ya kimataifa. Ndiyo sababu Agano Jipya lote liliandikwa kwa Kigiriki.

Upande wa Uyahudi uamuzi kuhusu vitabu vinavyofaa kuhesabiwa kuwa sehemu za Biblia ya Kiebrania lilifanywa kati ya miaka 80 - 135 BK]] ambapo wataalamu Wayahudi waliamua kukubali vitabu vile tu vilivyotunzwa kwa Kiebrania. Hivyo maandiko kadhaa zisizoandikwa kwa Kiebrania vilifungwa nje. Sababu mojawapo ya uamuzi wao ilikuwa kubishana na Wakristo waliovitumia.

Jumuia za Kiyahudi zilipokea uamuzi huo lakini Wakristo waliendelea kutumia Septuaginta, iliyotafsiriwa baadaye kwa Kilatini na lugha nyingine za mataifa na za makabila yaliyopokea imani ya Kikristo.

Hivyo Biblia ya Wakristo ulikuwa na vitabu vya Septuaginta hadi matengenezo ya Kanisa katika karne ya 16.

Martin Luther alianza kutafsiri Biblia upya kutoka lugha asilia akaona achague vitabu vyake, akinyofoa 7 vya Agano la Kale pamoja na vichache vya Agano Jipya kadiri alivyoviona kuwa na mafundisho sahihi kiimani. Hivyo upande wa Agano la Kale alilingana na Wayahudi na kutofautiana na jinsi ilivyokuwa kawaida katika Kanisa Katoliki ambalo katika Mtaguso wa Trento (karne ya 16) lilithibitisha matumizi ya vitabu 46 katika Agano la Kale.

Tangu Luther matoleo mengi ya Kiprotestanti huonyesha vitabu vya Agano la Kale kuwa 39. Mara nyingine vitabu 7 vya Deuterokanoni vinaongezwa baada ya Agano la Kale kama sehemu ya pekee vikiitwa "Apokrifa".

Vitabu vya Agano la Kale

Orodha hii inafuata kawaida ya Wakristo walio wengi. Umbo la majina ni ule wa tafsiri ya "Biblia - Habari Njema kwa Watu Wote". Vitabu saba vinafuatwa na alama ya DK ni vile ambavyo huhesabiwa kando na Waprotestanti wengi kama "Apokrifa" lakini hutazamiwa kama vitabu kamili vya Biblia (Deuterokanoni) katika mapokeo ya Kanisa Katoliki na ya Waorthodoksi wengi.

Vitabu vya Kihistoria

  • 1. Vitabu vitano vya Torati vinavyoitwa pia "vitabu vya Musa":

Vitabu vya Kishairi au vya hekima

Vitabu vya manabii

Viungo vya nje

The10Commandments.png Makala hii kuhusu mambo ya Agano la Kale bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Agano la Kale kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Mwanzo Kutoka Walawi Hesabu Kumbukumbu Yoshua Waamuzi Ruthu Samueli I Samueli II Wafalme I Wafalme II Mambo ya Nyakati I Mambo ya Nyakati II Ezra Nehemia TobitiDK YudithiDK Esta Wamakabayo IDK Wamakabayo IIDK Yobu Zaburi Methali Mhubiri Hekima DK SiraDK Wimbo Bora Isaya Yeremia Maombolezo BarukuDK Ezekieli Danieli Hosea Yoeli Amosi Obadia Yona Mika Nahumu Habakuki Sefania Hagai Zekaria Malaki - Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.

Biblia

Biblia ni jina la jumla kwa ajili ya vitabu vitakatifu vya dini ya Uyahudi na hasa ya Ukristo.

Neno limetokana na lugha ya Kigiriki ambayo ndani yake βιβλία (biblia) ina maana ya "vitabu" ikiwa ni wingi wa βιβλος (biblos). Hii ni kwa sababu Biblia ni mkusanyo wa maandiko mbalimbali yaliyoweza kutungwa kwa muda wa miaka 1000 hivi.

Hivyo Biblia ni tofauti na vitabu vingine kwa sababu iliandikwa na watu mbalimbali ambao hawakuwa pamoja wala hawakuandika kwa wakati mmoja, lakini vitabu vyote vimekusanywa na kuunda kitabu kimoja cha Biblia. Inasadikiwa na Wayahudi na Wakristo kwamba "Biblia ni kitabu kilichoandikwa na watu kwa uwezo wa Mungu".

Tunaweza kutofautisha:

Biblia ya Kiebrania au Tanakh inavyotumiwa na Wayahudi. Vitabu hivyo 39 kwa Kanisa Katoliki na wengineo ni sehemu kuu ya vile 46 vinavyoitwa "Agano la Kale" (wakati Wakristo wengine, hasa Waprotestanti, wanakubali hivyo 39 tu). Ndilo sehemu ya kwanza ya

Biblia ya Kikristo inavyotumiwa na Wakristo yenye vitabu vya Agano la Kale pamoja na Agano Jipya.

Biblia ya Kiebrania

Biblia ya Kiebrania ni namna mojawapo ya kutaja vitabu vitakatifu vya Uyahudi vinavyoitwa na Wayahudi wenyewe "Tanakh". Ndivyo vinavyounda pia sehemu ya kwanza ya Biblia ya Kikristo na kuitwa na Wakristo "Agano la Kale" (vikiwa pamoja na Deuterokanoni au vikiwa peke yake).

Vitabu hivyo, vilivyoandikwa kwa Kiebrania na sehemu ndogo kwa Kiaramu, vinaheshimiwa pia na Wakristo wakiamini ya kwamba ufunuo wa vitabu hivyo ulikuwa hatua ya kwanza iliyokamilishwa baadaye na hatua ya pili au "Agano Jipya" kwa ujio wa Yesu Kristo.

Kuna madhehebu na wataalamu wanaopendelea kuviita vitabu hivyo kwa jina la Biblia ya Kiebrania ili wasisitize usawa wa vitabu vilivyofunuliwa au wasionekane wanavikosea heshima vitabu ambavyo kwa Wayahudi si jambo la "kale".

Hivyo kichwa cha Kilatini "Biblia Hebraica" limekuwa jina la kawaida kwa matoleo ya kitaalamu ya maandiko haya.

Hata hivyo majina "Agano la Kale" na "Agano Jipya" yanapatikana katika Biblia yenyewe (taz. hasa Eb 8).

Biblia ya Kikristo

Biblia ya Kikristo ni mkusanyo wa maandiko matakatifu ya Ukristo. Maandiko hayo mbalimbali yanaitwa tangu zamani sana "vitabu" tu, inavyomaanishwa na neno la Kigiriki βιβλια, "biblia" ambalo ni wingi wa neno "biblos" yaani "kitabu".

Hutofautishwa na Tanakh ambayo ndiyo maandiko matakatifu ya dini ya Uyahudi na ambayo pengine inatajwa kwa jina lilelile la "Biblia", hasa katika matoleo ya Biblia ya Kiebrania. Vitabu vyake vimo katika sehemu ya kwanza ya Biblia ya Kikristo kwa jina la "Agano la Kale".

Biblia ya Kikristo hugawiwa sehemu mbili ambayo ni Agano la Kale na Agano Jipya. Agano la Kale lina maandiko yaliyoandikwa kabla ya Yesu Kristo na vitabu vya Agano Jipya viliandikwa baada yake.

Kitabu cha Baruku

Kitabu cha Baruku ni kimojawapo kati ya vitabu vya deuterokanoni vya Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo.

Kitabu cha Kwanza cha Wafalme

Kitabu cha Kwanza cha Wafalme ni sehemu ya Tanakh (Biblia ya Kiebrania na ya Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo. Hugawiwa katika sura 22.

Kitabu cha Methali

Kitabu cha Mithali kimo katika Tanakh (Biblia ya Kiebrania), hivyo pia katika Agano la Kale la Biblia ya Kikristo ambamo ni cha kwanza kati ya vitabu vya hekima.

Kitabu cha Nahumu

Kitabu cha Nahumu (kwa Kiebrania נחום, Nahum) ni kimojawapo kati ya vitabu 12 vya gombo la Manabii wadogo katika Tanakh (yaani Biblia ya Kiebrania) na kwa hiyo pia katika Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo.

Kitabu cha Pili cha Wafalme

Kitabu cha pili cha Wafalme ni sehemu ya Tanakh (Biblia ya Kiebrania na ya Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo. Hugawiwa katika sura 25.

Kitabu cha Sefania

Kitabu cha Sefania ni kimojawapo kati ya vitabu vya Tanakh (yaani Biblia ya Kiebrania), hivyo kinapatikana pia katika Agano la Kale ambalo ni sehemu ya kwanza ya Biblia ya Kikristo.

Kutokana na ufupi wake kimepangwa tangu kale kati ya vitabu 12 vya Manabii Wadogo.

Kitabu cha Wamakabayo II

Kitabu cha pili cha Wamakabayo ni kimojawapo katika ya vitabu vya deuterokanoni vya Agano la Kale katika Biblia ya Kanisa Katoliki na ya Waortodoksi wengi.

Sawa na Kitabu cha Wamakabayo I kinasimulia upiganaji uhuru wa Wayahudi wakiongozwa na familia ya Wamakabayo katika karne ya 2 KK, lakini hakikuandikwa na mtu yuleyule, ingawa jina lake halijulikani.

Anadhaniwa kuwa Myahudi msomi wa Aleksandria (Misri) au aliyeathiriwa na shule ya uandishi ya Misri.

Ingawa aliandikwa kwa ufasaha katika lugha ya Kigiriki, anaonekana ameshikilia kabisa Torati ya Uyahudi.

Kitabu kinaonekana kimeandikwa mwishoni mwa karne ya 2 KK kwa kufupisha vitabu vitano vya Yasoni wa Kirene (2Mak 2:19-32).

Kinasimulia kwa namna nyingine habari za awali za Kitabu cha kwanza cha Wamakabayo (176 KK - 160 KK); hivyo si mwendelezo wake, bali kinakikamilisha na kuzidisha mtazamo wake wa imani hasa upande wa Hekalu la Yerusalemu.

Kitabu hicho ni muhimu katika maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa Israeli, kwa kuwa kinafundisha uumbaji kutoka utovu wa vyote, ufufuko wa wafu, maombezi kwa ajili ya marehemu, uwepo wa malaika n.k.

Kama vitabu vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Kitabu cha Yona

Kitabu cha Yona ni kimojawapo kati ya vitabu vinavyounda Tanakh (yaani Biblia ya Kiebrania), kwa hiyo pia Agano la Kale, sehemu ya kwanza ya Biblia ya Kikristo.

Kitabu cha Yoshua bin Sira

Kitabu cha Yoshua bin Sira ni kimojawapo kati ya vitabu vya deuterokanoni vya Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo.

Mwandishi alikuwa Myahudi wa Yerusalemu aliyetunga kitabu chake kwa Kiebrania mnamo miaka 196 KK - 175 KK huko Aleksandria (Misri).

Halafu mjukuu wake alikitafsiri kwa Kigiriki akitanguliza dibaji. Wakatoliki na Waorthodoksi wanakubali kama Neno la Mungu tafsiri hiyo, si maandiko asili.

Ingawa kitabu hakionyeshi mara moja mpangilio mzuri, kwa kugusagusa mambo mbalimbali, mafundisho yake makuu ni kwamba Hekima, ambayo ni mamoja na Torati, ni sifa maalumu ya Wayahudi;

hao tu wanaweza kumfikia Mungu.

Kitabu kinatoa hasa maadili yanayofanana na yale ya Kitabu cha Mithali.

Kama vitabu vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Kitabu cha Yuditi

Kitabu cha Yudith ni kimojawapo kati ya vitabu vya deuterokanoni vya Biblia ya Kikristo.

Kimo katika Septuaginta na katika Agano la Kale la Kanisa Katoliki, la Waorthodoksi wengi na la baadhi ya Waprotestanti, lakini si katika Tanakh ya Uyahudi wala katika Biblia ya Waprotestanti.

Kitabu cha Zaburi

Kitabu cha Zaburi ni kimojawapo kati ya vitabu vya Tanakh (yaani Biblia ya Kiebrania) na kwa hiyo pia vya Agano la Kale ambalo ni sehemu ya kwanza ya Biblia ya Kikristo.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Samueli I

Kitabu cha kwanza cha Samueli kilikuwa sehemu ya kwanza ya Kitabu cha Samweli katika Tanakh (yaani Biblia ya Kiebrania) kabla hakijagawiwa pande mbili kutokana na ukubwa wake.

Kuanzia tafsiri ya kwanza (ya Kigiriki) inayojulikana kama Septuaginta na vilevile katika Agano la Kale la Biblia ya Kikristo kinahesabiwa kama kitabu kinachojitegemea.

Hata hivyo mada yake na ya Kitabu cha pili ni moja: kueleza habari za mwanzo wa ufalme wa Israeli chini ya Samueli aliyewapaka mafuta awaweke wakfu mfalme Sauli halafu mfalme Daudi.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Kwa habari zaidi tazama Vitabu vya Samweli.

Samueli II

Kitabu cha pili cha Samueli kilikuwa sehemu ya pili ya Kitabu cha Samweli katika Tanakh (yaani Biblia ya Kiebrania) kabla hakijagawiwa pande mbili kutokana na ukubwa wake.

Kuanzia tafsiri ya kwanza (ya Kigiriki) inayojulikana kama Septuaginta, halafu katika Agano la Kale la Biblia ya Ukristo, kinahesabiwa kama kitabu kinachojitegemea.

Hata hivyo mada yake na ya Kitabu cha kwanza (Samueli I) ni moja: kueleza habari za mwanzo wa ufalme wa Israeli chini ya Samueli aliyewapaka mafuta awaweke wakfu mfalme Sauli halafu mfalme Daudi.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Kwa habari zaidi tazama Vitabu vya Samweli.

Watakatifu wa Agano la Kale

Watakatifu wa Agano la Kale ni watu walioishi kabla ya Kristo ambao wanaheshimiwa na Wakristo wengi, na pengine na Waislamu n.k.

Baadhi yao ni:

Abeli

Abrahamu

Adamu

Amosi

Ana (mama wa Samweli)

Aroni

Baruku

Daudi

Elisha

Elia

Eva

Ezekieli

Gideoni

Hagai

Henoko

Hezekia

Hosea

Isaka

Isaya

Melkisedek

Mika

Musa

Nahumu

Nathani

Nuhu

Obadia

Raheli

Rebeka

Ruthu

Samweli

Sara

Sefania

Yakobo Israeli

Yeremia

Yoeli

Yona

Yoshua

Zekaria

Wimbo Ulio Bora

Wimbo Ulio Bora (kwa Kiebrania שיר השירים, Shir ha-Shirim), ni kitabu kimojawapo cha Tanakh (Biblia ya Kiebrania) na hivyo pia cha Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Wokovu

Wokovu kwa jumla unamaanisha kuondolewa hali isiyopendeza au ya hatari kabisa.

Kwa namna ya pekee, katika Ukristo Historia ya Wokovu ni wazo la msingi: maana yake ni kwamba, katika mfululizo wa matukio ya dunia hii, Mungu anawakomboa binadamu kutoka dhambi zao na kutoka matokeo yake katika maisha ya duniani na katika uzima wa milele.

Biblia ya Kikristo inatamka kuwa neema ya Mungu ndiyo inayookoa watu, kwa kuwa hao hawawezi kujikomboa peke yao, lakini wanapokea wokovu kama zawadi (neema, dezo) kwa njia ya imani.

"Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu" (Waraka kwa Waefeso 2:8).

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.